RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali
Mohamed Shein kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 53 cha
Katiba ya Zanzibar ya 1984 amefanya marekebisho katika muundo na
majukumu ya baadhi ya Wizara za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kufuatia
marekebisho hayo, baadhi ya shughuli za Wizara zimeunganishwa na
kuundiwa Wizara mpya na baadhi zimehamishiwa katika wizara mpya na
baadhi zimehamishiwa katika wizara nyengine.
Hata hivyo marekebisho hayo hayakuongeza idadi ya Wizara na kwa hivyo zinaendelea kubaki wizara 16. Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na
Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya MzeeMarekebisho ya muundo na
shughuli katika baadhi ya Wizara ni kama ifuatavyo.