Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dk Makongoro Mahanga
akisindikizwa na Polisi kutoka katika Ukumbi wa Arnautoglu Dar es
Salaam jana, baada ya mafuasi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi kumzonga
alipokwenda kuhudhuria hafla ya kuapishwa wenyeviti wa Serikali za Mtaa
wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilala.
Wakati utata
ukizidi kujitokeza katika uapishaji wa viongozi wa Serikali za Mitaa
Mkoa wa Dar es Salaam kutokana na waliodaiwa kushinda kuwekwa kando na
kuapishwa walioshindwa, Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk Makongoro
Mahanga jana alikumbana na zomeazomea hadi kulazimika kuondoka kwenye
Ofisi za Manispaa ya Ilala, Arnatouglou ambako shughuli hiyo ilikuwa
ikifanyika.
Dk Mahanga ambaye pia ni Mbunge wa Segerea (CCM),
alizomewa akitakiwa kuondoka katika eneo hilo, akidaiwa kwamba
angebadilisha matokeo na kuwapa ushindi wagombea wa chama chake.
Eneo hilo lilijaa wafuasi wa Chadema, CUF na CCM
huku kila kundi likiwa limesindikiza wenyeviti wake kuapishwa katika
shughuli ambayo ilifanyika kwa awamu tatu kwa kila jimbo; Segerea, Ilala
na Ukonga kupewa saa mbili.
Waziri Mahanga aliwasili wakati wa zamu ya Segerea
saa saba mchana, ndipo kundi la mashabiki wa upinzani lilipoanza
kumzomea na kuimba nyimbo za kumkashifu na kutaka atoke katika ukumbi
ulioandaliwa kwa ajili ya kuwaapisha wenyeviti. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.