Waziri mkuu wa Uingereza, hataendelea tena na wadhfa wake huo, iwapo atarudi madarakani katika uchaguzi mkuu wa mwezi Mei. David
Cameron, ameiambia BBC kuwa, anadhani awamu ya tatu inaweza kuwa ni
kipindi kirefu kwake kukaa madarakani na kiongozi mpya ni vizuri
kuchaguliwa.
Chama kikuu cha upinzani cha Leba kimemshutumu Bwana
Cameron kwa kuonyesha uzembe na kushinikiza muhula wa tatu, kwa chama
chake cha Conservative, hata kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu ujao. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Mabeki wa Coastal Union wakiwahani mpira na wachezaji waAzam wakati
wa mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye uwanja wa
Mkwakwani ,Tangajuzi.Azam ilishinda 1-0.
Mshambuliaji wa Azam FC, Didier Kavumbagu
amesema walihitaji ushindi wa zaidi ya bao moja dhidi ya Coastal Union
ila walikwamishwa na uwanja mbovu wa Mkwakwani na kushindwa kuonyesha
kiwango chao cha juu.
Mechi hiyo iliyochezwa juzi ilimalizika kwa
ushindi wa bao 1-0 kwa Azam na kuendelea kukaa katika nafasi ya pili
kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 36 nyuma ya pointi moja
dhidi ya Yanga wenye 37.
Bao pekee la Azam lilifungwa na mshambuliaji wao,
John Bocco, na Kavumbagu alilazimika kutolewa nje huku nafasi yake
ikichukuliwa na Gaudence Mwaikimba. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’
amewataka wachezaji wenzake kuhakikisha wanafunga mabao mengi na
kutoruhusu bao katika kila mechi watakayocheza kama wana nia ya
kuipokonya ubingwa Azam FC.
Cannavaro alisema katika kipindi hiki ambacho
Yanga na Azam FC zinaeendelea kushindana kileleni mwa msimamo wa Ligi
Kuu kitu pekee kinachotakiwa ni kufunga mabao mengi ili mwisho tofauti
ya mabao inaweza kuamua bingwa.
Cannavaro alisema kwa hatua ambayo ligi imefikia
ni lazima kila mchezaji apambane kuhakikisha timu inamaliza ikiwa bingwa
na si vinginevyo kwani malengo yao msimu huu yalikuwa ni kutwaa taji.
“Inapotokea nafasi ya kufunga tunatakiwa tufunge
pasipo kuangalia kuwa mfungaji ni beki, kiungo au mshambuliaji. Pia
wakati wa kujilinda inatakiwa kila mchezaji ashiriki kuzuia na kulinda
magoli, hapo tunaweza kuwa mabingwa bila wasiwasi.
Njia nzuri zaidi ya kuonyesha hilo ni angalau kufunga mabao mawili kwenye kila mechi mpaka mwisho wa msimu,” alisema Cannavaro.
Cannavaro alisema ushindi walioupata dhidi ya
Mgambo JKT juzi Jumapili, umerudisha morali ya kikosi chao kuelekea
mechi za mwishoni mwa ligi. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Michuano
ya netball ya Afrika ya Mashariki imemalizika Zanzibar huku timu ya
MOICT ya Kenya ikitwaa ubingwa kwa upande wa wanawake baada ya kuifunga
timu ya NIC ya Uganda kwa mabao 32-29.
NIC ndio walikuwa mabingwa
watetezi baada ya kulinyakua kombe hilo mwaka jana katika michuano
iliyofanyika Dar es Salaam. Hii ni mara ya pili kwa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania kuandaa michuano hiyo mara mbili mfululizo, zamu hii ikiwa
ni upande wa Tanzania Zanzibar (visiwani) katika viwanja vya Gymkhana.
Netball,
au mpira wa pete ni mchezo ambao kwa miaka mingi umekuwa ukihusisha
timu za wanawake pekee, lakini katika kuleta usawa (gender balance) kama
ilivyo kwa michezo mingine kama vile mpira wa kikapu (basketball), wavu
na mingineyo, mchezo huo katika miaka ya hivi karibuni, umekuwa
ukishirikisha timu za wanaume katika kuleta hamasa na ushindani.
Kwa
upande wa wanaume, wenyeji Polisi ya Zanzibar waliibuka washindi wa
michuano hiyo ya Afrika Mashariki, baada ya kuwafunga wenzao wa JKU (pia
ya Zanzibar) kwa mabao 38-34 katika mechi ya vuta nikuvute.
Michuano
hiyo hufanyika kila mwaka kwa nchi wanachama kupeana zamu za kuandaa
mashindano hayo. Nchi zilizoshiriki ni wenyeji Zanzibar, Kenya, Uganda
na Tanzania Bara.
Rwanda na Burundi ni sehemu ya jumuiya hiyo ya Afrika
ya Mashariki lakini hawana historia kubwa ya kuwa sehemu ya kuwa nchi
shiriki. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Baadhi ya wachezaji wa kiafrika watakaathirika na sheria hiyo.
Shirikisho
la kanda kanda nchini England FA sasa linakusudia kuandaa sheria
itakayo kupunguza idadi ya wachezaji kutoka nje ya nchi za Umoja wa
Ulaya watakaosajiliwa katika ligi za nchi hiyo.
Mwenyekiti wa
shirikisho hilo Greg Dyke asema kwamba ligi kuu ya England ipo kwenye
hatari ya kutowasaidia wachezaji raia wa Uingereza kama hatua
hazitachukuliwa.
Katika mpango pia itaweka sheria ngumu kwa wachazaji wenye vipaji waliokulia nchini humo.
Mikakati hiyo yote ni ya kuimarisha timu ya taifa ya England ambayo imekuwa haifanyi vizuri kwenye mechi za kimataifa. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
KAMATI maalumu ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), imekamilisha kazi
ya ugawaji wa majimbo 211 ambayo ni sawa na asilimia 88 kati ya majimbo
yote 239, imefahamika.
Wakati hayo yakiendelea, kamati hiyo imeshindwa kuafikiana katika
majimbo 28 ambayo yanasubiri uamuzi wa wenyeviti wa vyama vinavyounda
Ukawa, ambao watamaliza kiporo hicho mwezi huu.
Hatua hiyo imekuja baada ya viongozi wa juu wa umoja huo, kutangaza
mkakati wa kusimamisha mgombea mmoja wa urais na kuachiana majimbo ya
uchaguzi katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba. Ukawa ni umoja ulioanzishwa Februari mwaka jana wakati wa Bunge Maalumu
la Katiba, ukiundwa na vyama vya NCCR-Mageuzi, Chadema, CUF na NLD. Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya kamati hiyo maalumu ya Ukawa,
kiliiambia MTANZANIA jana kuwa kwa muda wa wiki moja sasa, kamati hiyo
imekamilisha kazi hiyo kwa kiwango kikubwa jambo ambalo limeelezwa
linaweza kutoa upinzani mkali kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika
Uchaguzi Mkuu. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Rais
Jakaya Kikwete akiwa na wakuu wa wilaya wapya walioteuliwa hivi karibuni.
RAIS
Jakaya Kikwete ameziagiza mamlaka za ulinzi na usalama kuhakikisha
shughuli ya kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura, upigaji kura ya
Katiba Inayopendekezwa unafanyika kwa amani na wasioitakia mema nchi
wasibadilishe matukio hayo kuwa fujo na kuingiza nchi kwenye vurugu.
Alitoa kauli hiyo juzi wakati akifungua mafunzo elekezi kwa wakuu
wapya 27 wa wilaya walioteuliwa hivi karibuni huku akiwataka kuwa na
ushirikiano na vyama vyote vya siasa.
Alisema kazi ya kuboresha daftari la wapiga kura, imeanzia Njombe na
itaendelea mikoa mingine na kuwataka viongozi hao kuhamasisha wananchi
kujitokeza kwa wingi na kukumbusha maana ya kuwa na kitambulisho cha
kura ambacho kitamwezesha kupiga kura ya maoni na katika uchaguzi mkuu
mwaka huu.
“Wananchi wasipoteze fursa waone haja ya kujiandikisha na watakaokosa
fursa ya kupiga kura hawataipata fursa hiyo tena. Tunataka Watanzania
wenye sifa washiriki kikamilifu kuhimiza wananchi wajiandikishe, na
kupiga kura,” alisema. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
WAKATI
wadau wa usafiri nchini wakipendekeza kushuka kwa nauli za daladala na
mabasi yaendayo mikoani, wamiliki wa mabasi wametishia kufuta utaratibu
wa kutowatoza nauli askari na kuongeza kuwa, hata nauli pungufu za
wanafunzi sasa zitakuwa historia.
Wadau wamependekeza kupunguzwa kwa nauli za mabasi yaendayo mikoani
kwa viwango vya kati ya asilimia 15 na 25 huku wakitaka nauli za
daladala zipungue kutoka Sh 400 hadi Sh 300 kwa njia ya umbali wa
kilometa 10.
Hayo yaliibuka jana wakati wa mkutano wa wadau kukusanya maoni kuhusu
mapitio ya viwango vya nauli za mabasi ya mikoani na daladala kupungua
kutokana na kushuka kwa bei ya mafuta ulioandaliwa na Mamlaka ya
Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra). Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Masheikh na wanazuoni wa Kiislamu, Sheikh
Khamis Mataka akizungumza jijini Dar es Salaam jana kuhusu msimamo wa
taasisi hiyo kuhusu Mahakama ya Kadhi, kuli ni Sheikh Mohamed Idd
Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni
wa Kiislamu Tanzania imejibu hoja zilizotolewa wiki iliyopita na Jukwaa
la Wakristo nchini kuhusu Katiba Inayopendekezwa, Mahakama ya Kadhi na
hali ya usalama na amani ya nchi.
Machi 10, mwaka huu maaskofu kupitia Jukwaa la
Wakristo Tanzania walitoa tamko na kuwataka waumini wao kuipigia kura ya
hapana, Katiba Inayopendekezwa kwa sababu imepatikana kwa njia za hila
na kibabe, jambo ambalo sasa limesababisha mvutano.
Katika tamko hilo lililosainiwa na Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT),
Askofu Dk Alex Malasusa, Mwenyekiti
wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Tarcicius
Ngalalekumtwa na Mwenyekiti wa Kanisa la Pentekoste Tanzania (CPCT),
Askofu Daniel Awet, maaskofu hao walisema uanzishwaji wa Mahakama ya
Kadhi ni uvunjifu wa Katiba na kuwa unahatarisha amani ya nchi. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Wajumbe
wa mashirika ya kiraia wa vijiji vya Tama na Itala kusini mwa tarafa la
Lubero jimboni kivu kaskazini, wanasema kutishiwa na kundi la waasi wa
kihutu toka Rwanda wa FDLR kundi wanao ongozwa na Kanali Kizito.
Vitisho
hivyo vinakuja kutoka uchapishaji wa ripoti wa mashirika ya kiraia
katika sekta hio inayo bainisha hali ya harakati makundi ya waasi na
wanamgambo katika maeneo hayo ambao wanahusika naunyanyasaji dhidi ya
raia.
Baadhi ya wanachama wa vyama vya kiraia katika vijiji vya
Tama na Itala wanasema kua raia katika maeneo hayo wanaishi katika hali
ya mafichoni kwa siku tano sasa kulingana na unyanyasaji kutoka waasi
wanao hishi maeneo hayo hasa FDLR huku wakisema nawaishi kwa tabu
wakilala usiku misituni. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Timu
za England zimetolewa katika kinyang'anyiro cha michuano klabu bingwa
barani Ulaya,baada ya Man City kuchabangwa bao 1-0 dhidi ya Barcelona na
kuondolewa katika mashindano hayo, ilikuwa zamu ya Manchester City
kufuata nyayo za waingereza wenzao kutupwa nje ya mashindano na miamba
ya soka ya Hispania Barcelona. Katika kipute hicho kilichopigwa katika
dimba la Nou Camp.
Wenyeji Barcelona walijipatia bao lao katika
dakika ya 31 baada mchezaji Ivan Rakitic kuitumia vema pasi maridadi
kutoka kwa Leonel Mess. Hadi mwisho wa mchezo Barcelona 1 Man City
hawakupata kitu na kufanya jumla ya matokeo kuwa ni 3-1 baada ya mchezo
wao wa awali vijana wa Manuel Pellegrini kuanguka nyumbani kwa jumla ya
mabao 2-1.
Na huko nchini Ujerumani vijana wa Jurgen Klopp
Borussia Dotmund, ilikiona cha moto baada ya kutandikwa bao 3 kwa
mshangao dhidi ya Juventus ya Italia,katika mtanange huo uliopigwa
katika dimba la Sigunal Iduna Park, mchezaji Carlos Tevez ndiye
aliyepeleka msiba kwa Wajerumani hao kwa kutumbukiza kimiani mabao
mawili.
Dakika tatu tu za mchezo huo zilimtosha Tevezi kufunga bao la
kuongoza kabla ya Morata kuandika bao la pili dakika ya 70 na kisha
Tevez kutikisa tena nyavu katika dakika ya 79. Matokeo ya jumla kati ya
timu hizo mbili yanakuwa ni 5-1 baada ya Juventus kushinda 2-1 katika
mchezo wa awali. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Mkazi wa Tunduma ambae jina lake halikufahamika mara moja akionyesha bomu la machozi ambalo halijatumika alilomnyang'anya askari na kukimbia nalo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akielekezwa kitu na wataalam wa ndege hiyo aliyozindua jana.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu jana alionekana kumpiga
kijembe Katibu MKuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana
aliposema kuwa sasa atakuwa anazurura angani.
Nyalandu alitoa kauli hiyo Dar es Salaam alipozindua ndege nyepesi
(Micro-Light, 5H – Hel), ambayo itatumika kupambana na ujangili katika
Hifadhi ya Taifa ya Selous.
“Karibuni wote, leo tunazururia hapa uwanja wa ndege na ninazindua ndege
hii nyepesi ambayo imetengenezwa Ufaransa, itatumika kupambana na
majangili katika Mbuga ya Selous.
“Kwa maana hiyo sasa tunaanza kuzururia angani kupambana na majangili na
nasisitiza kwamba ndege hii ni mpya kabisa na gharama za uendeshaji
wake ni ndogo kwa vile inatumia petroli,” alisema.
Hivi karibuni Kinana akiwa ziarani mkoani Arusha alimsifia Mbunge wa
Monduli, Edward Lowassa (CCM) kuwa ni mchapakazi lakini Waziri Nyalandu
ni mzururaji.
Akizungumza jana wakati wa uzinduzi wa ndege hiyo ya kupambana na
ujangili, Nyalandu alisema imetengenezwa kwa gharama ya Dola za Marekani
2,040,000 na ina uwezo wa kubeba askari mmoja na rubani.
Waziri Nyalandu alisema ndege hiyo imeundwa kwa usalama wa hali ya juu
kwa kuwekewa puto (parachute) ambalo litatumika kushuka chini iwapo
ndege itaishiwa mafuta angani.
“Itakapoanza kutumika itasaidia kuwabaini majangili, inakwenda kwa
mwendo mdogo iwapo angani hali ambayo inawezesha kuwaona majangili na
kila kinachoendelea ardhini kwa wepesi,”alisema Nyalandu. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Kitendo cha kutupiana mpira kati ya Ofisi ya Bunge, Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuhusu
hatima ya Zitto Kabwe, kimeufanya ubunge wa mbunge huyo kuendelea
kuning’inia huku mwenyewe akitazamiwa leo kueleza anachoita ‘maamuzi
magumu’.
Kutupiana mpira kulijitokeza jana baada ya Spika
wa Bunge, Anne Makinda kusema Bunge linasubiri taarifa rasmi ya
kufukuzwa uanachama kwa mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini kutoka NEC,
ambayo hata hivyo, nayo ilisema inasubiri taarifa kutoka Chadema huku
chama hicho kikisema kinashughulikia kwanza kesi zinazowakabili
wanachama wake wanaotuhumiwa kumpiga aliyekuwa mlinzi wa Katibu Mkuu
wake, Dk Willibrod Slaa.
Wakati Makinda akieleza hayo, taarifa kutoka kwa
watu wa karibu wa mbunge Zitto zilieleza kuwa leo ataibuka bungeni kwa
nia ya kuwaaga wabunge kama alivyoahidi wiki iliyopita. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.