Tuesday, November 19, 2013

KAGAME, MUSEVENI NA KENYATTA WASHTAKIWA KORTI YA JUMUIYA

kagamepx_deab7.jpg
Serikali za Rwanda, Uganda, Kenya na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, zimefunguliwa kesi katika Mahakama ya Afrika ya Mashariki, zikidaiwa kukiuka mkataba wa kuanzishwa kwa jumuiya hiyo.
Hatua hiyo inatokana na Serikali hizo kufanya vikao vitatu mfululizo na kuzitenga nchi za Tanzania na Burundi.
Walalamikaji katika kesi hiyo, ni Ally Msangi, David Makata na , John Adam, ambao ni Watanzania, wanaotetewa na wakili Mwandamizi, Jimm Obedi wa jijini Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine, walalamikaji wamewaomba majaji katika mahakama hiyo, kutoa tamko la kusitisha utekelezaji wa maazimio yote ya vikao vya wakuu wa nchi hizo tatu.
Pia wameomba majaji watoe tamko la kukomesha kurejewa kwa vikao kama hivyo kinyume cha mkataba wa jumuiya hiyo.
Kesi hiyo ya aina yake, ilifunguliwa jana katika Mahakama ya Afrika ya Mashariki na kupokewa na Ofisa Masijala i katika mahakama hiyo, Boniface Ogoti.
Kufunguliwa kwa kesi hiyo, kunakuja siku kadhaa baada ya Rais Jakaya Kikwete kuzilalamikia nchi hizo, kuhusu kuitenga Tanzania kwa kufanya mikutano mbalimbali ya maendeleo ya nchi zao. Nchi nyingine iliyotengwa ni Burundi.
Kikao cha kwanza cha pamoja kilifanyika Aprili mjini Arusha kabla viongozi hao kukutana Juni 25 na 26 jijini Entebbe nchini Uganda, walidai kuwa na nia moja ya kurahisha mawasiliano katika nchi hizo.
Mkutano mwilingine ulifanyika mjini Kigali Rwanda Oktoba 28 ukiwajumuisha Rais Yoweri Museven wa Uganda, Uhuru Kenyatta (Kenya), Salva Kiir (Sudan Kusini) na Paul Kagame.
Wakili wa walalamikaji Obedi, alisema katika kesi ya msingi, wanawashtaki Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Rwanda, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Uganda,Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Kenya na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo.

Monday, November 18, 2013

UFOO SARO: NI MIUJIZA YA MWENYEZI MUNGU TU NDIYO ILIYONIWEZESHA KUEPUKA KIFO.

Mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Ufoo Saro akisoma somo kwenye biblia  wakati wa ibada maalumu ya shukrani kwenye Kanisa la (KKKT ) Usharika wa Kibamba nje kidogo ya Jiji la Dare Salaam jana. Picha na Sanjito Msafiri.  
******
DAR ES SALAAM. 
MTANGAZAJI wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Ufoo Saro ambaye alijeruhiwa kwa kupigwa risasi na mzazi mwenzake, Anthery Mushi, amefanya ibada na kusema: “Namshukuru Mungu kwa kumponya.”
Ni mara ya kwanza Saro kuzungumza tukio hilo tangu aliporuhusiwa kutoka Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu, MOI ya Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa.

Katika ibada hiyo iliyofanyika katika Kanisa la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Kibamba, Jimbo la Magharibi, Ufoo huku akitokwa na machozi na wakati mwingine kushindwa kuzungumza alisema: “Ni miujiza tu ya Mungu yeye kunifanya mimi kuwa hai leo.”

Mtangazaji huyo ambaye alilazwa kwa zaidi ya wiki mbili, aliwashukuru watu wote waliomtia moyo, kumsaidia kipindi chote alichokuwa mgonjwa.

'KACHAA' BALOTELLI AFURAHIA KUREJEA ENGLAND

balotel_94581.jpg
Siku za furaha: Mario Balotelli akiwa mwenye furaha wakati wa mazoezi ya Italia Uwanja wa Craven Cottage jana
'KACHAA' Mario Balotelli alikuwa mwenye furaha aliporejea England wakati mshambuliaji huyo wa AC Milan alipokuwa akifanya mazoezi na kikosi cha Italia Magharibi mwa London.
Balotelli aliichezea Manchester City kabla ya kutibuana na aliyekuwa kocha wa timu hiyo Roberto Mancini na wachezaji wenzake kadhaa hivyo kuondoka, lakini nyota huyo mwenye umri wa miaka 23, aliyeondoka Etihad miezi 10 iliyopita, alikuwa mtulivu jana.
Kikosi cha The Azurri kinaendelea na maandalizi ya Fainali za Kobe la Dunia mwakani nchini Brazil na leo usiku kitacheza mechi ya kirafiki na Nigeria, kwenye Uwanja wa Fulham, Craven Cottage.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU NOVEMBA 18, 2013

DSC 0080 9c6c1
DSC 0081 b7da2

Sunday, November 17, 2013

TAIFA STARS SASA KUIKABILI ZIMBABWE J4

Taifa Stars sasa inacheza na Zimbabwe mechi ya Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)- FIFA Date itakayofanyika keshokutwa Jumanne (Novemba 19 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Awali Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ilikuwa icheze na Kenya (Harambee Stars), lakini Shirikisho la Mpira wa Miguu Kenya (FKF) lilituma taarifa jana jioni (Novemba 16 mwaka huu) likieleza kuwa timu yake haitacheza tena mechi hiyo.

Kikosi cha Zimbabwe chenye msafara wa watu 30 kinatarajia kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kesho (saa 3 asubuhi) tayari kwa mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 11 kamili jioni.

NIGERIA YA KWANZA KUKATA TIKETI YA BRAZIL 2014 BAADA YA KUIFUMUA ETHIOPIA 2-0

article-2508386-1973888200000578-737_634x423_5ac75.jpg
Timu ya taifa ya Nigeria imekua nchi ya kwanza ya Afrika kukata tiketi ya kecheza. Fainali za Kombe la Dunia mwakani baada ya ushindi wa mabao 2-0 nyumbani dhidi ya Ethiopia leo. Victor Moses alifunga kwa penalti dakika ya 20 na Victor Obinna akaongeza la pili dakika ya 82 kwa mpira wa adhabu, hivyo Super Eagles kufuzu kwa ushindi wa jumla wa 4-1, baada ya awali kushinda 2- mjini Addis Ababa mwezi uliopita katika mchezo wa kwanza

IVORY COAST NAYO YAFUZU KOMBE LA DUNIA BAADA YA SARE YA1-1 NA SENEGAL

IvoryCoast-celebrates130122G300_2ccf2.jpg
TIMU ya taifa ya Ivory Coast imefuzu Fainali zijazo za Kombe la Dunia baada ya sare ya 1-1 usiku huu ugenini na Senegal kwenye Uwanja wa Mohamed V in Casablanca, Morocco.
Matokeo hayo yanaifanya Didier Drogba na wenzake wafuzu kwa ushindi wa jumla wa 4-2 na kuungana na Nigeria iliyoitoa kwa jumla ya mabao 4-1 Ethiopia.
Ikiwa inajivunia ushindi wa 3-1 katika mchezo wa kwanza, Tembo walilazimika kusota kusawazisha bao baada ya Moussa Sow kutangulia kuwafungia Simba wa Teranga kwa penalti, kabla ya Salomon Kalou kusawazisha dakika za majeruhi.
Kikosi cha Senegal: Coundoul, S. Sane, L. Sane, Mane, Badji/Saivet dk82, P. Cisse, Mbodji, Gueye, Souare, Djilobodji na Ndoye/Sow 66.
Ivory Coast: Barry, K. Toure, Bamba, Gosso, Zokora, Romaric, Aurier, Y. Toure, Kalou, Gervinho/Sio dk80 na Drogba

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI NOVEMBA 17, 2013 YA DINI, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.
.
.

HASSAN DILUNGA ATUA YANGA

dilunga a6713
SAA chache baada ya kufunguliwa kwa Dirisha Dogo la Usajili kwa msimu wa 2013/14, vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom, Yanga jana walifanikiwa kumsajili kwa mkataba wa miaka mitatu kiungo Hassan Dilunga kutoka Ruvu Shooting ya Pwani.

Kwa mujibu wa kanuni, klabu za Ligi Kuu na Daraja la Kwanza zenye fursa ya kusajili wachezaji katika dirisha dogo ni zile ambazo hazijatumia nafasi zote 30 za wachezaji, usajili uliofunguliwa jana Novemba 15 na kutarajiwa kufungwa Desemba 15.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa klabu ya Yanga, Abdallah Bin Kleb, alisema jana kwamba usajili wa kiungo huyo ni utekelezaji wa maagizo ya Kocha Mkuu, Ernie Brandts, aliyoyaacha na benchi lake la ufundi kwa ajili ya kuboresha kikosi.

"Kocha aliacha mapendekezo ya usajili tuyafanyie kazi, la kwanza lilikuwa ni kuhakikisha tunampata Kaseja ili kuongeza nguvu miongoni mwa makipa, ambao tuliukamilisha mwishoni mwa wiki na sasa tumelimaliza la kiungo Hassan Dilunga," alisema Bin Kleb na kuongeza.

Kikubwa kuhakikisha kuwa, tunatekeleza maagizo yote yaliyo katika ripoti ya benchi la ufundi na kuyafanyia kazi ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kuboresha kikosi chetu kwa ajili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Usajili wa Dilunga kiungo aliyeteuliwa kikosi cha timu ya taifa, 'Taifa Stars', inayojiandaa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Harambee Stars, ametua Jangwani siku chache baada ya mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu walipomsajili mlinda mlango wa zamani wa Simba na Stars, Juma Kaseja, aliyekuwa hana timu tangu kumaliza mkataba wake na Wekundu wa Msimbazi.

MAREKANI YAIWEKA PABAYA TANZANIA, YAIITA KITOVU CHA ‘BIASHARA’ YA BINADAMU


UzaMtuClip 79203
Marekani imetoa ripoti inayozungumzia usafirishaji wa binadamu ya mwaka 2013, huku ikiitaja Tanzania kuwa kinara wa kunyanyasa wasichana, kuwatumikisha katika ngono na usafirishaji wa binadamu.
Ripoti hiyo iliyotolewa na idara ya nchi hiyo inayohusika na diplomasia (US Department of State, Diplomacy in Action), pia inaitaja Tanzania kuwa ni kitovu cha njia ya kusafirisha wanawake, watoto na wanaume ambao hutumikishwa kwenye kazi za mashambani na biashara ya ngono.


Ripoti hiyo iliyozinduliwa Julai mwaka huu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Seneta John Kerry inaweka bayana kwamba biashara ya usafirishaji wa binadamu hufanywa na baadhi ya ndugu na marafiki ambao hutoa ahadi kwa wahusika kwamba wanakwenda kuwasomesha au kuwatafutia ajira nzuri mijini.
"Unyonyaji wa wasichana wadogo na utumikishaji majumbani ndilo tatizo linaloongoza, ingawa kesi za watoto kusafirishwa kwa ajili ya biashara ya ngono katika mpaka wa Tanzania na Kenya zinaongezeka. Pia, wasichana wananyonywa kwenye maeneo ya utalii," inasema sehemu ya ripoti hiyo.

Saturday, November 16, 2013

KILI STARS YAPANGWA NA ZAMBIA, BURUNDI CHALLENGE 2013

9_e471e.jpg
Kikosi cha Taifa Stars amacho kinaundwa na wachezaji wengi wa Bara
Na Prince Akbar, Dar es Salaam
TANZANIA Bara maarufu kama Kilimanjaro Stars imepangwa katika Kundi B kwenye michuano ya CECAFA Challenge pamoja na Zambia, Burundi na Somalia.
Katika michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Novemba 27 mjini Nairobi, Kenya, wenyeji Harambee Stars wamepangwa na Ethiopia, Zanzibar na Sudan Kusini katika Kundi A.
Mabingwa watetezi, Uganda wamepangwa Kundi C pamoja na Rwanda, Sudan na Eritrea. Ratiba ya michuano hiyo inatarajiwa kutolewa wiki ijayo.

MAKUNDI CHALLENGE 2013:
KUNDI A- Kenya, Ethiopia, Zanzibar, South Sudan
KUNDI B- Tanzania, Zambia, Burundi and Somalia
KUNDI C- Uganda, Rwanda, Sudan and Eritrea.

MGAO WA UMEME KUANZA LEO NCHI NZIMA

aa_29e0f.jpg
Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Badra Masoud akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kuwepo kwa upungufu wa umeme kwenye gridi ya Taifa kuanzia tarehe 16 hadi 26 November, 2013 kutokana na upungufu wa gesi kutoka katika Kisiwa cha Songosongo kilichopo Wilaya ya Kilwa, Mkoa wa Lindi Unaosababishwa na Matengenezo ya Kiufundi kwenye visima vya gesi unaofanywa na Kampuni ya Pan Afrika ili kuboresha upatikanaji wa gesi ya kutosha kwenye visima hivyo.

SHIRIKA LA UMEME TANZANIA
MPR/PR/12
Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) linasikitika kuwajulisha wateja wake wote kwamba kutawepo na upungufu wa umeme kwenye gridi ya Taifa kuanzia tarehe 16 hadi 26 November, 2013 kutokana na upungufu wa gesi kutoka katika Kisiwa cha Songosongo kilichopo Wilaya ya Kilwa, Mkoa wa Lindi Unaosababishwa na Matengenezo ya Kiufundi kwenye visima vya gesi unaofanywa na Kampuni ya Pan Afrika.
Lengo la matengenezo hayo ni kuboresha upatikanaji wa gesi ya kutosha kwenye visima hivyo.
Kutokana na Matengozo hayo Mikoa iliyounganishwa katika gridi ya Taifaa itaathirika kwa kukosa umeme kwa baadhi ya maeneo kwa nyakati tofauti.
Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza kwa baadhi ya maeneo yatakayokuwa yakikosa umeme.
Imetolewa na: BADRA MASOUD
MENEJA UHUSIANO

RATIBA YA SHUGHULI YA KUAGA MWILI WA DKT. SENGONDO MVUNGI LEO - JUMAMOSI NOVEMBA 16 2013

Mvungi_01_f96b1.jpg
NOVEMBA 15, 2013 – UWANJA WA NDEGE WA MWALIMU JK NYERERE
Saa 12:50 jioni
Kuwasili kwa mwili wa Marehemu – Uwanja wa Ndege wa Mwalimu JKN
KESHO, NOVEMBA 16, 2013 – VIWANJA VYA KARIMJEE
Saa 2:00 – 3:30 asubuhi
Kuwasili kwa Wageni, Wananchi na Waombolezaji
Saa 3:30 asubuhi
Kuwasili Mwili wa Marehemu
Saa 4:00 – 5:45 asubuhi
Ibada ya Misa Takatifu, Viwanja vya Karimjee
Saa 5:45 – 6:55 mchana
Salaam za Rambirambi na Neno la Shukurani
Saa 6:55 – 8:40 Mchana
Kuaga Mwili wa Marehemu
Saa 9:00 Alasiri
Msafara kupeleka mwili wa marehemu Kibamba Msakuzi
KESHO KUTWA, NOVEMBA 17, 2013 – NYUMBANI KWA MAREHEMU - KIBAMBA, MSAKUZI
Saa 2:30 – 4:30 asubuhi
Ibada ya Misa nyumbani kwa marehemu
Saa 5:00 asubuhi
Kuanza safari ya kwenda Chanjale, Kisangara Juu, Mwanga, Kilimanjaro

TATOO NA MUONEKANO MPYA WA RAY..... VYAWACHEFUA WASHABIKI WAKE

 
Huu  ni  muonekano  mpya wa  Vicent  Kigosi ambao ni moja ya maandalizi ya movie  yake  mpya ...
Ni  muonekano  ambao  kwa  kiasi  flani  umewachefua  mashabiki  wake  ambao  dakika  chache  baada  ya  picha  hizo  kuwekwa  walijimwaga  kwa  comment  ambazo hazikumuunga  mkono  kwa  asilimia  zote.



  Je nageukia bongoflava au kuna nini kinakuja?. Aliadika  Ray  kwenye  moja  ya  picha  zake.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...