Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samia Suluhu.
WAKATI Mbunge
wa Bariadi Magharibi (Chadema), John Shibuda akiwasilisha maoni ya
wachache ya Kamati namba 8 ya Bunge Maalum la Katiba linaloendelea na
vikao vyake mjini Dodoma Jumatano mchana, Makamu Mwenyekiti wa Bunge
hilo, Samia Suluhu alimsifu na kusema kuwa mwakilishi huyo wa wananchi
ndiye orijino, ukimuona mwingine ni photokopi.
Shibuda
aliyeingia katika ukumbi huo akipingana na msimamo wa chama chake
kilichoamua kususia vikao hivyo kwa kushirikiana na vyama vya CUF na
NCCR-Mageuzi, alitumia pia nafasi hiyo kuwapiga vijembe viongozi wake,
akisema hana matatizo na Chadema, isipokuwa ana ‘bifu’ na mfumo wa
utumishi wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini.
Akifafanua
kauli yake hiyo, Shibuda anayefahamika kwa mbwembwe na mikogo ya lugha,
alisema yeye ni kama mchezaji wa mpira aliye staa, akiwatolea mfano
Cristiano Ronaldo na Lionel Messi, ambao wanaponunuliwa na timu yoyote,
huenda kwa ajili ya kuiimarisha na si vinginevyo.
Mbunge wa Bariadi Magharibi (Chadema), John Shibuda.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz