Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbroad Slaa akizungumza na wenyeviti wenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), James Mbatia (kulia) na Ibrahim Lipumba baada ya kumaliza kuzungumza na waandishi wahabari kuhusu mchakato wa Katiba na Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa), umemtaka Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba (BMK), Samuel
Sitta kusitisha vikao vya Bunge sasa mpaka mwafaka utakapopatikana kwa
kuwa kuendelea kwake kunahalalisha ulaji wa fedha za walipakodi.
Akisoma tamko la vyama hivyo mbele ya wanahabari
jana, Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, James Mbatia, alisema: “Ukawa tunapaza
sauti zetu, tukisema hapana! Hapana! Haikubaliki.”
Alisema kwa kuwa Rais Jakaya Kikwete na Kituo cha
Demokrasia Tanzania (TCD), wameafikiana kuahirishwa kwa Bunge hilo
kupisha maandalizi ya Bunge la Muungano wa Tanzania, kuendelea kwa BMK
hadi Oktoba 4 ni ufujaji wa fedha za umma.
Mbatia alisema TCD walikubaliana kuwa mchakato wa Katiba hauwezi kufikia mwisho sasa kutokana na mambo kadhaa kutokwenda sawa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz