Wednesday, March 11, 2015

HII NDIO ORODHA YA ABIRIA WALIOANZIA SAFARI STENDI KUU MBEYA, NANE NANE, UYOLE NA CHIMALA NA BASI LA MAJINJAH SPECIAL


Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.


Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Thursday, February 19, 2015

HAYA NDIO MAJINA YA WAKUU WA WILAYA WAPYA, PAUL MAKONDA, SHABAN KISSU...!!!

http://jambotz8.blogspot.com/

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete  amefanya mabadiliko ya wakuu wa Wilaya ili kuboresha utendaji kazi.
Mabadiliko hayo yamezingatia kuwepo kwa nafasi wazi ishiri na saba (27) zilizotokana na:

a) Kufariki dunia Wakuu wa Wilaya 3;
b)Kupandishwa cheo Wakuu wa Wilaya 5 kuwa wakuu wa Wakuu wa Mikoa:
c)Kupangiwa Majukumu Mengine wakuu wa Wilaya 7; na
d)Kutengua uteuzi wa Wakuu Wawilaya wengine 12.

katika babadiliko hayo Rais Kikwete amewateua wakuu wapya wa Wilaya 27 kujaza nafasi hizo zilizo achwa wazi.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.


Aidha, Wakuu wa Wilaya siti na nne (64) wamebadilishwa vituo vyao vya kazi na Wakuu wa Wilaya arobaini na mbili (42) wameendelea kubaki katika vituo vyao vya sasa. 
Walio teuliwa ni pamoja na Zelothe Steven (Musoma), Mboni Muhita(Mufundi), Paul Makonda (Kinondoni), Shaabani Kissu (Kondoa)

SOMA MAGAZETI YA LEO FEBRUARI 19, 2015

.

.
.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

OBAMA: VITA DHIDI YA MAAGAIDI SI UISLAM

Rais Barack Obama wa Marekani
Rais Barack Obama ameliambia kongamano dhidi ya misimamo mikali ya kidini akisema kuwa kuwa wako kwenye vita si na Waislamu bali na magaidi waliouchafua Uislamu.
Bwana Obama amesema ni sharti dunia ikabiliane na itikadi zilizopindishwa na makundi kama Islamic State yanayochochea vita na kuwapa vijana mafundisho yenye misimamo mikali ya imani ya kidini .
Ameyasema hayo katika mkutano wa siku tatu unaofanyika mjini Washington ambapo amesema dunia inatakiwa kukabiliana na makundi ya aina hiyo.
Rais Obama ameeleza kuwa manung'uniko waliyonayo vijana lazima yashughulikiwe ili kuondokana na hisia za makundi yenye misimamo mikali ya kiitikadi. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

LIBYA YAOMBA KUONDOLEWA VIKWAZO

Afisa wa Libya katika kikao cha kimataifa
Serikali ya Libya inayotambuliwa kimataifa imeliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuiondolea nchi hiyo vikwazo vya silaha ili kukabiliana na kuzorota kwa hali ya usalama nchini humo.
Akihutubia kikao cha dharura cha baraza hilo, waziri wa mambo ya nje wa Libya,Mohammed al-Dairi amesema hatua hiyo itaisaidia serikali ya Libya kujenga jeshi lake, ili kuwatokomeza Islamic State na makundi mengine ya wapiganaji.
Waziri huyo wa mambo ya nje wa Libya aliungwa mkono na waziri wa mambo ya nje wa Misri Sameh Shoukry, ambaye amesema jumuia ya kimataifa inatakiwa kuisaidia serikali ya Libya ili kuonyesha mamlaka yake nchini humo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

REAL MADRID WANG'ARA LIGI YA MABINGWA

 Cristiano Ronaldo wa Real Madrid akishngilia bao lake katika mchezo wa ligi ya mabingwa kati ya Real Madrid na Schalke uliomalizika kwa Real Madrid kushinda 2-0 
 
Michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, hatua ya kumi na sita bora, iliendelea Jumatano usiku kwa kuzikutanisha timu za FC Basel ya Uswisi na FC Porto ya Ureno katika mchezo ambao FC Basel ndio waliokuwa wenyeji na mchezo wa pili ukiwa kati ya wenyeji Schalke 04 ya Ujerumani dhidi ya mabingwa watetezi Real Madrid ya Hispania.
Tuanze na mchezo wa FC Basel dhidi ya FC Porto. Mpambano huo ulimalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1. Wenyeji FC Basel ndio waliokuwa wa kwanza kujipatia goli katika dakika ya 11 likifungwa na Gonzalez ambalo lilidumu hadi kipindi cha pili, FC Porto waliposawazisha katika dakika ya 75 kwa mkwaju wa penalti iliyofungwa na Danilo baada ya mchezaji wa FC Basel Samuel Walter kuunawa.
Katika mchezo huo ambao ulitawaliwa kwa kiasi kikubwa na wageni, FC Porto wakimiliki kwa asilimia 63% huku wenyeji wakiwa na asilimia 37% ulimalizika kwa mwamuzi wa mchezo huo Clattenburg kuwaonya wachezaji tisa kwa kadi za njano, watano wakiwa ni wa FC Basel na wanne kutoka FC Porto. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Sunday, February 01, 2015

SOMA MAGAZETI YA LEO FEBRUARI 01, 2015

.
.
.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Saturday, January 24, 2015

HIKI NDICHO ALICHOKISEMA PROF. MUHONGO ALIPOTANGAZA KUJIUZULU LEO...!!!

Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhuongo akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhuongo, amejiuzulu wadhifa huo kutokana na kuchoshwa na sakata la Akauti ya Tegeta Escrow.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, Barabara ya Samora, Profesa Sospeter Muhongo amesema ameamua kujiuzulu ili kuwa sehemu ya suluhisho la suala la akaunti ya Tegeta Escrow.

Aidha Muhongo alisema kuwa suala la ankauti ya Tegeta Escrow limekuwa likizungumzwa na kufanya mambo mengine yasiendelee na huku watanzania walio wengi ni masikini wakihitaji umeme na sio kuuliza tegeta Escrow. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Friday, January 23, 2015

HATIMA YA MUHONGO NDANI YA SAA 48 ZIJAZO...!!!

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.

Zikiwa zimebaki siku tatu kabla ya Bunge la Jamhuri ya Muungano kuanza mjini Dodoma, sasa hakuna shaka kwamba Rais Jakaya Kikwete atafanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri wakati wowote kuanzia leo na kabla ya Jumapili (saa 48) kutokana na kukabiliwa na safari ya nje.
Rais anatarajiwa kufanya mabadiliko hayo baada ya kumwondoa Anna Tibaijuka, ambaye alikuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kuhusishwa na kashfa ya uchotwaji fedha kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow baada ya kuingiziwa Sh1.6 bilioni kwenye akaunti yake.
Mwingine ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, ambaye anatuhumiwa kutoshughulikia kwa makini sakata hilo na kusababisha Serikali kupoteza fedha hivyo kuwapo kwa uwezekano mkubwa wa kumvua uwaziri utakaomlazimu Rais kufanya mabadiliko madogo kwenye baraza lake, ikiwa ni miezi isiyozidi mitano kabla ya kuvunja Bunge kupisha Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.
Habari ambazo Mwananchi imezipata zinaeleza kuwa Rais Kikwete anaweza kutangaza mabadiliko hayo wakati wowote kuanzia leo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

HUYU NDO MTANZANIA TAJIRI ANAYE ENDESHA MAGARI YA KIFAHARI NA YA BEI KULIKO MTANZANIA MWINGINE...!!!

Kama ndo machine aliyo nunua safari hii basi katisha aisee maana hii ni one of the most expensive and luxury cars around na hela yake ni ndefu sana. It's confirmed gari kanuna na soon mtaiona mitaa ya kati. Davis yaelekea ni mpenzi sana wa magari mazuri na of course uwezo wa kuyanunua anao cause he works so damn hard. Hongera sana Davis can't wait to see this new toy in Bongo.  Hii ndo inaitwa "Tumia Pesa Ikuzoeee"
Hi ni gari nyingine aina ya Lamborghini anayo miliki mfanyabiashara Davis Mosha huko Bongo.  "Heshima Pesa Shikamoo Makelele"
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

EMIRATES KUMWAGA AJIRA KWA WATANZANIA

Simba Yahya
 Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Simba Yahya

KATIKA kutekeleza moja ya malengo ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa hususan kuwatafutia ajira Watanzania nje ya nchi, Wizara hiyo kupitia Ubalozi Mdogo wa Tanzania uliopo Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu umefanikisha kulishawishi Shirika la Ndege la Emirates kuajiri Watanzania wengi zaidi kuanzia mwaka 2015.
Emirates, moja ya mashirika ya ndege tajiri zaidi duniani, linamiliki zaidi ya ndege za kisasa 280, huku likiwa na safari za uhakika duniani kote.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Simba Yahya alisema shirika hilo litaajiri Watanzania katika kada mbalimbali.
“Wamekubali kuajiri Watanzania katika kada mbalimbali, ambapo maofisa wake wanaosimamia ajira watakuja nchini (Tanzania) Machi 2015 kwa ajili ya kuwafanyia usaili Watanzania watakaoomba kazi hizo na kupata uteuzi wa awali,” alisema.
Aliwataka Watanzania kuchangamkia ajira hizo, ambazo awali zilitangazwa Julai 2014, lakini ni Watanzania wachache tu walioomba na hivyo kutofikia lengo lililokusudiwa.
“Baada ya mazungumzo ya kina, uongozi wa Emirates umekubali kuongeza muda wa kuzitangaza ajira hizo kwa mara nyingine na kupanga kufanya usaili kama ilivyoelekezwa hapo awali,” alisema.
Aliwasisitiza Watanzania wenye sifa na vigezo stahiki, kutumia fursa hiyo kuomba nafasi hizo na pia kujiandaa vyema katika usaili ili wajihakikishe ajira katika soko la ajira la kimataifa.
Kaimu Mtendaji Mkuu kutoka Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESA), Boniface Chandaruba aliwataka waombaji wote kuhakikisha wanapata barua kutoka wakala huo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

SOMA MAGAZETI YA LEO JANUARI 23, 2015


.
.

.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

KAMATI TATU ZA BUNGE ZAMGOMEA MAKINDA


Spika wa Bunge, Anne Makinda (kulia) akiongoza kikao cha Kamati ya Uongozi kinachojumuisha wenyeviti wote wa Kamati za Bunge kilichokutana jana kupanga ratiba ya mkutano wa Bunge unaotarajiwa kuanza vikao vyake Jumanne ijayo. Kikao hicho kilifanyika katika Ofisi Ndogo ya Bunge.

Danadana zimeendelea juu ya utekelezaji wa azimio la tatu la Bunge kuhusu kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow linaloagiza kuwajibika kwa wenyeviti wa kamati zake tatu za kudumu, baada ya juzi Spika wa Bunge, Anne Makinda kukaririwa akisema wameshajiuzulu, lakini wajumbe wake wameibuka jana na kusema hawatafanya uchaguzi hadi watakapopata maelekezo kutoka Ofisi ya Spika.

Azimio hilo ambalo ni moja ya manane ya Bunge hilo linasema: “Kamati husika za Kudumu za Bunge zichukue hatua za haraka na kwa vyovyote vile kabla ya Mkutano wa 18 wa Bunge, kuwavua nyadhifa zao wenyeviti tajwa wa kamati husika za kudumu za Bunge.”

Wenyeviti hao na kamati zao katika mabano ni Victor Mwabalaswa (Nishati na Madini), Andrew Chenge (Bajeti) na William Ngeleja (Katiba, Sheria na Utawala).

Juzi, Spika Makinda aliwaeleza waandishi wa habari kwamba wenyeviti waliotakiwa kuvuliwa nyadhifa zao tayari wamejiuzulu na kamati husika zinatakiwa kufanya uchaguzi kupata wengine wapya. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

CCM YAREJESHA AMANI SUDAN KUSINI

Rais Jakaya Kikwete akiwa na Rais Salva Kiir wa Sudan ya Kusini (kushoto), Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan, Dk Riek Machar (wa pili kulia) na Deng Alor Kuol wakitia saini mkataba wa makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudan Kusini katika Hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha juzi usiku. Nyuma yao ni mjane wa marehemu, John Garang aliyekuwa Mwenyekiti wa SPLM, Rebecca Nyandeng de Mabior na Ofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Thobias Makoba. Nyuma yao wakishuhudia utiaji saini huo ni Makamu wa Rais, Dk Mohamed Ghalib Bilal, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Rais Yoweri Museveni wa Uganda. (Picha na Ikulu).
BAADA ya miezi mitano ya mazungumzo ya kurejesha amani Sudan Kusini yaliyoratibiwa na chama tawala, CCM, hatimaye Rais wa nchi hiyo, Salva Kiir na hasimu wake, Riek Machar wamesaini makubaliano ya kusitisha mapigano, yaliyoibuka tangu mwaka 2011.
Kutokana na machafuko hayo, zaidi ya raia 20,000 wa Sudan Kusini, wamepoteza maisha huku wengine zaidi ya milioni moja wakikosa makazi.
Walisaini makubaliano hayo juzi usiku jijini hapa, huku marais wa ndani na nje ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wakiongozwa na Rais Jakaya Kikwete, wakishuhudia.
Wengine walioshuhudia makubaliano hayo ni Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, Naibu Rais wa Afrika ya Kusini, Cyril Ramaphosa , Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Salva Kiir, Riek Machar na Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...