Viongozi sita wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), akiwamo Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe wamefutiwa dhamana na kuwekwa mahabusu katika Kituo Kikuu cha Polisi (Central), jijini Dar es Salaam.
Pamoja na Mbowe, viongozi wengien ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Vincent Mashinji, Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko.
Viongozi hao wameripoti kituoni hapo leo Jumanne Machi 27, saa tatu asubuhi ikiwa ni mwendelezo wa kuitikia wito wa polisi ambao wamekuwa wakiwahoji kwa madai ya kufanya mkusanyiko usio halali Februari 16, mwaka huu.
Wakili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Fredrick Kihwelo wamefutiwa dhamana kwa sababu baadhi ya viongozi walikuwa wanakaidi kuripoti polisi kila wanapotakiwa kufanya hivyo huku Msigwa akiongezwa katika orodha ya viongozi hao baada ya kuhojiwa jana na kupewa dhamana ambayo pia leo imefutwa.