Monday, September 08, 2014

WEZI WA GARI LA RAIS WAFIKISHWA MAHAKAMANI



Gari la msafara wa Rais Kenyatta lilipatikana mjini Kampala Uganda

Watu watano akiwemo raia mmoja wa Uganda pamoja na fundi mmoja wa magari wameshitakiwa kwa kosa la wizi wa gari la msafara wa ulinzi wa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta nchini Kenya.
Watano hao pia walishitakiwa kwa kumuibia gari inspekta wa polisi David Machui aliyekuwa akiendesha gari hilo aina ya BMW 735 tarehe 26 mwezi Agosti mjini Nairobi lilipoibwa.
Washukiwa hao wote walikanusha madai hayo kwamba walihusika katika wizi wa gari hilo.
Kila mshukiwa aliachiliwa kwa kima cha shilingi milioni 5 isipokuwa mwanamume mmoja aliyesemekana kuwa na kesi tofauti mahakamani.
Raia wa Uganda Robert Mande Ochan, aliamrishwa na mahakama kutoa dhamana ya shilingi milioni mbili ili aweze kuachiliwa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

TUHUMA ZA UBAKAJI DHIDI YA AU

Shirika la haki za binadamu la Human Rights Watch limetoa ripoti kuhusu udhalilishwaji kijinsia wanaofanyiwa wanawake nchini Somalia na askari wa kulinda amani nchini humo.Majeshi hayo yamo nchini Somalia yakiwakilisha Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa kupambana na wapiganaji wa kikundi cha Kiislam cha Al Shaabab.
Shirika hilo la kutetea haki za binadamula Human Rights Watch limesema liliwahoji wanawake 21, wakiwemo wasichana waliobakwa na wanajeshi hao mwaka 2013.
Visa vingi vimeripotiwa katika kambi zinazosimamiwa na wanajeshi wa Burundi na Uganda.
Walinda amani wa Muungano wa Afrika wamedaiwa katika ripoti hiyo, kutumia chakula cha misaada kushawishi wasichana na wanawake kufanya mapenzi nao.
Wanajeshi hao wanadaiwa pia kuwabaka ama kuwadhalilisha kingono wanawake waliofika katika kambi hizo kuomba msaada wa matibabu au maji. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

LIONEL MESSI AMGARAGAZA CRISTIANO RONALDO TUZO YA FIFA 15, LIGI KUU ENGLAND

1410107894477_wps_32_image001_png
Mcheza bora wa dunia: EA Sports wamemuweka nyota wa Barcelona, Lionel Messi kuwa namba moja katika michezo mipya ya FIFA 15
CRISTIANO Ronaldo alimgaragaza Lionel Messi katika tuzo ya  Ballon d’Or mapema mwaka huu,lakini nyota huyo wa Barcelona amelipa kisasi kwa mpinzani wake huyo mkubwa kwa kushinda tuzo nyingine.
Akiwa amepata pointi 93 kati ya 100, messi amekuwa namba moja katika tuzo ya michezo ya Video ya FIFA, (FIFA 15) ambayo itatangazwa rasmi septemba 26 mwaka huu huko UK.
Ili kuwapa nafasi mashabiki kupiga kura kabla, waendeshaji wa tuzo hiyo, EA Sports walitangaza majina ya wachezaji 50.
Wanted man: Barcelona are sure to prove popular on the new game given Messi's eye catching statistics

MORIS AREJEA MAZOEZINI TAYARI KWA KUIKABILI YANGA


BEKI tegemezi wa Azam FC,Aggrey Moris leo ameanza mazoezi na timu yake kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga uliopangwa kufanyika Jumapili hii uwanja wa taifa..
Meneja wa Azam FC,Jemedari Said amesemeiambia Father Kidevu Blog kuwa Moris ameanza mazoezi na kikosi hicho baada ya kupona Malaria iliyomsumbua kwa wiki moja.
Moris hakuweza kusafiri na kikosi cha Taifa Stars juzi kutokana na kusumbuliwa na maradhi hayo na baada ya kupona anatarajiwa kuwemo kwenye kikosi cha Azam kitakacho pambana na Yanga Jumapili. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

OKWI HURU KUCHEZA SIMBA


Wajumbe wa Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya TFF wakiwa katika mkutano jijini Dar es Salaam jana. 


Utata wa Emmanuel Okwi umemalizwa rasmi na mchezaji huyo wa Uganda sasa yupo huru.

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ilikutana jana na kupitia masuala mbalimbali ikiwamo mgogoro wa kimkataba kati ya klabu ya Yanga na mchezaji Emmanuel Okwi.

Mkataba huo ulipitiwa na kamati ikiwamo kumsikiliza mchezaji mwenyewe pamoja na upande wa Yanga na kuridhika kuwa mkataba kati ya pande hizo umevunjika.

Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Boniface Wambura alisema jana kuwa mkataba wa pande mbili haupo kwa sababu Yanga ilikiuka kipengele namba 8 kuhusu malipo ya ada ya usajili.

“Yanga ikiwa mwajiri, haikutekeleza kipengele hicho cha kimkataba hadi kufikia Juni 27 mwaka huu ilipoandika barua TFF kuomba mkataba huo uvunjwe. Kwa maana hiyo Okwi ni mchezaji huru, hivyo yuko huru kujiunga na timu yoyote,” alisema Wambura.

Alifafanua kuwa mkataba ni uhusiano kati ya mwajiri (Yanga) na mwajiriwa (Okwi), ambapo Kamati imebaini kuwa uhusiano huo haupo, hivyo hakuna mazingira ya pande hizo mbili kuendelea kufanya kazi pamoja. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Sunday, September 07, 2014

HAYA NDIO MAAMUZI YA WAZIRI MWAKYEMBE KUFUATIA AJALI ILIYOTOKEA MUSOMA NA KUUA WATU 39

Waziri wa uchukuzi, Mhe Harrison Mwakyembe
Kufuatia ajali ya mabasi iliyoua takbriban watu 39 Musoma, Waziri wa uchukuzi, Mhe Harrison Mwakyembe amefanya maamuzi kadhaa, kupunguza ajali za barabarani. Ifuatayo ni kauli yake:
1.Tunaanza na hawa waliopata ajali, nimeelekeza na najua vyombo vinavyohusika Polisi pamoja na SUMATRA watatekeleza… kwanza kuzifungia kampuni za haya mabasi ya J4 na Mwanza Coach wasijihusishe na usafirishaji wa abiria tena, hatuwezi kuwa tunapata ajali za kijingajinga namna hiyo, nimeliona eneo lenyewe liko wazi kabisa lakini ni watu tu wameamua, dereva wa huku anamuona mwenzake na kusema mimi lazima anipishe’ – Dr. Mwakyembe
2. Tumeelekeza Wafanye uhakiki wa madereva wao wote na tunahitaji picha zao lakini vilevile tunahitaji mikataba ya kazi, hatutaki mabasi ya kupeleka abiria yaendeshwe na watu tu kwa majaribio, nataka ushahidi wa kila dereva kwamba amejiunga na hii mifuko ya akiba ya Wafanyakazi, tuone kabisa mchango wa Mwajiri na mfanyakazi kila mwezi’
3. Nimeagiza lazima tuangalie BIMA ya hiyo gari, unajifikiria mwenyewe tu ukipoteza gari ulipwe kidogo gari yako lakini hufikirii kuhusu binadamu…. bila comprehensive haendeshi mtu gari kuchukua abiria.
Tamasha la Fiesta lililokua lifanyike Ijumaa hapa Musoma sasa imefahamika litafanyika Jumapili ya kesho September 7 2014 ambapo pia imehamasishwa kwa wingi watu kujitokeza ili mapato hayo yapelekwe kwa ndugu waliopoteza watu na majeruhi ajalini. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

'SHEMEJI' AELEZA JINSI MBASHA ALIVYOMBAKA...!!!

  Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Emmanuel Mbasha

Shahidi wa kwanza katika kesi ya kubaka inayomkabili mwimbaji wa nyimbo za Injili, Emmanuel Mbasha, ameieleza mahakama jinsi mshtakiwa alivyomkaba shingo na kumziba mdomo kwa kutumia nguo, kisha kumbaka.
Shahidi huyo ambaye ni shemeji yake, mwenye umri wa miaka 17, aliyasema hayo jana wakati akitoa ushahidi wake katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala.
Hata hivyo, kesi hiyo ilisikilizwa kwa faragha (Chamber Cort) baada ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali Nassoro Katuga kuiomba mahakama kesi hiyo kuendeshwa kwa faragha kwa kuwa imefikia hatua ya kusikilizwa na sheria inaonyesha kuwa mtoto huyo yupo chini ya miaka 18.
Ombi hilo lilikubaliwa na pande zote mbili na kesi hiyo kuendeshwa katika mahakama ya faragha na Hakimu, Wilbaforce Luhwago aliomba watu wote walikuwepo ndani ya mahakama hiyo kutoka nje ili kupisha upande wa mashtaka kutoa ushahidi.
Akiongozwa na mwendesha Mashtaka wa Serikali Nassoro Katuga, shahidi huyo alidai siku ya tukio, Mei 23, mwaka huu, mshtakiwa aliondoka na mke wake kwenda kufuatilia mkanda wa video lakini ghafla alirudi nyumbani kwake Tabata Kimanga akiwa peke yake.
Alidai siku hiyo ya tukio mshtakiwa alifanikiwa kufanya mapenzi na binti huyo na kumwambia asimwambie mtu wakati mke wake akiwa hayupo nyumbani hapo.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 12,2014. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na Mwananchi

AL-SHABAAB WATHIBITISHA KIFO CHA KIONGOZI WAO

Wapiganaji wa Alshabaab

Kundi la wapiganaji wa kisomali Al-shabaab limethibitisha kuwa kiongozi wake Ahmed Abdi Godane aliuawa siku ya jumatatu katika shambulizi la angani lililotekelezwa na wanajeshi wa Marekani.
Msemaji wa Alshabaab amesema kuwa wanachama wengine wawili wa kundi hilo pia walifariki katika shambulizi hilo ,yapata kilomita 170 kusini mwa mji mkuu wa Mogadishu .
Ripoti zinasema kuwa kundi la Alshabaab limemchagua kiongozi mpya Ahmad Omar,katika mkutano uliofanyika katika eneo lisilojulikana.
Mwandishi wa BBC mjini Nairobi amesema kuwa kiongozi huyo hafahamiki vyema. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

LOIC REMY: BADO SIELEWI KWANINI SIO MCHEZAJI WA LIVERPOOL…LAKINI NINA FURAHA KUWA CHELSEA

1410045801087_wps_63_France_s_forward_Loic_Rem
Tatizo: Loic Remy  alikaribia kusajiliwa Liverpool kabla ya dili kushindikana.
MSHAMBULIAJI wa Chelsea,  Loic Remy amesema bado haelewi kwanini dili la kujiunga na Liverpool majira ya kiangazi lilivunjika.
Nyota huyo mwenye miaka 27 alitazamiwa kujiunga Anfield kwa dau la paundi milioni 8 kabla ya wekundu hao kulitupilia mbali dili hilo wakidai mchezaji huyo ameshindwa kufuzu vipimo vya afya.
Remy alishindwa kufuzu vipimo vya afya kutokana na matatizo ya moyo na goti, lakini alishangazwa na tangazo hilo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
“Binafsi sikuelewa. Tatizo wakati wa vipimo vya afya? sijui. Walitengenezea, lazima itakuwa hivyo,” aliwaambia Daily Star.
Mfaransa huyo alirejea QPR na alionekana katika mechi ya ligi kuu kabla ya kujiunga na Chelsea wiki ya mwisho ya usajili ambapo atacheza kumsaidia Diego Costa ambaye amepata majeraha ya nyama za paja katika majukumu ya kimataifa.
Delight: Remy signed for Chelsea on final week of the transfer window
 
Remy, ambaye aliifungia Ufaransa bao la ushindi dhidi ya Hispania siku ya alhamisi, alisema; “Kichwani mwangu, nilitaka kuendelea kukaa QPR, lakini sikuogopa kwa sababu nyingi  nilizonazo: Kwa jinsi nilivyojiimarisha, kujiamini kwangu na kwa namna Chelsea walivyonihitaji, nilikubali kwasababu hii ni moja ya klabu kubwa duniani.
“Nina furaha ya kujiunga na klabu hii” Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

LOUIS VAN GAAL HANA LA KUJITETEA KWA MANCHESTER UNITED, KIKOSI CHAKE KINA THAMANI YA PAUNDI MILIONI 379

1410038770007_Image_galleryImage_MILTON_KEYNES_ENGLAND_AUG
Hakuna kujitetea:Kikosi cha Manchester United chini ya Louis van Gaal kina thamani inayofikia paundi milioni 379
LOUIS van Gaal hatakuwa na la kujitetea kama Manchester United itashindwa kupambana kusaka ubingwa msimu huu.
Hii inatokana na ukweli kwamba Van Gaal ndiye kocha mwenye kikosi ghali zaidi katika ligi ya England kwa sasa.
Baada ya usajili mkubwa majira ya kiangazi, tafiti zinaonesha kuwa bosi huyo wa United ana kikosi chenye thamani ya paundi milioni 379.4.
Thamani hiyo haifikiwi na Manchester City ya Manuel Pellegrini na Chelsea ya Jose Mourinho.
Tangu kustaafu kwa Sir Alex Ferguson mwaka mmoja uliopita kampeni za kuwania ubingwa ziliisha na United wamejaribu kutumia paundi milioni 215 kusajili wachezaji ili kurudi katika kiwango cha juu.
Big deals: Angel di Maria and Radamel Falcao both arrived at Old Trafford in big-money moves this summer

JUAN MATA SOKONI JANUARI, ARTURO VIDAL, MATS HUMMELS KWENYE RADA, RONALDO NAYE ANAWEZA KURUDI OLD TRAFFORD

1410046545686_Image_galleryImage_VERONA_ITALY_AUGUST_30_Ar
Siku zijazo: Manchester United  bado wanaiwinda saini ya  Arturo Vidal (pichani juu)
MANCHESTER United bado hawajamaliza matumizi makubwa ya fedha katika dirisha la usajili.
Katika dirisha dogo la usajili mwezi januari mwakani wametenga paundi nyingine milioni 50  kwa ajili ya kunasa saini za wachezaji wengine.
Tayari United imeshatumia paundi milioni 150 katika dirisha la usajili majira ya kiangazi jumlisha kumsajili Radamel Falcao.
Arturo Vidal, Mats Hummels na Sami Khedira ndio wachezaji wanaowaniwa zaidi na United.
Jaun Mata Garcia atauzwa mwezi januari kama sehemu ya kuongeza wachezaji wapya ili kuimarisha kikosi cha Louis van Gaal.
Pia kuna taarifa kuwa mwanasoka bora wa dunia na Ulaya, Cristiano Ronaldo anaweza kurejea Manchester United.
Nyota huyo anayekipiga Real Madrid ana mapenzi makubwa na klabu yake hiyo ya zamani na anasema anaipenda toka moyoni.
On the move: United will look to sell Juan Mata as Louis van Gaal continues his rebuilding process
Atletico Madrid, Roma na Juventus  zipo tayari kumsajili Mata aliyesajiliwa na United kutoka Chelsea mwezi januari kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 37.
United inatarajia kukubali ofa ya paundi milioni 20. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Saturday, September 06, 2014

MORSI ASHTAKIWA KWA KUTOA SIRI ZA MISRI

Mohammed Morsi akiwa Kizimbani

Kiongozi mkuu wa mashtaka nchini Misri amemfungulia mashtaka aliyekuwa rais wa taifa hilo Mohammed Morsi kwa kupeleka stakhabadhi za siri kutoka idara ya usalama nchini Qatar.
Bwana Morsi amekuwa akizuiliwa jela tangu jeshi limuondoe madarakani mwaka uliopita wakati wa maandamano ya kumtaka ajiuzulu.
Tayari kiongozi huyo anakabiliwa na hukumu ya kifo katika mahakama nyengine tofauti.
Kundi la Muslim Brotherhood ambalo ni mwanachama wa maisha limepigwa marufuku na viongozi wake wengi huku wengine wakihukumiwa kifo.
Qatar imekuwa ikimuunga mkono Bwana Morsi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

DAMU YA WALIOPONA EBOLA KUTIBU UGONJWA HUO

Mkutano wa WHO kuhusu Ebola mjini Geneva.

Shirika la afya duniani WHO limesema kuwa damu ya watu ambao wameponea ugonjwa wa Ebola inaweza kutumiwa kuwauguza wagonjwa wengine.
Katika mkutano mjini Geneva, wataalam wa shirika hilo walikubaliana kwamba hii itakuwa njia ya haraka na ilio salama dhidi ya ugonjwa wa Ebola,sababu kuu ikiwa kwamba kinga ya mwili katika damu ya mtu aliyepona inaweza kukabiliana na virusi hivyo.
Wataalam hao pia wanataka matibabu mengine kuharakishwa ikiwemo dawa ya Zmapp pamoja na chanjo zengine mbili.
Idadi ya watu wanaodaiwa kufariki kutokana na ugonjwa wa Ebola imepita elfu mbili.
Zaidi ya watu elfu nne wameambukizwa ugonjwa huo huku tiba yake ikiwa bado haijajulikana. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Friday, September 05, 2014

TAZAMA PICHA ZA AJALI ILIYOTOKEA MUSOMA NA KUUA WATU ZAIDI YA 40

 Basi la Kampuni ya J4 EXPRESS lenye nambari za usajili T 677 CYC lililokuwa likitoka Musoma kuelekea Silari Mkoani Mara likiwa limeumia vibaya sana baada ya kugongana uso kwa uso na Basi lingine la Kampuni ya MWANZA COACH lenye nambari za usajili T 736 AWJ katika eneo la SabaSaba, Mjini Musoma mchana wa leo.
Watu zaidi ya 40 wamepoteza maisha papo hapo na wengine kujeruhiwa vibaya kwa mujibu wa Ripota wetu aliopo eneo la tukio, ilielezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni Basi la J4 ambalo lilikuwa likijaribu kuipita gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye nambari za usajili T 332 AKK katika sehemu ambayo mbele kuna daraja linaloweza kupitisha gari moja kwa wakati huo, kutokana na kuwa basi hilo lilikuwa kwenye mwendo kasi liliweza kuisukuma kwa ubavuni gari hiyo ndogo ambayo haikuweza kuhimili nguvu ya Basi hilo na kutoka kwenye njia na kwenda kuingia mtoni hali iliyoipelekea dereva wa basi hilo kuamini kuwa atawahi kupita katika daraja hilo bila kufahamu kuwa Basi lingine linalokuja mbele nalo liko kwenye mwendo kasi huku nalo likitaka kuwahi kupita kwenye daraja hilo. Ndani ya gari hiyo ndogo kulikuwa na watu watatu, ambapo wawili wamefariki na mmoja amejeruhiwa.
Basi la Kampuni ya MWANZA COACH lililokuwa likitokea Musoma kwenda Mwanza linavyoonekana baada ya kugongana uso kwa uso na Basi la Kampuni ya J4 EXPRESS.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz 

BUNGE LA KATIBA LAKATAA ELIMU YA KIDATO CHA NNE KWA WABUNGE


Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Pandu Amir Kificho (kulia) akiwaeleza jambo wajumbe wa bunge hilo walipohudhuria kikao cha 32 cha Bunge mjini Dodoma jana.

Pendekezo la Rasimu ya Katiba kuwa wabunge walau wawe na elimu ya kidato cha nne limetupiliwa mbali na wajumbe wa Bunge Maalumu, baada ya Kamati karibu zote kulikataa.
Kamati hizo zimependekeza kigezo cha elimu kuanzia walau kidato cha nne kama sharti muhimu la mtu anayetaka kugombea Ubunge kiondolewe, badala yake mgombea ama ajue tu kusoma na kuandika, au ajue kusoma na kuandika Lugha ya Kiswahili au Kiingereza kama ilivyo kwenye Katiba ya sasa.Mbali na pendekezo hilo, kamati hizo zimegawanyika kuhusu Ibara ya 129 ya Rasimu ya Katiba inayowapa wananchi nguvu ya kumuondoa mbunge wao madarakani kabla ya miaka mitano kumalizika.
Hayo yalijitokeza bungeni Dodoma jana, wakati kamati hizo zikiwasilisha taarifa zake kuhusu Sura ya 9 na 10 ya Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa bungeni na Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...