Saturday, September 27, 2014

UKAWA WASEMA JK, CCM HAWAELEWEKI



 
Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) umesema kuwa Rais Jakaya Kikwete na CCM hawaeleweki ukidai ni kutokana na kukiuka makubaliano yao kuhusu kuendelea kwa Bunge Maalumu la Katiba mjini Dodoma.

Umoja huo pia umedai kwamba Mahakama Kuu ya Tanzania imeshindwa kutoa uamuzi fasaha kuhusu tafsiri ya kisheria ya mamlaka ya Bunge hilo katika kurekebisha Rasimu ya Katiba kwa kuogopa lawama kutoka Ukawa na CCM.

Ukawa unaoundwa na vyama vya Chadema, CUF, DP, NLD na NCCR-Mageuzi ulieleza hayo jijini hapa jana ulipozungumzia Mchakato wa Katiba ulipofikia, hasa baada ya Bunge hilo kufanya marekebisho ya kanuni kwa wajumbe wake kuruhusiwa kupiga kura kwa njia ya mtandao.

Mwenyekiti mwenza wa Ukawa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema kuwa makubaliano ya kusitishwa kwa Bunge hilo kati yao na Rais Kikwete yameshindwa kutekelezwa, jambo ambalo wanashindwa kuelewa sababu zake. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

JAJI WARIOBA AWAPANIA WAJUMBE WA KATIBA

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Joseph Warioba akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Miaka 19 ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dar es Salaam jana.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema Rasimu ya Katiba iliyopendekezwa na Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalumu la Katiba imeondoa mambo manne muhimu yaliyokuwa kiini cha kupata Katiba ya mageuzi.
Akiyataja mambo hayo muhimu ambayo ni maadili ya viongozi wa umma,  madaraka ya wananchi, mgawanyo wa madaraka na muungano. “Tutakutana mtaani. Tume tutaendelea kutetea rasimu yetu na wao wawaeleze wananchi kwa nini wameondoa maoni yao yaliyokuwa katika Rasimu ya Pili ya Katiba,” aliongeza kwa ufafanuzi Jaji Warioba.
Akizungumza katika maadhimisho ya miaka 19 tangu kuanzishwa kwa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Dar es Salaam jana, Jaji Warioba alisema rasimu hiyo inatofautiana kwa kiasi kikubwa na rasimu iliyotolewa na tume hiyo Desemba mwaka jana.
“Sina hakika kama tutapata Katiba Mpya labda Katiba iliyoboreshwa. Rasimu au Katiba itakayopendekezwa na Bunge Maalumu haitapigiwa kura hadi 2016. Sina hakika kama kura hiyo itapigwa kwa kuwa hakuna maridhiano hasa kuhusu muungano,  rasimu hiyo itaanza kupingwa tangu siku ya kutolewa kwake,” alisema. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI SEPTEMBA 27, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.


.
.
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

KESI YA MUBARAK YAAHIRISHWA MISRI

Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak akiwa mahakani
Uamuzi wa kesi inayomkabili rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak kuhusu mashtaka ya ufisadi na mauaji ya waandamanaji wakati wa mapinduzi ya mwaka 2011 umeahirishwa.
Jaji alisema kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutokana na sahabu ya kuwepo kwa ushahidi ambao bado mahakama haijausikiliza.
Wakati wa kesi ya leo kanda moja ya video ilionyesha mrundiko wa stakabadhi za ushahidi.
Bwana Mubarak alipatikana na hatia mnamo mwaka 2012 na kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani lakini baadaye hukumu hiyo ikabatilishwa.
Mahakama hiyo imesema kuwa itatoa hukumu yake mwezi Novemba. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MWANAMKE APIGWA MAWE HADI KUFA SOMALIA


Wapiganaji wa Alshabaab
Mwanamke mmoja ameuawa kwa kupigwa mawe nchini Somalia na kundi la wanamgambo wa Al Shabaab.
Ripoti zinasema kuwa takriban watu 200 akiwemo gavana wa eneo hilo walishuhudia watu wakimpiga mawe mwanamke huyo kwenye mji wa Barowe.
Mwanamke huyo wa umri wa miaka 30 alikuwa ameshutumiwa kwa kufanya mapenzi nje ya ndoa.
Wadadisi wanasema kuwa mauaji hayo ini ishara ya ushawishi wa kundi la Al shabaab hata baada ya kushambuliwa na serikali ya Somalia pamoja na vikosi vya muungano wa Afrika.
Mji wa Barowe ambao uko umbali wa kiomita 200 kutoka mji mkuu Mogadishu umekuwa ngome ya Al Shabaab. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na BBC

LOUIS VAN GAAL AKIRI WACHEZAJI MAN UNITED HAWAELEWI MBINU ZAKE

1411724782154_wps_5_FILE_PHOTO_Louis_van_Gaal
Louis van Gaal alishuhudia vijana wake wakipokea  kutoka kwa Leicester wikiendi iliyopita
LOUIS van Gaal  amekiri kuwa wachezaji wa Manchester United wana matatizo ya kuelewa mbinu zake mpya.
Mholanzi huyu aliitisha kikao kilichodumu kwa saa moja baada ya kufungwa na 5-3 na Leicester jumapili iliyopita.
Mshambuliaji wa United, Robin van Persie alisema kulikuwa na mgongano wa mawazo katika kikao hicho, lakini anahisi yote ilikuwa ni kwa faida ya kikosi.
The defeat prompted the Dutchman to accept that some of his players have not adapted to his methods
Mholanzi huyu amekiri kuwa Kipigo kilitokana na ukweli kwamba baadhi ya wachezaji wameshindwa kuelewa mbinu zake
Ikiwakosa wachezaji 10 kutokana na majeruhi na kutumikia adhabu, leo United inatarajiwa kuwa na muonekano mpya dhidi ya West Ham, Ingawa Van Gaal amekiri baadhi ya wachezaji hawajaendana na mbinu zake.
“Tulizungumaza mambo mengi na wanatakiwa kufanyia kazi” Alisema Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

RATIBA EPL LEO: LIVERPOOL v EVERTON, CHELSEA v ASTON VILLA, ARSENAL v TOTTENHAM, HULL CITY v MAN CITY, MAN UNITED v WEST HAM…!!!

article-2771118-21B0F6B100000578-503_964x386  Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
StandingsENGLAND: Premier League  
04:45   Liverpool - Everton      
07:00   Chelsea - Aston Villa      
07:00   Crystal Palace - Leicester      
07:00   Hull City - Manchester City      
07:00   Manchester United - West Ham      
07:00   Southampton - QPR      
07:00   Sunderland - Swansea      
09:30   Arsenal - Tottenham  

Friday, September 26, 2014

BAWACHA YAPANGA KUMUONA RAIS KIKWETE KWA MAANDAMANO...!!!


Mwenyekiti wa Baraza la wanawake Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bawacha), Halima Mdee akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu mandamano ya kupinga kuendelea kwa vikao vya Bunge la katiba. Kulia ni Makamu Mwenyekiti Bara, Hawa Mwaifunga.

Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) limetangaza maandamano kwenda Ikulu kumuomba Rais Jakaya Kikwete asikubali kutia saini Rasimu ya Katiba inayopendekezwa iwapo itapitishwa na Bunge.

Mwenyekiti wa Bawacha, Halima Mdee alisema jana kwamba maandamano hayo yatafanyika mwishoni mwa wiki ijayo, baada ya maandalizi yatakayofanyika kwa siku saba kuanzia jana kukamilika.

Mdee ambaye pia ni mbunge wa Kawe, alisema baraza hilo limeamua kuitisha maandamano hayo ili kuwakilisha kilio cha wanawake ambao ndiyo waathirika wa kwanza pale nchi inapokuwa katika mfumo usio wa haki.

Alivitaka vyombo vya dola hasa polisi kujitokeza kuwasindikiza na kuandamana nao kwa kuwa nao ni miongoni mwa Watanzania ambao wataathiriwa na uamuzi usiolenga kujenga umoja wa kitaifa.

Hata hivyo, Polisi imetahadharisha kuwa itaendelea kuwachukulia hatua za kisheria wanachama wa Chadema watakaojiingiza katika maandamano yaliyopigwa marufuku nchini. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA WATISHIWA MAISHA


Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, wakiwa katika vikao vya Bunge hilo Dodoma jana. Picha ya Maktaba

Siku tatu kabla ya Bunge la Katiba kuanza kupigia kura Rasimu ya Katiba inayopendekezwa, watu wasiojulikana wameanza kusambaza vitisho vya kuwatia hofu wajumbe wa Bunge hilo.

Watu hao wamesambaza vipeperushi katika maeneo mbalimbali ya mji wa Dodoma usiku wa kuamkia jana, wakiwataka wajumbe kutoingia bungeni vinginevyo yatakayowapata watajuta, huku wajumbe kutoka Zanzibar wakitishiwa kwa ujumbe wa simu kupitia mtandao wa WhatsApp.

Tayari, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd ametoa kauli kuhusu vitisho hivyo akisema Serikali itachukua kila hatua kuhakikisha wajumbe kutoka visiwani humo ambao wamekuwa wakipokea vitisho wanakuwa salama.

Mbali na kusambazwa kwa karatasi hizo, maandishi mekundu yamechorwa katika kuta za jengo la Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma yakisomeka, “No Katiba. No ufisadi.” Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO IJUMAA SEPTEMBA 26, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.


.
.
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

ZAIDI YA RAIA 3, 000 WA ULAYA NI WAFUASI WA I.S


Inakisiwa kuwa zaidi ya raia 3000 kutoka Ulaya ni wafuasi wa Islamic State
Idadi ya raiya kutoka Uropa wanaojiunga na kundi la wapiganaji wa Kiislamu nchini Syria na Iraqi imeongezeka hadi zaidi ya 3,000 kulingana na mkuu wa kitengo cha kupambana na ugaidi bara la ulaya.
Gilles de Kerchove ameonya kuwa mashambulizi ya hewa yanayofanywa na nchi za Magharibi yataongezea hatari ya mashambulizi ya kulipiza kisasi katika bara la Ulaya.
Vikosi vikiongozwa na Marekani vimetekeleza mashambulizi ya hewa mia mbili dhidi ya wanamgambo wa Islamic state wa Iraqi tangu Agosti na Jumatatu iliyopita wakaanza kulenga wale walioko Syria.
Bunge la Uingereza litapiga kura kwa mashambulizi ya hewa dhidi ya Iraqi siku ya Ijumaa.
Kundi la IS wameteka sehemu kubwa za Syria na Iraqi katika miezi ya hivi karibuni.
CIA inakisia kuwa kundi la IS linaweza kuwa na wapiganaji mpaka 31,000 huko Iraq na Syria, mara tatu zaidi ya wale waliohofiwa.
Mashambulizi haya yaliotekelezwa siku ya Alhamisi na ndege za Marekani, Saudi na UAE zilikuwa zinalenga mitambo 12 ya kusafisha mafuta nchini Syria .
Msemaji wa Pentagon Rear Admiral John Kirby alisema kuwa kusudi la mashambulizi haya ya hewa halikuwa kuwaua wanamgambo hao lakini ilikuwa kuharibu maeneo ambayo yalikuwa yakiletea kundi hilo fedha kupitia soko nyeusi.
Baadaye, siku ya Ijumaa, wabunge wa Uiungereza wataulizwa kuunga mkono mashabulizi dhidi ya wanamgambo wa IS Iraqi lakini sio Syria. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

TALIBAN YATEKA MJI WA GHAZNI AFGHANISTAN


Afisa wa usalama akishika doria katika mji wa Ghazni
Maafisa huko mashariki mwa Afghanistan wanasema kuwa wapiganaji wa Taliban wamechukua udhibiti wa baadhi ya Wilaya katika jimbo la Ghazni.
Watu zaidi ya 70 wanahofiwa kufariki katika Wilaya ya Ajrestan katika mapambano hayo ya kuteka vijiji vyao hapo jana jioni.
Ripoti zinasema Kuna makabiliano makali ya risasi huku walinda usalama wakifanya kila wawezalo kujaribu kutwaa tena wilaya hizo zilizotekwa.
Ghazni ni mji muhimu umnaochukuliwa kama mlango unaounganisha mji mkuu Kabul na eneo la kusini mashariki mwa nchi hiyo.
Wadadisi wa hali ya usalama nchini humo wanasema kuwa kutekwa kwa mji huo ni ilani kwa miji iliyoko karibu na
Ghazni huenda pia zikatekwa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

AZAM YAZIPIGA BAO SIMBA NA YANGA


Klabu ya Azam FC ndiyo inayoongoza kwa kulipa posho kubwa wachezaji wake kati ya timu zote 14 zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa wachezaji wa Azam ndiyo vinara wa kupata posho zilizoshiba wakizizidi Yanga na Simba ambao kwa kauli yao wamekubali matokeo.

Mgawanyo huo unaonyesha kwamba Azam kila inaposhinda mechi moja ya ligi inavuna kiasi cha Sh 4milioni, ambapo kila mchezaji anapewa Sh130,000 kiwango ambacho ni kikubwa kwa Simba na Yanga

Kitu kibaya kwa Azam ni pale inapotoa sare au kufungwa, ambapo hakuna chochote watakaochopata ingawa Simba na Yanga huambulia kitu zikitoka sare.

Hata hivyo, kiutaratibu unaonekana utaratibu unaotumiwa na Simba ndiyo mzuri kwani wachezaji wake hupata 40 % ya pato la mlangoni endapo timu hiyo inaibuka na ushindi huku ikiambulia 20% inapopata sare katika michezo yao.

Yanga, ambayo hivi karibuni wachezaji wake waliwasilisha maombi maalumu juu ya kutaka kubadilishiwa viwango vya posho, mpaka sasa wanaambulia kiasi cha Sh70,000 kila mchezaji kwa mechi wanayoshinda na hupata Sh 30,000 wanapopata sare.

“Hatuwezi kushindana na Azam, unajua Azam hata kama haupo katika orodha ya wachezaji wanaocheza mechi, Sh130,000 ipo palepale, lakini Simba na Yanga haipo hivyo, mchezaji anayecheza mechi anapata zaidi ya yule aliyekosa mechi,” alisema mmoja wa mabosi wa Simba ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

TFF YAZIKINGIA KIFUA SIMBA NA YANGA


Wachezaji wa kimataifa wa Yanga, Gelinson Santos ‘Jaja’ (kushoto) na Andrey Coutinho. Picha na maktaba.

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limezikingia ‘kifua’  Simba na Yanga na kueleza kuwa haliwezi kwa sasa kuzinyang’anya pointi kwa kuchezesha wachezaji wasio na vibali vya kufanya kazi  nchini.

Katibu Mkuu wa TFF, Celestine Mwisigwa alisema jana  kuwa suala hilo lipo kisheria zaidi.

“Kama kweli Simba, Yanga wamechezesha wachezaji wasio na vibali vya kufanya kazi nchini ni kosa na Serikali, inaweza kuwachukulia hatua klabu na wachezaji wao,” alisema Mwesigwa.

Hata hivyo, alisema kuwa adhabu ya kunyang’anywa pointi haielezi moja kwa moja na hadi sasa hakuna timu iliyokwenda TFF kulalamikia suala hilo.

“Hatuwezi sisi kuzinyang’anya pointi kama hakuna timu iliyokuja kwetu kulalamika, isitoshe Simba nimezungumza nao leo (jana) baada ya gazeti  kuripoti habari hiyo wakasema tayari wamewaombea vibali wachezaji na kocha wao, hivyo siwezi kujua nani mkweli, Simba na Uhamiaji,” alisema .

Juzi, Idara ya Uhamiaji ilitoa tamko kuhusu baadhi ya wachezaji na makocha wa kigeni wa timu hizo kutokuwa na vibali  vya  kufanya kazi nchini na kueleza kuwa tayari imeanza msako wa kuwakamata watakapoonekana wakijihusisha na mazoezi au mechi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Wednesday, September 24, 2014

ESTER BULAYA ATANGAZA VITA NA WASIRA...!!!




Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Mkoa  wa Mara, Ester Bulaya akizungumza  katika mahojiano maalumu na waandishi wa gazeti hili, Dar es Salaam jana.

Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Ester Bulaya ametangaza rasmi nia ya kugombea ubunge katika Jimbo la Bunda ambalo linashikiliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wasira.

Kwa nia hiyo, Bulaya anaweza kuwa ametangaza vita dhidi ya Wasira ambaye hivi karibuni akiwa Bunda, alitangaza kukitetea kiti chake hicho katika Uchaguzi Mkuu 2015.

Julai 8, mwaka huu Wasira akiwa kwenye kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya CCM wilayani Bunda, alitangaza kuwa atatetea nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu ujao, huku akijigamba kuwa yeye ni “mwarobaini wa matatizo” yanayowakabili wakazi wa jimbo hilo.

Kabla ya kutangaza nia hiyo, mara kadhaa Wasira amekuwa akihusishwa na suala la urais na ni mmoja wa makada sita wa CCM ambao walipewa adhabu na chama hicho Februari 18 mwaka huu, baada ya kukutwa na makosa ya kuanza mapema kampeni za urais mwaka 2015.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili jana, Bulaya alisema atagombea ubunge katika Jimbo la Bunda na anamtakia kila heri mpinzani wake huyo (Wasira) katika nafasi ya juu ya urais anayotaka kuwania. Alisema ameamua kufanya hivyo baada ya kuombwa na watu kadhaa kutoka jimboni humo wakiwamo vijana, wazee na kinamama. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...