Dk. Harrison Mwakyembe.
Sifa hiyo sasa imegeuka na kuonekana sisi ni mabingwa wa kusafirisha dawa za kulevya. Hakika hili la kubobea katika biashara ya dawa za kulevya siyo sifa ya kujivunia hata kidogo mbele ya mataifa.
Hakuna siri wala kificho kwamba Tanzania sasa imejizolea medani za aibu kimataifa kwani katika miaka ya hivi karibuni, imekuwa na sifa ya kuwa moja ya vinara wa biashara ya dawa za kulevya duniani.
Ni aibu na ni sifa inayochafua taswira ya nchi yetu, kwani hivi sasa Watanzania wanaosafiri nje ya nchi wanaficha nyuso zao kwa aibu kutokana na upekuzi wa aina yake wanaofanyiwa na mamlaka za forodha na uhamiaji katika nchi wanazopitia.