Baadhi
ya wabunge na wadau wa elimu wametaka Serikali kutoishia kufuta
matokeo ya mtihani wa kidato cha nne, bali iwajibishe Baraza la Mtihani
Tanzania (Necta) kwa kufelisha wanafunzi.
Akizungumza kuhusu kauli ya Serikali kufuta matokeo hayo jana, Mbunge wa Bukoba Vijijini, Jason Rweikiza alisema taarifa ya tume ingekuwa tofauti na ilivyotolewa ilikuwa isababishe vurugu nchini.
“Kauli
hii ya Serikali ndiyo iliyotegemewa na wadau wa elimu, tume wangefanya
vinginevyo tunge-riot (fanya vurugu), kwa sababu matokeo yaliyotolewa
na Necta siyohalisi. Tume imefanya kazi nzuri na kilio cha wanafunzi kimesikika,” alisema Rweikiza na kuongeza:
“Sasa
na hili nalisema bila kificho, Necta lazima wawajibishwe kwa sababu
wanafunzi wanne wamejiua kwa matokeo hayo yasiyo halali, kule kwangu
(Bukoba Vijijini) wanafunzi wamekata tamaa na wanaolewa. Hiyo yote ni
hasara ambayo haina wa kuilipa.”
Aliongeza
kuwa nchi nyingi duniani ikiwamo Marekani, mtihani wa mwisho
hauchukuliwi kama kigezo kwa sababu inategemea mwanafunzi jinsi
alivyoamka siku ya mtihani na kwamba, wanatumia mitihani iliyopita
kufanya tathmini yao.
“Necta
ni aibu tangu uhuru hawajawahi kufanya mambo ya ajabu kama hivi.
Lazima wawajibishwe kwani wanafunzi wamepoteza maisha kwa sababu yao,”
alisema.
Mbunge
wa Ngara, Deogratias Ntukamazina alisema suala la mfumo wa kuweka
viwango haliwezi kuchukuliwa peke yake kwa kusababisha matokeo mabaya.
Ntukamazina
ambaye kitaaluma ni mwalimu, alisema suala la kufeli kwa wanafunzi
analigawa sehemu mbili; taaluma na maslahi kwa walimu.
Ombi
la ziada lazima liangaliwe tofauti na hivi sasa. Serikali inapojaribu
kutumia kigezo kimoja cha upangaji matokeo kuwa ndicho kilichosababisha
kufeli kwa wanafunzi hao.
“Suala la vitabu, vitendeakazi, mazingira ya kazi, walimu kukata tamaa hatutakiwi kupuuza haya mambo,” alisema Machali.
Alisema
suala la maslahi ya walimu lazima Serikali ikae nao hata kama siyo
kiwango wanachotaka, lakini iwaongezee kidogo na kwamba, kufutwa kwa
matokeo hayo ni jambo zuri lakini siyo mwisho wa tatizo, huku akiongeza
kuwa hata alama zikipunguzwa aliyeandika zombi kavaa viatu hatapata
kitu.
“Unabadili
mfumo wa kupanga matokeo na madaraka, mathalan mwaka jana daraja D
ilikuwa alama 35, zamani ilikuwa 21. Hivi hawa wanafunzi umewaandaa kwa
sababu walikuwa wameshajipanga kwa 21, huyu wa Zombi hata ungempa
mtihani kutwa nzima asingeweza kupata hizo alama,” alisema.
Mbunge huyo alisema suala la elimu halitakiwi kufanyiwa mzaha na Serikali inatakiwa kusema ukweli.
SOURCE:::MWANANCHI:::
Mbunge huyo alisema suala la elimu halitakiwi kufanyiwa mzaha na Serikali inatakiwa kusema ukweli.
SOURCE:::MWANANCHI:::
No comments:
Post a Comment