Thursday, April 05, 2018
Wednesday, April 04, 2018
TAZAMA MUONEKANO MPYA WA MBOWE BAADA YA KUKAA MAHABUSU KWA SIKU SABA
Baada ya kukaa mahabusu kwa siku saba na
kusherehekea sikuu ya Pasaka wakiwa gerezani, Mwenyekiti wa Chadema
Taifa Mhe. Freeman Mbowe pamoja na vigogo wengine sita wa chama hicho
leo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia kwa dhamana, baada ya
kukamilisha masharti.
KIKWETE AINGILIA KATI AFYA YA MZEE MAJUTO, HII HAPA AHADI YAKE
LICHA
ya kufanyiwa upasuaji wa tezi dume bado hali ya staa wa filamu za
Kibongo, Amri Athuman ‘Mzee Majuto’ ni tete ambapo Rais Mstaafu wa Awamu
ya Nne, Dk Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK’, amejitosa baada ya kumuona
alivyodhoofu kwa sasa.
JK na Mzee Majuto walikutana uso kwa
uso wikiendi iliyopita katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar ambako
kulikuwa na shughuli ya utoaji tuzo za filamu zilizojulikana kwa jina la
Tuzo za Kimataifa za Sinema Zetu ambapo walionekana wakiteta kwa dakika
kadhaa kabla ya kila mmoja akaenda kukaa kwenye siti yake.
Mzee Majuto alionekana akiwa amedhoofu
kwani aliingia ukumbini akitembea kwa msaada wa fimbo huku akionekana
kutokuwa mchangamfu kama ilivyo kawaida yake, hali iliyowahuzunisha
mashabiki wake waliokuwa ukumbini hapo.
AGNES MASOGANGE AKWEPA KWENDA JELA BAADA YA KULIPA FAINI
Msanii wa kupamba video za muziki (Video Queen), Agnes
Gerald ‘Masogange’ amekwepa kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kulipa faini ya Sh. milioni 1.5.
Msanii maarufu nchini, Agnes Gerald maarufu Masogange alikutwa na hatia ya
kutumia dawa za kulevya na kuhukumiwa kwenda jela au kulipa faini.
Hakimu wa Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu, Wilbard Mashauri, ametoa hukumu hiyo leo Aprili 3 na kuieleza mahakama kuwa Masogange katika kosa la kwanza amekutwa na hatia ya kutumia dawa za kulevya aina ya heroin na kosa la pili kutumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam.
“Hivyo katika kosa la kwanza, mahakama inamhukumu kwenda jela miaka miwili au kulipa faini ya Sh1 milioni na kwa kosa la pili, amehukumiwa kwenda jela miezi 12 au kulipa faini ya Sh 500, 000,” amesema Hakimu Mashauri.
Februari 17 mwaka jana, aliyekuwa Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro aliwaeleza wanahabari kuwa Masogange amepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kupimwa iwapo anatumia dawa hizo za kulevya.
NUKUU SITA (6) MAARUFU ZA WINNIE MANDELA ENZI ZA UHAI WAKE
Winnie Madikizela-Mandela enzi za uhai wake.
Mwanasiasa na
mwanaharakati aliyepigana dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi Afrika
Kusini Winnie Madikizela-Mandela alifariki dunia Jumatatu akiwa na miaka
81.
Alikuwa mke wa zamani wa rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini
Nelson Mandela lakini alikuwa na msimamo mkali zaidi kumshinda hata Bw
Mandela mwenyewe. Winnie alifahamika sana na wengi kama Mama wa Taifa.
Winnie alikuwa
nembo kuu ya vita dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi, na ingawa sifa
zake ziliingia doa miaka ya baadaye, lakini bado alitambuliwa kama
mtetezi wa wanyonge.
Tuesday, April 03, 2018
MBOWE NA WENZIE KUACHIWA LEO...??!
Viongozi sita wa Upinzani nchini (CHADEMA) wanatarajiwa kuachiliwa kutoka kizimbani baada ya kulipa dhamana, siku ya Alhamisi.
Viongozi
hao akiwemo mwenyekiti Freeman Mbowe,
walishtakiwa kwa uchochezi, kuleta vurugu na kuandamana mwezi wa
Februari mwaka huu.
Alhamisi
iliopita, mahakama ya hakimu mkazi Kisutu iliwapatia dhamana viongozi
hao sita lakini kusema kuwa watasalia rumande hadi kesi leo tarehe 3
Aprili ambapo wataletwa mahakamani kukamilisha masharti ya dhamana.
Wanasiasa
hao hawakuletwa mahakamani katika uamuzi wa dhamana yao huku afisa wa
magereza akiiambia mahakama ni kutokana na gari lililotakiwa
kuwasafirisha kuja mahakamani hapo kuwa bovu.
Miongoni mwa
mashtaka waliyosomewa ni pamoja na maandamano yaliyosababisha kifo cha
mwanafunzi wa chuo cha NIT Akwilina Akwiline. Wanashtakiwa pia kuendelea kufanya mkusanyiko usio halali wilayani Kinondoni shtaka linalowakabili washtakiwa wote.
Monday, April 02, 2018
TAZAMA PICHA ZA NDEGE MPYA YA TATU AINA YA BOMBARDIER Q400 IKIWASILI NCHINI TOKA CANADA
Ndege ya 3 aina ya Bombardier Q400 imewasili leo nchini toka Canada na
kupokelewa na kuzinduliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Tunapenda kuwataarifu wadau wetu kuwa hivi karibuni tutapatikana kwa website ya jambotz.co.tz
MKE WA MANDELA AFARIKI DUNIA AKIWA NA MIAKA 81
Winnie Mandela, mke wa zamani wa Nelson Mandela, ambaye pia alipigana dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini amefariki dunia akiwa na miaka 81. Habari za kifo chake zimethibitishwa na msaidizi wake.
Winnie alizaliwa Oktoba 26, 1936 ingawa yeye na mumewe Nelson Mandela walitalikiana mapema miaka ya 1990, Winnie Madikizela Mandela kama alivyofahamika rasmi alisalia kutoa mchango katika maisha ya Mandela.
Alikuwepo na walishikana mikono alipokuwa akiondoka gerezani baada ya kufungwa kwa miaka 27. Lakini maisha yake pia yalikumbwa na utata. Winnie alikuwa na miaka 20 hivi pale alipojipata katika siasa.
MWIGULU AWAASA MAASKOFU KUHUBIRI INJILI ILI WANANCHI WAWE NA HOFU YA MUNGU KUEPUSHA MATUKIO YA KIKATILI
Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Mwigulu Nchemba akionesha
albam ya "Usife Moyo" ya Rose Muhando, kulia ni Mkurugenzi wa Msama
Promotion Alex Msama na Kushoto ni Rose Muhando wakishiriki tukio hilo
katika Tamasha la Pasaka lililofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba
jijini Mwanza jana jioni
Waziri wa Mambo ya Ndani,Dkt Mwigulu Nchemba akipokelewa na
Mkuu wa Mkoa Mwanza Mh. John Mongela mara baada ya kuwasili uwanja wa
CCM Kirumba,tayari kwa kuzindua tamasha la pasaka kwa mara ya kwanza
chini ya Kampuni ya Msama Promotions Ltd sambamba na uzinduzi wa albamu
ya Muimbaji nyota wa muziki wa Injili Rose Muhanda iitwaya 'Usife Moyo'
yenye jumla ya nyimbo saba.
Baadhi ya Wakazi wa jiji la Mwanza wakifuatilia yaliyokuwa
yakijiri katika tamasha la pasaka mapema jana jioni ndani ya uwanja wa
CCM
Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza ambae pia ni Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. Angelina Mabula
akimtunza muimbaji wa nyimbo za injili Christopher Mwahangila mapema
jana jioni ndani ya tamasha la pasaka.
Waziri Wa mambo ya ndani Mhe. Dkt Mwigulu Lameck Nchemba
amewasihi viongozi mbalimbali wa dini nchini wakiwemo Maaskofu na
Mashekh kutumia muda wao mwingi kwa kutembelea mikoa mbalimbali nchini
kunapotokea zaidi matukio ya kikatili ikiwemo mauaji ili kuhubiri injili
wananchi wawe na hofu na Mungu jambo litakalopelekea kupunguza ukatili
na watu kumjua Mungu.
TANZANIA YASHIKA NAFASI YA 13 KWA NCHI ZINAZOVUTIA UWEKEZAJI
Shirika
la Utafiti la Quantum Global limetoa ripoti ya nchi ambazo zinaongoza
kwa kuvutia uwekezaji barani Afrika ambapo nchi ya Morocco imeshika
nafasi ya kwanza ikifuatiwa na Misri na Algeria.
Nafasi ya nne imeshikwa na Botswana,
Ivory Coast nafasi ya tano, Afrika Kusini nafasi ya sita, Ethiopia
nafasi ya saba, Zambia nafasi ya nane, Kenya nafasi ya tisa na Senegal
ikishika nafasi ya 10.
Ripoti hiyo imeitaja Tanzania kuwa nchi ya 13 kwa kuwa na kuvutia uwekezaji. Nchi 10 ambazo zimetajwa kuwa hazivutii uwekezaji ni;
1. Afrika ya Kati2. Liberia
3. Somalia
4. Eritrea
5. Equatorial Guinea
6. Gambia
7. Sierra Leone
8. Guinea
9. São Tomé and PrÃncipe
10. Zimbabwe
WAZIRI MKUU AZINDUA MBIO ZA MWENGE MKOANI GEITA
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwansha Mwenge wa
Uhuru kuzindua mbio zake kwenye uwanja wa Magogo mjini Geita, Aprili 2,
2018 Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi
Mwenge wa Uhuru kiongozi wa vijana sita watakaokimbiza Mwenge huo,
Charles Kabeho wakati alipozindua mbio za Mwenge wa Uhuru kwenye uwanja
wa Magogo mjini Geita, Aprili 2, 2018. Wapili kulia ni Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Jenista Mhagama. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
SOMA MAGAZETI YA LEO JUMATATU YA PASAKA APRIL 02, 2018 YA UDAKU, MICHEZO NA HARDNEWS
Tunapenda kuwataarifu wadau wetu kuwa hivi karibuni tutapatikana kwa website ya jambotz.co.tz
MPENZI WA CRISTIANO RONALDO APOST INSTAGRAM KWA KISWAHILI
Lugha
ya Kiswahili inazidi kukuwa na kuwavutia watu wengi dunia, jana April 1, 2018
moja kati ya post za mitandao ya kijamii zilizochukua headlines ni post ya
mwanamitindo Georgina RodrÃguez ambaye ni
mpenzi wa staa wa soka wa Real Madrid Cristiano
Ronaldo.
Georgina RodrÃguez ni
mwanamitindo na ndio mpenzi wa sasa wa Ronaldo na wamefanikiwa kupata mtoto
mmoja anayejulikana kwa jina la Alana Martina,
hivyo katika insta story yake amepost picha yake na Ronaldo na kuandika ‘Hakuna Matata’
Msemo wa
hakuna matata ni msemo wa Kiswahili ambao umeonekana kupendwa na umekuwa msemo
maarufu sana kwa wageni wanaopenda kujua lugha ya Kiswahili, huo huwa ni msemo
wao wa kwanza kujifunza lakini haijajulkana bado Georgina
RodrÃguez ameujulia wapi msemo huo.
Subscribe to:
Posts (Atom)