NI
siku ya furaha kwa Kanye West! Kim Kardashian amejifungua mtoto wa kike
Jumamosi asubuhi katika hospitali ya Cedars-Sinai Medical Center, Los
Angeles, mtandao wa OMG umethibitisha.
Inasemekana Kardashian,
32, alikuwa na West pembeni mwake wakati wa kujifungua, kumkaribisha
duniani binti yao mwezi mmoja kabla ya muda uliotarajiwa. Tarehe halisi
ya kujifungua ilitazamiwa kuwa Julai 11.
"Kim aliugua Ijumaa
usiku na hatimaye kupata mtoto mapema," chanzo cha hospitali kimeileza
Us Weekly. “Inafurahisha, wote katika hali nzuri!"
Kanye West,
36, na Kim - wote wawili wakiwa ndo mara ya kwanza kuwa wazazi, wamekuwa
wapenzi tangu Aprili 2012. Desemba 30, 2012, West alitangaza kwamba
mpenzi wake alikuwa na mimba wakati wa tamasha lake Atlantic City.
"Simamisha
muziki na wote mpige kelele kwa mama kijacho," alisema West jukwaani
akionyesha kidole kwa Kim ambaye alikuwa mmoja wa watazamaji.
