Viongozi mbalimbali wa Chadema wameanza kupiga kampeni za urais mwaka 2015 kupitia Operesheni Pamoja Daima. (HM)
Akihutubia mamia ya wakazi wa Mkoa wa Njombe huku mvua kubwa ikinyesha jana, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa aliwatahadharisha vigogo wa Serikali wanaoiba fedha za umma kuwa, atawashtaki na kuwafilisi iwapo chama hicho kitashinda uchaguzi mwaka 2015.
Alisema chama hicho kikishinda dola, kitaboresha masilahi kwa watumishi waadilifu lakini mafisadi wanaotafuna fedha za Serikali watapata wakati mgumu.
"Tutakuwa wakali kwa walarushwa," alisema Dk Slaa.
Dk Slaa alisema watendaji walarushwa na wezi watashtakiwa ili mali walizowaibia Watanzania zirejeshwa Serikalini.
"Ninawapa miezi 15 kabla ya uchaguzi mkuu, vigogo hao kurudisha mali walizoiba vinginevyo watajuta kwa sababu tutawashtaki tutakapoingia madarakani." alisema.
Naye Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo alisema chama hicho kitatumia kila aina ya 'silaha' kilichonayo kuhakikisha majimbo yote ya Mkoa Kilimanjaro yananyakuliwa na chama hicho 2015.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz |