Saturday, May 03, 2014

ABSALOM KIBANDA AFUNGUKA NDANI YAMAANDIMISHO YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI

DSC_0017
Baadhi ya waandishi wa habari na wadau kutoka asasi mbalimbali nchini wakifanya usajili kwenye kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.
Na Waandishi Wetu, Arusha
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda ametoa wito kwa waandishi wa habari nchini kuyapa uzito matukio yanayowatokea waandishi wa habari na kuyapigia kelele kwa nguvu zote ili kuyakomesha.
Kibanda aliyasema hayo jana mjini Arusha katika kongamano lililoandaliwa kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani na kuongeza kwamba wakati umefika kwa waandishi wa habari kuondoa tofauti zao na kuungana pamoja kuongeza nguvu waliyonayo kukabiliana na ukatili unaoendelea dhidi ya waandishi wa habari katika miaka ya hivi karibuni.
“Baadhi ya wahariri huwa hawayaandiki madhila yanayowasibu waandishi wa habari na kuyapa uzito unaostahili aidha kwa huyapuuzia au kudharau kwa kuwa hayawahusu moja kwa moja,” alisema Kibanda.
Aliongeza kwa kusema kuwa vyombo vya habari mara nyingi vimekuwa vikinyooshewa vidole na kulaumiwa kwa kutokufanya kazi kwa uadilifu jambo ambalo linatafsiriwa kuwa ni la uonevu, vinatumiwa vibaya na hakuna anayesimama kuvitetea kutokana na mchango wake mkubwa katika jamii. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
DSC_0053
Afisa Mipango Kitengo cha Mawasiliano, Habari na Tehama UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, akiwasilisha mada kuhusu mchango wa uhuru wa vyombo vya habari katika utawala bora, kukuza uwezo na kupunguza umaskini kongamano la waandishi wa habari lilioandaliwa kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yanayofanyika jijini Arusha.
“Kwa sasa tasnia hii iko kwenye wakati mgumu sana kwani hata marais wa nchi mbalimbali mfano Uganda, Kenya hata Marekani wanakinzana na vyombo vya habari kwa madai kuwa kauli zao zinapotoshwa, laikini ukweli ni kwamba ni vyema kauli hizo za viongozi zikachunguzwa kwa undani zaidi ili kuelewa iwapo zina uwajibikaji ndani yake,” alisema Kibanda. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Kibanda aliongeza kuwa wakati umefika sasa kwa waandishi kutambua kuwa kuna ajenda za siri zilizojificha dhidi ya uteswaji wa waandhishi wa habari hivyo yasidharauliwe, yafanyiwe kazi kwa kina ili kuelewa kiini cha tatizo kwa kupata ufumbuzi.
Kwa upande wake mwandishi mkongwe na aliyetunukiwa tuzo ya maisha mwaka 2012 na Baraza la Habari Hamza Kasongo alisema vyombo vya habari vina nguvu kubwa katika kushawishi hivyo vitumie nguvu hiyo kama muhimili wa nne wa nchi katika kuzikabili changamoto zilizopo.
“Kuwe na mtandao unaoeleweka wa mawasaliano kati ya waandishi wa habari nchini ili kuhakikisha kuwa matatizo yaliyopo yanatatuliwa bila woga na kwa ujasiri kwa lengo la kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa,” alisema Kasongo.
DSC_0060
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kitivo cha Sheria , Bw. James Jesse, akitoa mada kuhusu umuhimu wa sheria katika kulinda haki ya uhuru wa kujieleza kwa kila mtu wakati wa kongamano la waandishi wa habari lilioandaliwa kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani yanayofikia kilele leo jijini Arusha.
Mwanahabari mwingine mkongwe Dokta Samwilu Mwaffisi aliyetoa mada ya Maadili ya Uandishi wa Habari alisema kuwa kuna haja ya waandishi kuzingatia uhuru wa habari walionao kwa kuzingatia maadili yanayowaongoza ili kuboresha heshima waliyonayo katika jamii kwa kuandika ukweli na uhakika, bila upendeleo, kutoa fursa ya kujitetea na kukubali kuomba radhi pale unapokosea.
“Kuandika habari zenye kuzingatia maadili kunapunguza manung’uniko, mashauri na kuongeza heshima ya chombo cha habari na mwanahabari mwenyewe,”
Akizungumzia suala la ufanisi, Rais wa Vilabu vya Waandishi wa Habari, Kenneth Simbaya, aliwaasa waandishi wa habari kusimamia ukweli katika kazi zao na kuacha kufanya kazi kwa mazoea jambo ambalo litakawaweka huru zaidi katika utekelezaji wa shughuli zao za uandishi wa habari.
Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na umoja wa asasi mbalimbali chini ya uenyekiti wa MISA TANZANIA unafikia kilele chake tarehe 3 Mei kwa kuzindua majarida mbalimbali, matamko kutoka asasi mbalimbali na kuhitimishwa kwa tafrija ya chakula cha jioni chini ya mgeni rasmi Jaji Mstaafu Mheshimiwa Mark Bomani.
DSC_0341
Mwanahabari Mkongwe kutoka Chuo Kikuu Huria, Dokta Samwilu Mwaffisi (kulia) akiwasilisha mada ya Maadili ya Uandishi wa Habari kwenye kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha. Kushoto ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Iringa, Bw. Simon Berege.
DSC_0311
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda, akitoa maoni yake wakati wa kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.
DSC_0079
Pichani juu na chini ni baadhi ya waandishi wa habari wakongwe, mabalozi na wanahabari washiriki katika kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.
DSC_0028Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
DSC_0283Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
DSC_0371
Mwandishi wa Habari Chokonozi, Bw. Fredrick Katulanda, akielezea madhila mbalimbali yaliyomsibu katika utekelezaji wake wa kuandika habari za uchambuzi.
DSC_0119
Mwanahabari Mkongwe Bi. Leila Sheikh akichangia mada ya Mchango wa Uhuru Wa Vyombo Vya Habari Katika Utawala Bora, Kukuza Uwezo Na Kupunguza Umaskini wakati wa kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
DSC_0348
Mmiliki wa Gazeti tando la Mjengwa na Kituo cha Redio Kwanza Jamii, Bw. Maggid Mjengwa akielezea jinsi Intaneti inavyoweza kuunganisha mtandao wa Redio.
DSC_0339
Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania (COMNETA) na Mkurugenzi wa kituo cha mawasiliano Sengerema, Bw. Felician Ncheye akichangia mada.
DSC_0386
Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Mama Rose Haji Mwalimu, (kushoto) akiwa na baadhi ya washiriki wa Kongamamo hilo.
DSC_0310
Rais wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Kenneth Simbaya, akishiriki kwenye kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.
DSC_0281
Picha juu na chini Baadhi ya washiriki wakichangia maoni yao kwenye kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.
DSC_0322
DSC_0214
Kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 likiendelea.
DSC_0164
Mwanakamati wa maandilizi ya maadhimisho ya Kongamano la Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014, Usia Nkhoma Ledama wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda nje ya ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa AICC jijini Arusha.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...