KESI inayomkabili staa wa filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu ya kudaiwa
kumtukana matusi ya nguoni na kumpiga vibao meneja wa hoteli, Goodluck
Kayumbu ilizua kituko baada ya shahidi kugeuka ‘bubu’ ghafla.
Kituko hicho kilijiri Agosti 20, mwaka huu katika Mahakama ya Mwanzo Kawe jijini Dar ambako kesi hiyo inaunguruma.
Mmoja wa makarani wa mahakama hiyo aliyeomba hifadhi ya jina lake, alisema kitu kilichoonekana kituko ni pale shahidi wa mwisho aliposhindwa kutoa ushahidi baada ya sauti kukauka ghafla.
“Mlalamikaji alifika hapa na mashahidi wake watatu, Boniface Mati, Taito Osa na Melao ambapo wawili walitoa ushahidi lakini Taito alishindwa kutoa ushahidi wake kwani sauti ilikata ghafla na ndipo hakimu Bernice akamuamuru anyamaze na kupanga tarehe nyingine ya kuwasikiliza mashahidi hao,” alisema karani huyo.
Mlalamikaji wa kesi hiyo, alipoombwa na paparazi wetu azungumzie ‘ ishu’ ya shahidi wake kushindwa kuzungumza alisema amekubaliana na uamuzi wa mahakama na anasubiri tarehe ya kurudi mahakamani ambayo ni Septemba 30, mwaka huu.