Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Lambert Mende, ameiambia DW mjini Kinshasa kuwa serikali ya nchi hiyo haijashangazwa na hatua hiyo ya M23, lakini akasisitiza kuwa wanachotaka wao ni kuona waasi hao wakiweka silaha chini, kama wanavyotakiwa na jumuiya ya kimataifa na pia serikali ya Kongo.
Jana, Rwanda ililishutumu jeshi la
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kile ilichokiita uchokozi wa
makusudi, baada ya kombora linaloaminika kutoka upande wa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo kuanguka nchini Rwanda, na kumuuwa mwanamke mmoja
na kumjeruhi vibaya mtoto wake mchanga.