Serikali ya afrika Kusini imekanusha taarifa za vyombo vya
habari kwamba aliyekuwa kiongozi wa afrika Kusini, Nelson Mandela,
ambaye amelazwa hospitali tangu mwezi wa Juni, kwamba alirejeshwa
nyumbani Johannesburg Ijumaa usiku.
Taarifa
ya serikali imesema kuwa Bwana Mandela bado yuko hospitali mjini
Pretoria na kwamba bado mahtuti, lakini hali yake imetulia.
Kulazwa kwa muda mrefu kwa kiongozi huyo kumewatia wasiwasi raia wa taifa hilo na ulimwengu kwa jumla.
Mandela
ambaye ana umri wa miaka 95, alikuwa Muafrika wa kwanza kuwa rais wa
taifa la Afrika Kusini, na anaheshimiwa na wengi kama baba wa taifa.
No comments:
Post a Comment