Maajabu
mengi sana hugundulika duniani kila siku , lakini kuna kila uwezekano
kuwa ajabu lililoko kwenye story hii likawa ajabu la kipekee .
Mwanasheria mmoja ambaye ni raia wa Kenya ameibuka na kuzishitaki
serikali za Israel na Italia kwa kosa la kuhusika kwenye kifo cha Yesu
Kristo .
Mwanasheria
huyo Dola Indidis amefungua kesi hiyo kwenye mahakama ya dunia The
Hague kule kule ambako rais wa taifa Lake (Kenya ) Mh Uhuru Kenyatta na
Makamau wake William Ruto nao wana kesi ya kujibu .
Mwanasheria
huyo amesema kuwa lazima serikali za mataifa hayo ziwajibike kwa
kitendo cha unyama alichofanyiwa mwanzilishi wa dini ya madhehebu ya
Kikristo ambaye ni Yesu aliyesulubiwa msalabani pasipo kuwa na hatia
yoyote ya kustahili adhabu hiyo .
Dola
Indidis amefungua shitaka hilo dhidi ya Mfalme wa uliokuwa Ufalme wa
Roma Tiberio pamoja na watawala waliokuwa chini yake wakati huo wakiwemo
Pontio Pilato na Mfalme Herode pamoja na viongozi wa kiyahudi wakiwemo
mafarisayo na masadukayo ambayo kwa pamoja walikula njama ya kumuua
Bwana Yesu .