Michuano
ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, hatua ya kumi na sita bora,
iliendelea Jumatano usiku kwa kuzikutanisha timu za FC Basel ya Uswisi
na FC Porto ya Ureno katika mchezo ambao FC Basel ndio waliokuwa wenyeji
na mchezo wa pili ukiwa kati ya wenyeji Schalke 04 ya Ujerumani dhidi
ya mabingwa watetezi Real Madrid ya Hispania.
Tuanze na mchezo wa
FC Basel dhidi ya FC Porto. Mpambano huo ulimalizika kwa matokeo ya sare
ya bao 1-1. Wenyeji FC Basel ndio waliokuwa wa kwanza kujipatia goli
katika dakika ya 11 likifungwa na Gonzalez ambalo lilidumu hadi kipindi
cha pili, FC Porto waliposawazisha katika dakika ya 75 kwa mkwaju wa
penalti iliyofungwa na Danilo baada ya mchezaji wa FC Basel Samuel
Walter kuunawa.
Katika mchezo huo ambao ulitawaliwa kwa kiasi
kikubwa na wageni, FC Porto wakimiliki kwa asilimia 63% huku wenyeji
wakiwa na asilimia 37% ulimalizika kwa mwamuzi wa mchezo huo Clattenburg
kuwaonya wachezaji tisa kwa kadi za njano, watano wakiwa ni wa FC Basel
na wanne kutoka FC Porto. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.