Katibu Mkuu wa TFF, Celestine Mwisigwa alisema jana kuwa suala hilo lipo kisheria zaidi.
“Kama kweli Simba, Yanga wamechezesha wachezaji
wasio na vibali vya kufanya kazi nchini ni kosa na Serikali, inaweza
kuwachukulia hatua klabu na wachezaji wao,” alisema Mwesigwa.
Hata hivyo, alisema kuwa adhabu ya kunyang’anywa
pointi haielezi moja kwa moja na hadi sasa hakuna timu iliyokwenda TFF
kulalamikia suala hilo.
“Hatuwezi sisi kuzinyang’anya pointi kama hakuna
timu iliyokuja kwetu kulalamika, isitoshe Simba nimezungumza nao leo
(jana) baada ya gazeti kuripoti habari hiyo wakasema tayari wamewaombea
vibali wachezaji na kocha wao, hivyo siwezi kujua nani mkweli, Simba na
Uhamiaji,” alisema .
Juzi, Idara ya Uhamiaji ilitoa tamko kuhusu baadhi
ya wachezaji na makocha wa kigeni wa timu hizo kutokuwa na vibali vya
kufanya kazi nchini na kueleza kuwa tayari imeanza msako wa kuwakamata
watakapoonekana wakijihusisha na mazoezi au mechi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz