BARAZA la Taifa la Elimu na Ufundi (Nacte) limezuia vyuo 163 kudahili wanafunzi katika kozi mbalimbali ngazi ya astashahada na shahada, baada ya kukutwa na upungufu ikiwako kutokuwa na walimu wenye sifa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Machi 23 Mkuu wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Nacte, Dkt. Annastella Sigwejo amesema walifanya uhakiki kwa vyuo 459, kati ya hivyo 296 ndivyo vimekidhi vigezo vya kutoa elimu kwa kiwango kinachotakiwa.
“Kutokana na hali hiyo hivyo ndivyo vinaruhusiwa kudahili wanafunzi kwa ajili ya kozi mbalimbali ngazi ya astashahada na stashahada kwa muhula wa udahili wa Machi na Aprili mwaka huu.”
Amesema licha ya kwamba vyuo vilivyosajiliwa viko 580 waliamua kujiridhisha kwa kuvifanyia uhakiki ambapo walifanikiwa kuhakiki vyuo 459.