Wakristo wamesema Serikali ya Rais Jakaya Kikwete imeshindwa kuwasaidia ili waishi kwa amani na utulivu katika nchi yao.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodoma, Amon Kinyunyu
Kauli
hiyo ilitolewa jana na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodoma, Amon Kinyunyu, wakati akisoma tamko
la Maaskofu wa madhehebu ya Kikristo Tanzania katika ibada ya Ijumaa
Kuu iliyofanyika katika Kanisa lililopo eneo la Jamatini.
Katika
tamko hilo alilolisoma kwa niaba ya Maaskofu wote, Kinyunyu alisema
kuwa umefika wakati ambao Wakristo wamechoka na vitendo wanavyofanyiwa
na baadhi ya waumini wa dini zingine.
“Tatizo
ni kuwa Serikali inashindwa kuchukua hatua mapema, makanisa
yanachomwa, migogoro inazidi, lakini hakuna hatua zozote ambazo
Serikali inachukua katika kunusuru hali hiyo, tumechoka,” alisema.
“
Serikali imeshindwa kuchukua hatua kwa muda mwafaka kwa kila jambo
ambalo linatokea kwa Wakristo na hata inapoonyesha kuwa imechukua hatua
haionyeshi sana kujali juu ya yale wanayofanyiwa Wakristo. Askofu huyo
alisema kuwa matokeo yanayotokea Zanzibar mathalan, Wakristo wanaoishi
huko yamewasababishia hofu hivyo wengi kuanza kuvikimbia visiwa hivyo
na kukimbilia Tanzania Bara.
Kwa
mujibu wa Askofu Kinyunyu, suala la uchomaji wa makanisa hadi sasa
limeshindwa kupatiwa ufumbuzi na kila kukicha bado makanisa yanaendelea
kuchomwa moto akahoji Serikali kukaa kimya maana yake nini.
Aidha,
tamko hilo limeitaka Serikali kuweka utaratibu mzuri na ufafanuzi wa
kina kuhusu uchinjaji wa nyama ambao umekuwa ni tatizo kubwa hapa
nchini. “Hapa litolewe tamko kila mtu kwa imani yake achinje mwenyewe
siyo kuanza kulaumiana au kumpa haki mmoja akachinja na mwingine
akaachwa. Tunaomba sana ufafanuzi wa kina juu ya suala hilo ili kuondoa
mgogoro baina yetu na wenzetu.”
wamekuwa wakifanyiwa, lakini akasisitiza kuwa wanatakiwa kupigana kwa maombi na ndiyo silaha kubwa ya ushindi.
Katika
hatua nyingine, wakati Wakristo wakiwa na hofu ya kusherehekea Sikukuu
ya Pasaka watu wasiofahamika wamevamia makanisa matatu ya Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Kaskazini na kuvunja ofisi za
wachungaji na wainjilisti.