MICHUANO ya Kombe la Mapinduzi inaanza kutimua vumbi leo Visiwani
Zanzibar ambapo Simba itacheza na Mtibwa Sugar, na mabingwa watetezi,
Azam watacheza na KCCA ya Uganda Ijumaa kwenye Uwanja wa Amaan.
Mashindano hayo ni maalumu kwa ajili ya kuadhimisha siku ya Mapinduzi
ya Zanzibar yanashirikisha timu mbalimbali kutoka ukanda wa Afrika
Mashariki na Kati ambazo ni KCCA, Sports Club Villa zote kutoka Uganda,
El Merreikh ya Sudan, Ulinzi ya Kenya, Azam, Simba na Yanga zote kutoka
Tanzania Bara na Shaba, JKU, Mtendeni, Mafunzo na KMKM kutoka Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa waandaaji wa mashindano hayo ambao
ni Chama cha Soka cha Zanzibar (ZFA) zilisema kwamba baadhi ya timu
zimeshawasili kwa ajili ya mashindano hayo.
Michuano ya mwaka huu inatarajia kuwa na ushindani mkali kutokana na
kushirikisha timu nyingi kubwa na zinazofahamiana kutoka ukanda huu wa
Afrika Mashariki na Kati. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.