Thursday, January 22, 2015

MAFURIKO MTWARA, NYUMBA 200 ZAZINGIRWA NA MAJI

Wakazi wa Mtaa wa Kiangu Manispaa ya Mtwara Mikindani wakipita kwenye maji  kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha mkoani humo.

Zaidi ya nyumba 200 zimezingirwa na maji katika Manispaa ya Mtwara Mikindani kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha hasara kubwa ambayo thamani yake bado  haijajulikana.
Kufuatia  hali hiyo Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu ametoa saa 24 kwa wataalam kuhakikisha wanayaondoa maji ndani ya makazi ya watu.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Wilaman Ndile amemwambia mkuu huyo wa mkoa alipotembelea maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko hayo kuwa zaidi ya nyumba 200 zimezingirwa na maji katika mitaa mbalimbali ya manispaa hiyo.
Alisema kuwa hakuna mtu aliyeripotiwa kupoteza maisha kutokana na mafuriko hayo lakini kumetokea uharibifu mkubwa wa mali na vyakula.
 “Mvua kubwa zilizonyesha jana usiku zimeshababisha mafuriko haya…tatizo kubwa mji wetu hauna mifereji ya kupeleka maji baharini…athari ni kubwa sana,” alisema Ndile.
Aliongeza kuwa “Mitaa ya Magomeni, Chuno, Kiangu, Skoya,Kisutu Nabwada ndiyo yaliyoathiriwa zaidi na tatizo hili”
Alia Mussa ni mmoja wa waathirika wa mafuriko hayo kutoka Mtaa wa Kisutu eneo la Nabwada alisema kuwa amepoteza fedha kiasi cha Sh300,000, nguo, chakula na vyombo vya ndani.
“Tunaomba msaada kwa viongozi kunusuru hali hii, tunaona serikali yetu kama imetutupa, hatuna chakula, wala fedha za kununua chakula, kila kitu kimeloa,” alisema Mussa.
Dendegu amewaagiza wataalam wa mipango miji, zimamoto na manispaa kuhakikisha ndani ya saa 24 wanayaondoa maji hayo katika ya makazi ya watu. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

MWIGULU ATII AGIZO LA KINANA, ASITISHA ZIARA ZAKE MIKOANI

Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba 

Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amesitisha ziara zake za mikoani ili kutii agizo alilopewa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana.
Nchemba ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, alisema jana kuwa anawajibika kutekeleza amri hiyo kutoka ndani ya chama.
Alisema agizo hilo halina lengo baya zaidi ya kukijenga chama ili kufikia malengo ikiwa ni pamoja na kuimarisha nidhamu miongoni mwa wanachama.
“Huwa ananituma, anaweza akaniambia nifanye au nisifanye jambo ambalo halina masilahi ya chama,” alisema Nchemba.
Utekelezaji huo umekuja baada ya Nchemba kuandikiwa barua na Kinana ambayo pia imezagaa katika mitandao ya kijamii ikimtaka kusitisha ziara anazozifanya maeneo mbalimbali kwa kuwa hazina baraka za chama hicho.
Katika barua hiyo iliyoandikwa Januari 18, ilieleza Nchemba amekuwa akifanya ziara nyingi katika mikoa na wilaya bila ya ushirikishwaji wa makao makuu, mikoa na wilaya na hasa kamati za siasa.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

TTCL YAFILISIKA

Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura

KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imetangazwa kufilisika, kutokana na kutokuwa na mtaji baada ya mwekezaji, Kampuni ya simu za mkononi ya Bharti Airtel, kushindwa kuwekeza kwa miaka 14.
Kutokana na hatua hiyo, Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC) imeamua kupeleka suala hilo bungeni ili kuweka mipango ya kimkakati kuifufua kampuni hiyo. Kwa kuanzia, Msajili wa Hazina amepewa kazi ya kufanya tathmini ya kina.
Hayo yalibainika jana katika kikao cha uongozi wa kampuni hiyo na kamati hiyo, inayoongozwa na Kabwe Zitto, iliyotaka kufahamu maendeleo ya kampuni hiyo, ambayo kwa miaka mingi imekuwa ikikabiliwa na changamoto kadhaa katika ushindani wa huduma za simu hususani katika siku za mkononi.
Umekuwepo pia mvutano mkali baina ya Serikali na Kampuni ya simu za mkononi ya Bharti Airtel kuhusu hatima ya asilimia 35 ya hisa, ambazo kampuni hiyo inamiliki ndani ya Kampuni ya TTCL. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

JANGA LA TATU JESHI LA POLISI


 
Jeshi la Polisi Tanzania, limekumbwa na janga la tatu katika kipindi kisichozidi miezi saba baada ya watu wanaosadikiwa kuwa majambazi kuvamia na kuua askari wake wawili katika Kituo cha Ikwiriri wilayani Rufiji juzi na kisha kupora bunduki saba na risasi 60.
Tukio hilo limefanya jumla ya askari waliouawa kufikia watano huku bunduki 22 na risasi zaidi ya 120 zikiwa zimeporwa baada ya kuvamiwa kwa vituo vitatu vya polisi tangu Juni 11 mwaka jana.
Mbali na Ikwiriri, vituo vingine vilivyovamiwa ni Mkamba Kimanzichana, Mkoa wa Pwani na Bukombe mkoani Geita.
Matukio hayo yametokea ikiwa ni mwaka mmoja na wiki tatu tangu Ernest Mangu alipoanza kazi ya Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) akimrithi mtangulizi wake, Said Mwema. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

MAKINDA: SIWATAMBUI CHENGE NA NGELEJA...!!!


 
Spika wa Bunge, Anne Makinda akipokea kutoka kwa Balozi wa China hapa Nchini,  Dk LU Youquing baadhi ya vifaa vya Tehama vilivyotolewa na serikali ya China kwa ajili ya kusaidia shughuli za Bunge, katika hafla iliyofanyika kwenye ofisi ya spika Dar es Salaam jana. Kulia ni Kamishna wa Bunge, Dk Maua Daftari.

Spika wa Bunge, Anne Makinda amesema hawatambui wenyeviti wa kamati tatu za kudumu za Bunge ambao Bunge liliazimia wavuliwe nyadhifa zao kutokana na kutajwa katika kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow.
Pamoja na kuwapo kwa maagizo ya Bunge, baadhi yao wanaendelea kujinasibu kuwa bado ni wenyeviti huku mmoja wao akiongoza vikao vya kamati.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Makinda alisema anachofahamu ni kuwa wenyeviti hao tayari wamaeshajiuzulu na kamati zao zinatakiwa kufanya uchaguzi wa wenyeviti wengine.
Wanaotakiwa kuachia nyadhifa zao ni Victor Mwabalaswa (Nishati na Madini), Andrew Chenge (Bajeti) na William Ngeleja (Katiba, Sheria na Utawala), ambaye hadi jana mchana alikuwa akiongoza kikao cha kamati hiyo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

SOMA MAGAZETI YA LEO JANUARI 22, 2015

.

.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

WHATSAPP YAWABANA WATUMIAJI

Mtandao wa WjhatsApp 
 
Mtandao wa kijamii wa WhatsApp unawabana watu wanaotumia huduma hiyo kupitia programu bandia na ambayo haijaidhinishwa ya Android kwa muda wa saa 24.
WhatsApp ambayo inamilikiwa na Facebook, ilisema kuwa imechukua hatua dhidi ya watumiaji wa huduma ya WhatsApp Plus kwa sababu ya wasiwasi kwamba programu hiiyo huenda iksababisha kuvuja kwa taarifa za siri za watumiaji wa WhatsApp.
Programu hio bandia na isio rasmi ya Android inawezesha watumiaji wa WhatsApp Plus kupamba mawasiliano yao wanavyotaka.
Wataalamu wanasema kwamba watumiaji wa Android wanapaswa kuwa makini na kutahadhari kuhusu wanavyodownload programu flani au 'Apps'. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

WATOTO WA HOSNI MUBARAK KUACHIWA

 Aliyekuwa rais wa Misri Hosni Mubarak na wanawe Alaa na Gamal wakiwa kizimbani
 
Mahakama nchini Misri imeamrisha kuachiliwa kwa watoto wa kiume wa rais wa zamani Hosni mubarak wakati wanaposubiri kesi yao pamoja na baba yao inayohusu ufisadi.
Wakili wa Alaa na Gamal Mubarak anasema kwa anatarajia wawili hao kuachiliwa leo.
Hasira kutokana na kile kilichoonekana kama jitihada za kumuandaa Gamal Mubarak kuweza kumrithi babake kama rais ni moja ya sababu zilizosababisha maandamano makubwa yaliyomundoa madarakani rais Hosni Mubarak. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Na BBC

UJUMBE WA UTURUKI SOMALIA WASHAMBULIWA

Hoteli ilioshambuliwa 
 
Kumekuwa na shambulizi la mlipuaji wa kujitolea muhanga katika hoteli moja mjini Mogadishu nchini Somali ambapo maafisa wa Uturuki walikuwa wakijiandaa kumlaki rais Recep Teyyip Erdogan.
Takriban raia watatu wa Somali waliuawa wawili kati yao wakiwa maafisa wa usalama wakati gari lililojaa vilipuzi lilipogonga lango la hoteli.
Uturuki hatahivyo imesema kuwa hakuna mjumbe wake aliyejeruhiwa na kwamba ziara ya rais Erdogan itaendelea kama ilivyopangwa siku ya ijumaa.
Kundi la wapiganaji wa Alshabaa limesema kuwa lilitekeleza shambulizi hilo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

TUNISIA KUTOANA JASHO NA ZAMBIA

Afcon
 
Zambia italazimika kuimarisha safu ya kati katika mechi didi ya Tunisia kufuatia jeraha la mchezaji Nathan Sinkala ambalo limemuweka nje ya michuano yote ya mataifa ya Afrika.
Hatahivyo kikosi hicho cha Chipolopolo hakina tatizo kubwa juu wachezaji wake.
Mkufunzi wa Tunisia ana wachezaji wa kutosha wa kujumuisha katika timu yake,ijapokuwa wamekuwa na tatizo katika hoteli yao.
Kunako mwendo wa saa nane leo alfajiri ,kulikuwa na maji chungu nzima katika vyumba vya hoteli wanaolala wachezaji wa kikosi hicho.
Inadaiwa kuwa wachezaji hao walilazimika kubadili vyumba huku wachezaji wengine wakilazimika kulala wanne katika chumba kimoja. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Wednesday, January 21, 2015

KANISA KATOLIKI LAUNGA MKONO MAANDAMANO DRC

maandamanoDRC
 
Mkuu wa kanisa katoliki nchini Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo ameunga mkono maandamano ya kupinga mabadiliko katika ya sheria ya uchaguzi ambayo imezua siku tatu za maandamano.
Kadinali laurent Monsengwo ameitaka mamlaka kwa maneno yake mwenyewe kusitisha mauaji ya raia wake. Amewataka waandamanaji kuweka amani.

Makundi ya haki za kibinaadamu yamesema kuwa zaidi ya watu 40 wamefariki katika ghasia hizo.
Vyama vya upinzani vinasema kuwa sheria hiyo iliyopendekezwa ililenga kuchelewesha uchaguzi ili rais Joseph Kabila aendelee kuwa mamlakani baada ya kipindi chake cha utawala kuisha mwaka ujao. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

MWANAJESHI WA UK HATIANI KWA KUMBAKA MTOTO

Ikiwa atapatikana na hatia mwanajeshi huyo atafungwa jela miaka 10 
 
Mwanajeshi mwingereza ameshtakiwa kwa kosa la kumbaka na kumdhalilisha mtoto mwenye umri wa miaka 6 nchini Austria.
Viongozi wa mashitaka wanasema kuwa mwanajeshi huyo ambaye hajatajwa alikamatwa mwezi Novemba katika eneo la Tyrol ambako alikuwa anafanya mazoezi yake ya kijeshi.
Anatarajiwa kufikishwa mahakamani tarehe 10 mwezi Machi.
Msemaji wa kiongozi wa mashtaka alisema kua wendeshja mashtaka wanaamini kwamba mwanajeshi huyo aliingia nyumbani kwa familia ya msichana huyo akiwa mlevi nyakati za asubuhi na kufanya kitendo hicho.
Mwanajeshi huyo alipatikana katika chumba cha mtoto huyo baada ya babake kusikia kelele.
Alikamatwa mjini Neustift na ikiwa atapatikana na hatia huenda akafungwa jela miaka 10.
Msemaji wa kiongozi wa mashtaka aliambia BBC kuwa mtoto huyo alihojiwa na kiongozi wa mashitaka. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Na BBC

TAZAMA PICHA ZA SAMATTA KATIKA MAJARIBIO CSKA MOSCOW

15922_870694186307442_880608052995095050_n 
Hatimaye nyota ya mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe Mbwana Samatta imeanza kung’ara katika anga ya kimataifa ya soka.
Taarifa zilizothibitishwa ni kwamba mshambuliaji huyo yupo kwenye majaribio katika klabu ya CSKA Moscow – moja ya klabu kubwa kabisa nchini Urusi ambayo kwa miaka kadhaa imekuwa ikitawala soka la nchi hiyo na kucheza katika michuano ya mabingwa wa ulaya.
10690055_930864356931841_364362052221467735_n
Samatta alipewa nafasi ya kufanya majaribio ya siku 3 na klabu hiyo kwenye kambi yao ya mazoezi iliyopo Spain, lakini sasa ameongezewa wiki moja ya ziada ili maofisa ya jopo ya ufundi la timu hiyo wapate muda wa kumuangalia vizuri.
10689498_930864360265174_71847191900962169_n
Pamoja na CSKA Moscow – timu nyingine ambazo zinatajwa kumtaka mshambuliaji huyo ni Inter Milan na Udinese za Italia, Atletico Madrid ya Spain, FC Basel ya Uswis na Kaiserslauten ya Ujerumani. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

TAMBWE ASIMULIA ANAVYOTESWA, YANGA YASHITAKI

muro 2
Klabu ya Yanga imepanga leo kuwasilisha malalamiko yao juu ya tukio la kunyanyaswa kwa mshambuliaji wake Amissi Tambwe kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lakini pia mchezaji husika amefafanua kwa kina juu ya manyanyaso anayoyapata.
 
Akizungumza mchana wa leo katika makao makuu wa klabu hiyo Mkuu wa Kitengo cha Habari Jerry Muro amesema uongozi wao unakusudia kuwasilisha malalamiko yao hayo ambayo mengi yametokana na vitendo alivyofanyiwa Tambwe wikiendi iliyopita katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting ambapo wanataka mapendekezo yao manne yafanyiwe kazi.
Muro amesema kwanza Yanga ingwetaka kuona TFF inawachukulia hatua kali wahusika wote waliomdhalilisha Tambwe huku pili wakilitaka shirikisho hilo kutoa hadharani taarifa ya tathimini ya waamuzi wa mchezo huo lengo likiwa ni kujua umakini wa waamuzi hao. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
muro
“Tatu tungewaomba wenzetu wa TFF kwa kuwa wao wapo kimya pia kuwachukulia hatua wahusika wote waliosimamia mchezo huo kwa kushindwa kubaini haya ambayo vyombo vya habari imeyafichua lakini ikiwezekana wafungiwe na Yanga hatuwataki kuwaona wanachezesha mechi zetu vinginevyo tutagoma na hata Ruvu nao tungependa kuona wanapewa adhabu kwa viongozi wao kushabikia maovu haya.
Aidha Tambwe mwenyewe amechukizwa na matukio hayo akisema ameshangazwa kuona anafanyiwa vitendo vya kinyama ambapo mengine hawezi kuyaweka hadharani.
“Mpira ni starehe mimi sikatai mchezaji anikabe lakini ni jinsi gani unanikaba hapo ndiyo tatizo, naambiwa mimi mkimbizi hivi hawa wenzangu wanajua maana na haya maneno yapo mengi ambayo nimedhalilishwa nayo kiungwana siwezi kuyaweka wazi hapa lakini viongozi nitawaeleza,”alisema Tambwe. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

KLABU KUJIGHARAMIA HOTELI MICHUANO YA CAF

NGASA 
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limefanyia marekebisho kanuni zake za michuano ya ngazi ya klabu kwa upande wa malazi ambapo sasa timu zitachagua na kujilipia zenyewe hoteli zinapokuwa kwenye mechi za ugenini. Kabla ya marekebisho ya kanuni hiyo, timu ngeni ilikuwa ikilipiwa hoteli na timu mwenyeji kwa msafara usiozidi watu 25. CAF ilikuwa imepitisha hoteli maalumu katika kila nchi ambapo mwenyeji alitakiwa kuziweka timu ngeni.
Kwa marekebisho hayo, Chama cha Mpira wa Miguu cha nchi mwenyeji kitakuwa na wajibu wa kuitafutia hoteli timu ngeni iwapo tu kitaombwa kufanya hivyo, lakini jukumu la kulipia malazi litakuwa la timu yenyewe.
Mwaka huu Tanzania inawakilishwa na timu mbili za Azam na Yanga katika michuano ya CAF. Azam inacheza Ligi ya Mabingwa (CL) ambapo itaanzia nyumbani Februari 15 mwaka huu kwa kuikaribisha El Merreikh ya Sudan kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.
Nayo Yanga itacheza michuano ya Kombe la Shirikisho (CC), na imepangiwa kucheza mechi ya kwanza nyumbani dhidi ya BDF IX ya Botswana. Mechi hiyo itafanyika Februari 14 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...