Viongozi kutoka mataifa ya Jumuiya ya Ulaya wanaokutana mjini Brussels kuimarisha vikwazo wanavyowekea Urusi,wameamua kuongeza idadi ya Warusi wanaopaswa kuwekewa vikwazo kibinafsi.
Orodha ya awali ya 21 sasa imeongezewa watu wengine 12.
Viongozi hao wa Jumuiya ya Ulaya pia wametoa wito kwa Tume inayosimamia jumuiya hiyo iwe tayari kuimarisha vikwazo zaidi vya kiuchumi dhidi ya Urusi iwapo hali hiyo ya sintofahamu itaendelea.
Kiongozi wa Ujerumani, Angela Merkel, amesema kuwa wale ambao majina yao yameongezwa kwa orodha ya hapo awali hawataruhusiwa kutembelea Ulaya na mali yao itapigwa tanji kama ilivyofanyika kwa maafisa 21 wa Urusi na Ukraine mapema juma hili.
Bi Merkel pia alisema kuwa Jumuiya ya Ulaya iko tayari kuunga mkono Serikali mpya ya Ukraine kifedha, bora tu iafikiane na Hazina ya Fedha duniani (IMF).
Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron amesema hatua muhimu zimechukuliwa kufikia sasa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz