Jeshi la Polisi kitengo cha Kupambana na Dawa za kulevya limekamata
kilo 40 za dawa za kulevya aina ya heroine zenye thamani ya shilingi
bilioni 2.
Tukio hilo lilitokea juzi eneo la Tegeta nje kidogo ya Jiji la Dar es
salaam ambapo Polisi walifaniikiwa kuwanasa watu wawili wakiwa na dawa
hizo ndani ya nyumba inayomilikiwa na mchungaji ambaye wakati huo alikua
katika kanisa lake lililopo eneo la Sinza.
Kamanda wa kikosi cha kupambana na dawa za Kulevya Godfrey Nzowa alilithibitishia Gazeti la MTANZANIA kuwa kuwepo kwa tukio hilo akiomba jina la mchungaji huyo lihifadhiwe kuepusha kuvuruga uchunguzi.
“Ni kweli tukio la aina hiyo lipo lakini watu kama hawa siwezi
kusema moja kwa moja ni Mchungaji ndio muhusika hadi nipate
vithibitisho vya kutosha ikiwa kuendesha kanisa kwani wengi wao
wanatumia makanisa kama mwamvuli wa kujificha na kufanya biashara
hii,”Alisema Nzowa.
Alisema kwa sasa watu hao wanashikiliwa na Jeshi hilo ambapo wawili
kati yao si raia wa hapa nchini wakati upelelezi ukiendelea kabla ya
kuweka hadharani ukweli wa mambo. Asante kwa kutembelea blog hii, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz