Mama mzazi wa watoto wawili mmoja wa miaka
11 na mwingine 15 wanaodaiwa kubakwa na baba wa watoto hao akilia kwa
uchungu wakati akihojiwa na waandishi wa habari kuhusiana na tukio hilo,
wilayani Kibaha mkoani Pwani.
Mkazi mmoja wa Miembe Saba wilayani Kibaha
mkoani Pwani amekamatwa na polisi akituhumiwa kuwabaka watoto wake
wawili wadogo kwa zaidi ya miaka miwili sasa.
Habari zilizolifikia gazeti hili, zilisema kuwa
katika tukio hilo ambalo limethibitishwa na polisi na watoto wenyewe,
baba huyo alianza kuwafanyia binti zake vitendo hivyo mwaka 2013 kwa
siku ambazo mkewe ambaye nimama wa wasichana hao hakuwapo hadi usiku wa
Machi 19, mwaka huu. Kwa sasa tunayahifadhi majina ya familia hiyo.
Watoto hao mmoja mwenye umri wa miaka 15 anayesoma
darasa la saba na mdogo wake mwenye umri wa miaka 11 aliyeanza kubakwa
akiwa darasa la tatu. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.