Kampuni ya mabasi ya Scandinavia Express ni kampuni pekee ya kitanzania iliyowahi kutokea kwa kuwa na huduma za uhakika na za viwango vya hali ya juu kabisa kulinganisha na huduma zinazotolewa na kampuni za sasa. Kampuni hii ilijijengea jina kubwa na sifa nzuri ndani na nje ya nchi kwa huduma bora walizokuwa wakizitoa kwa abiria wake na pia kuliletea sifa taifa la Tanzania kwa kujulikana kuwa na mabasi ambayo ni quality na high class.
Kampuni ya Scandinavia ilianzishwa zaiidi ya miaka thelathini na tano (35) iliyopita ikiwa na mabasi machache tu aina ya LEYLAND na ilipofika mwaka 1982 kwa mara ya kwanza Scandinavia walinunua basi lao la kwanza la kisasa kutoka kampuni ya SCANIA TANZANIA COACHES aina ya SCANIA ambalo kutokana na ubora wake na uzuri wake kwa kipindi hicho waliamua kulitumia kwa safari yao mpya waliyoianzisha ya Dar es salaam hadi Iringa.
BASI LA KWANZA LA KISASA KUNUNULIWA NA SCANDINAVIA 1982
Kadiri mahitaji ya usafiri yalivyokuwa yakiongezeka ndipo michirizi ya
rangi ya BLUU,KIJIVU na NYEKUNDU ikaanza kuonekana katika mabasi mengi
zaidi yaliyokuwa yakisafirisha abiria karibia kila kona ya Tanzania.
Ilipofika mwaka 2001 kampuni ya Scandinavia walianzisha safari yao ya
kwanza kabisa kutoka nje ya nchi kwa safari ya Dare es salaam hadi
Nairobi nchini Kenya,ambapo mafanikio ya ruti hiyo yalipelekea kuzaliwa
kwa ruti nyingine kati ya Nairobi hadi Mombasa na Mombasa hadi Dar es
salaam. Katika mwaka wa 2002 kampuni ya Scandinavia walipanua wigo wa
huduma zao kwa kuanza ruti mpya ndani ya Afrika mashariki kwa safari za
Dare es salaam hadi Kampala nchini Uganda.
Ilipofika mwaka 2003 kampuni ya Scandinavia ilipanua wigo zaidi kwa kuanza kwenda katika mji mkuu wa nchi ya Zambia Lusaka. Wakati huo wote kampuni ya Scandinavia ilikuwa chini ya mkurugenzi na mwanzilishi wake MR.MUHAMED ABDULLAH. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Kampuni ya Scandinavia ilianza kutumia mabasi ya kisasa mwaka 1982 na
kuanzia hapo walikuwa wakiongeza mabasi kadili ya mahitaji ya kampuni na
abiria pia na kufikia jumla ya mbasi 100 ambayo yalikuwa yakitoa huduma
za usafiri ndani na nje ya nchi na mengi ya mabasi hayo yalikuwa ni ya
kisasa yaliyonunuliwa kutoka kiwanda cha SCANIA na MARCOPOLO kilichopo
nchini BRAZILI.
KWA HISTORIA HII FUPI YA KAMPUNI YA SCANDINAVIA WAMILIKI WA MABASI
WANATAKIWA AJIFUNZE KUWA NA HUDUMA BORA NA ZA VIWANGO VYA HALI YA
KUMFANYA ABIRIA ASINUNG'UNIKE .
TAZAMA PICHA MBALIMBALI ZA MABASI YA KAMPUNI YA SCANDINAVIA HAPA CHINI!
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Chanzo: Tanzania Bound Buses Blog
3 comments:
No one can provide such service. We all miss this quality service.
Kampuni iliyokuwa inajali wateja wake kwa kila njia
Serikali ingewatazama wawekezaji wazawa kama hawa
Post a Comment