Tuesday, August 13, 2013
MWINGEREZA ADAKWA NA NYARA ZA SERIKALI ZENYE THAMANI YA SH 118,314,900
(Picha na maktaba)
RAIA wa Uingereza, Robert Dewar, amekamatwa na nyara za serikali zenye thamani ya sh 118,314,900 jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, mtuhumiwa huyo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trans Afrikas Logistics (TALL), akikamatwa Agosti 9, mwaka huu, akiwa na nyara hizo.
Alizitaja nyara hizo kuwa ni vipande vinane vya meno ya tembo, vinyago 11, meno ya tembo 20, meno 20 na kucha 22 za Simba, ndege mmoja aina ya kasuku, vipande vya miti ya mpingo na idadi kubwa ya vinyago, vyote vikiwa na uzito wa kilogramu 24.
Mtuhumiwa huyo pia alikutwa akiwa na mawe yanayodhaniwa kuwa ni madini pamoja na ganda moja la bomu lenye ukubwa wa milimita 130.
Kamishna Kova aliongeza kuwa mtuhumiwa amekuwa akisafirisha vitu hivyo sehemu mbalimbali duniani, na kwamba atafikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika.
Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi limeahidi zawadi nono ya sh milioni 100 kwa mtu atakayetoa au kufanikishwa kukamatwa wahalifu wanaotuhumia kutumia tindikali kuwadhuru watu mbalimbali.
CRDB YAKABIDHI WODI YA WAZAZI NA VIFAA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA META-MBEYA
Waziri
wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji
wa benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla
ya kukabidhi wodi ya wazazi iliyofanyiwa ukarabati na benki hiyo katika
Hospitali ya Rufaa Mbeya, Kitengo cha Huduma ya Akinamama na
Watoto-Meta. Hafla hiyo ilifanyika mjini Mbeya, mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa benki ya CRDB, Tully Mwambapa akizungumza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akifafanua jambo wakati wa hafla hiyo.
Monday, August 12, 2013
HII HAPA BARUA RASMI YA MWINYI KAZIMOTO KWA TFF AKIOMBA MSAMAHA KWA KITENDO CHA KUTOROKA
MWINYI KAZIMOTO
P O BOX 21923
DOHA, QATAR
TANZANIA FOOTBALL FEDERATION
P O BOX 1574
DAR-ES-SALAAM
TANZANIA
YAH: KUOMBA MSAMAHA KWA CHAMA CHA MPIRA TANZANIA
Husika na kichwa cha habari hapo juu
mimi mchezaji MWINYI KAZIMOTO naomba msamaha kwa kitendo nilichokifanya
cha kuondoka kambini timu ya taifa na kuiacha nchi yangu katika kipindi
kigumu hali ya kuwa walikuwa na mechi ngumu na muhimu dhidi ya Uganda.
Halikuwa lengo langu kuidhoofisha nchi
yangu bali ni tamaa yangu ya kucheza mpira nje ya nchi ndiyo
iliyonifanya niondoke katika kipindi hicho, na nashukuru mungu
nimefanikiwa kupata team nchini Qatar, naamini watanzania wataipokea
habari hii kwa vizuri.
Mwisho kabisa napenda kuwahakikishia
watanzania na chama cha mpira kwa ujumla kwamba naahidi nitaitumikia
nchi yangu muda wowote watakaponihitaji.
Natumai chama cha mpira na watanzania kwa ujumla watanielewa na watanisamehe.
Wenu mtiifu
MASIKINI WASTARA ALA IDD MAKABURINI...!!!
Ishu hiyo ilijiri Ijumaa iliyopita siku ya sikukuu hiyo ambapo Wastara alitundika picha zake zikiwa zinamuonesha akiwa ameshika tama na nyingine akiwa analifanyia usafi kaburi la marehemu Sajuki lililopo katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar.
Wastara alikiri
kuwa aliitendea haki Sikukuu ya Idd kwani alipata nafasi ya kuzuru
kaburi la mumewe na kujisikia faraja japo kimwili hayupo naye lakini
kiroho wako pamoja.
“Sikukuu yangu nimeitendea haki sana kwa kwenda kuzuru kaburi la mume wangu, alhamdullilah nimefarijika sana, kimwili siko naye ila atabaki kuwa fikrani mwangu milele,” aliandika Wastara.
“Sikukuu yangu nimeitendea haki sana kwa kwenda kuzuru kaburi la mume wangu, alhamdullilah nimefarijika sana, kimwili siko naye ila atabaki kuwa fikrani mwangu milele,” aliandika Wastara.
Mashabiki wake na wadau mbalimbali walimpa pole huku wengine wakimpongeza kwa hatua hiyo kwani wasanii wengine waliotumia sikukuu hiyo kujiremba, kwenda klabu na kujirusha. Sajuki alifariki dunia Januari 2, mwaka huu na kuacha mtoto mmoja wa kike.
PETE NA CHENI ANAZOVAA DIAMOND ZINA THAMANI YA SHILINGI MILIONI 24...!!!
Akihojiwa juzi kwenye kipindi cha The Trend cha NTV, mtangazaji wa show hiyo Larry Madowo aliuliza thamani ya bling alizokuwa amevaa.
“It’s a bit expensive,” alijibu Diamond huku akizishika bling hizo.
“Kama hii na hii it’s about dola 2000 something au 1,500, hii peke yake dola 2,000.”
Hata hivyo
zingine alishindwa kukumbuka bei yake japo kwa kuangalia saa yenye
diamond aliyokuwa nayo, pete zingine mbili za dhahabu na almasi na
cheni mbili kubwa za dhahabu gharama yake kwa ujumla inaweza kufika dola 15,000 ukijumlisha na hizo zingine alizotaja gharama yake.
“Zina rates tofauti lakini ni gharama kidogo,” alisema staa huyo.
“Zina ishara? Maanake wengine wanaweza kusema ni Illuminati ama nini,” aliuliza Larry.
“Sidhani mimi
navaa tu hii diamond ni jina langu, hii crown as mtu anayelead, kuna
diamond nyingi hapa, hii ina alama flani kama ya batman as am flying,”
alijibu Diamond.
Aidha Diamond alimtaja Usher Raymond kama msanii anayemtazama na kufuata nyayo zake zaidi.
“I don’t know
men, namuona kama anajua sana anachokifanya, tangia nilipokuwa
nikimfuatilia mpaka leo. Unajua wanamuziki wengi akitoka mwanamuziki
flani yeye anapotea, Usher Raymond yupo. Ukiangalia vitu vyangu mimi
namuiba sana. MSIKILIZE HAPO CHINI
FLAVIANA MATATA AENDELEA KUITOA KIMASOMASO TANZANIA, AFRIKA NA KIMATAIFA
NYOTA ya
mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania, Flaviana Matata amezidi kung’ara baada
ya kuingia katika orodha ya wanamitindo saba bora kwa upande kipato.
Kwa mujibu
wa gazeti la biashara la kimataifa la Forbes kwa bara la Afrika (Forbes Africa)
lililotolewa hivi karibuni, Flaviana ni mrembo pekee aliyeingia katika orodha
hiyo kwa wanamitindo wa Afrika Mashariki na kuzidi kuipeperusha vyema bendera
ya Tanzania kimataifa.
Katika
orodha hiyo, mwanamitindo Maria Borges wa Angola ndiyo aliibuka namba moja na wengine sita pamoja na Flaviana wakibaki kutoa
ushindani mkubwa kwa mlimbwende huyo wa Angola.
Mbali ya
Flaviana, wanamitindo wengine ambao wapo katika orodha hiyo ni Candice
Swaenpoel, Katryn Kruger wote wakitokea Afrika Kusini, Ajak Deng, Grace
Bol ( Sudan) na Liya Kebede wa Ethiopia,.
Flaviana
Matata aliibuka katika jukwaa la kimataifa kama Miss Universe Tanzania mwaka
2007 na aliweka historia kwa kuingia 10 bora na baada ya kumaliza muda wake
aliendelea na fani ya uanamitindo Afrika
kusini na baadaye alipata nafasi ya kufanya kazi Marekani na Ulaya katika
makampuni makubwa ya uanamitindo ya Next Models International na sasa yuko
Wilhelmina Models.
MGOSI: NARUDI UPYA MSIMU UJAO LIGI KUU...!!!
Mussa Hassan Mgosi.
Na Martha Mboma
MSHAMBULIAJI mkongwe hapa Bongo,
Mussa Hassan Mgosi, amesema amerudi upya, hivyo mashaibiki wake
watarajie mambo mapya katika msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kiungo huyo amejiunga na Mtibwa Sugar hivi karibuni akitokea JKT Ruvu. Kabla ya hapo alikuwa akiichezea timu ya DC Motema Pembe ya DR Congo ambayo alijiunga nayo akitokea Simba.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Mgosi alisema kwa sasa anaendelea na maandalizi ya nguvu, hivyo mashabiki watarajie vitu vipya kutoka kwake.
“Nimerudi
kivingine katika soka, hivyo mashabiki wangu watarajie mengi mazuri
kutoka kwangu, ninaamini nitafanya vizuri.
SHEIKH PONDA NA UAMSHO WAHUSISHWA NA SHAMBULIO LA TINDIKALI, ZANZIBAR
Gazeti la kila siku la Telegraph la hapa Uingereza linaripoti kuwa baadhi ya viongozi wa dini ya Kiislam visiwani Zanzibar wanaamini kuwa shambulio la tindikali dhidi ya mabinti wawili wa Kiingereza, Kirstie Trup na Katie Gee lilifanywa na wafuasi wa kikundi cha UAMSHO, ambacho kinataka Zanzibar ijitenge na Tanzania Bara na kisha kuanzisha sheria kali za Kiislam.
Huko nyuma kumeshatokea mashambulizi dhidi ya viongozi wa dini ya
Kiislam na Kikristo, ikiwa ni pamoja na mashambulio ya tindikali na
mauaji.
"Ofkoz, itakuwa kazi ya Uamsho," alinukuliwa Sheikh Fadhil Soraga,
aliyeshambuliwa kwa tindikali Novemba mwaka jana, na anaamini wahusika
katika tukio hilo dhidi yake walikuwa UAMSHO.
Wiki mbili zilizopita, vipeperushi vya vyenye wito mkali wa uchochezi
dhidi ya Wakristo vilisambazwa sehemu mbalimbali huo Zanzibar, tukio
linalohusishwa na harakati za UAMSHO.
"Siku 10 tu zilizopita, walikuwa wanasema wanaandaa kitu kikubwa. Tukio
hili, ambalo Waislamu wote twapaswa kulilaani, ni kazi ya kundi hilo
(UAMSHO)," alisisitiza Sheikh Soraga.
MWANAUME AFIA GESTI AKIFANYA MAPENZI NA MPENZI WAKE JIJINI DAR....!!!
MFANYABIASHARA wa sokoni Kariakoo jijini Dar ambaye pia ni mkazi wa Kigogo Flesh, Hamad Kiponda (46), amefia nyumba ya kulala wageni akiwa na mpenzi wake Latifa Saidi (25).
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi alisema tukio hilo lilitokea juzi saa saba mchana katika nyumba hiyo iitwayo Sansiro iliyoko Kiwalani kwa Gude.
Alisema kuwa kutokana na tukio hilo, Latifa alitoa taarifa polisi kwamba mpenzi wake aliishiwa na nguvu ghafla na kuanza kutokwa povu mdomoni wakati wakifanya mapenzi. Minangi alieleza kuwa mtoa taarifa huyo aliomba msaada kwa wahudumu wa gesti hiyo, lakini Kiponda alifariki papo hapo kabla ya kupelekwa hospitali.
Chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika, wakati mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi huku Latifa akishikiliwa kwa kuhojiwa.
Wakati huo huo, moto umezuka ghafla katika nyumba ya Matiku Nestori (43) mkazi wa Tuamoyo Kigamboni, yenye vyumba sita na kuteketeza vyumba vinne pamoja na mali zote zilizokuwemo ndani ambazo bado thamani yake haijajulikana. Kwa mujibu wa Kamanda Minangi tukio hilo lilitokea juzi saa nane mchana na chanzo cha moto huo inasadikiwa ni hitilafu ya umeme iliyosababisha moto kuanzia kwenye nguzo.
Alisema kuwa kutokana na tukio hilo, Latifa alitoa taarifa polisi kwamba mpenzi wake aliishiwa na nguvu ghafla na kuanza kutokwa povu mdomoni wakati wakifanya mapenzi. Minangi alieleza kuwa mtoa taarifa huyo aliomba msaada kwa wahudumu wa gesti hiyo, lakini Kiponda alifariki papo hapo kabla ya kupelekwa hospitali.
Chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika, wakati mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi huku Latifa akishikiliwa kwa kuhojiwa.
Wakati huo huo, moto umezuka ghafla katika nyumba ya Matiku Nestori (43) mkazi wa Tuamoyo Kigamboni, yenye vyumba sita na kuteketeza vyumba vinne pamoja na mali zote zilizokuwemo ndani ambazo bado thamani yake haijajulikana. Kwa mujibu wa Kamanda Minangi tukio hilo lilitokea juzi saa nane mchana na chanzo cha moto huo inasadikiwa ni hitilafu ya umeme iliyosababisha moto kuanzia kwenye nguzo.
MAN UNITED WAIBUKA VINARA WA NGAO YA HISANI BAADA YA KUITUNGUA WIGAN KWA MAGOLI 2 KWA O KATIKA DIMBA LA WEMBLEY
Meneja
Mpya Wa Man U David Moyes akiwa ameshika ngao ya Hisani pamoja na
Mchezaji wa Man U mara baada ya kukabidhiwa leo katika uwanja wa Wembley
baada ya kuitungua Wigan Kwa Magoli 2 kwa 0. Hili ni Kombe la Kwanza
kwa Kocha Mpya huyo wa Man United david Moyes
Wachezaji
wa Man U wakishangilia Mara baada ya Kuibuka Kinara kwa kuitungua Wigan
2 kwa 0 katika Mchezo wa Kuwania Ngao ya Hisani uliofanyika Katika
Dimba la Wembley Uingereza
Sunday, August 11, 2013
SERIKALI YA RWANDA IMEAPA KUTOWAFUKUZA WATANZANIA...!!!
Akizungumzia sakata la wahamiaji haramu wa Kinyarwanda kufukuzwa na serikali ya Tanzania amesema, kila nchi inayo mamlaka ya kufanya vile inafaa lakini ingekuwa vizuri Tanzania ingewasiliana na Rwanda ili kujua wataondokaje na kupokelewa vipi.
Amesisitiza, "Kwa kuwa wenzetu wameamua kufanya hivyo, tupo tayari kuwapokea wananchi wetu" Lakini pia, Waziri huyo amesema waasi wa FDRL ni kikundi cha wauaji wanaojipanga kuangamiza watu fulani nchini Rwanda hivyo wanatakiwa kupingwa kwa nguvu zote badala ya kuwatambua na kuzungumza nao kama kundi halali na lenye nia njema.
Naye Mtanzania Mohammed, amependekeza Rais Kagame na Kikwete wakutane na kufikia suluhu.Pia baadhi ya Wanyarwanda wamelalamikia kutokutendewa haki kwa kutenganishwa na wake,waume, n.k
TAARIFA RASMI YA JESHI LA POLISI KUHUSU KUPIGWA RISASI SHEKHE PONDA
Advera Senso- SSP-Msemaji wa Jeshi la Polisi.
--
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA
DAR ES SALAAM AGOSTI 10, 2013.
1. MNAMO
TAREHE 10, AGOSTI ,2013 MAJIRA YA SAA 8 MCHANA, MAENEO YA SHULE YA
MSINGI KIWANJA CHA NDEGE MANISPAA YA MOROGORO, KULIFANYIKA KONGAMANO LA
BARAZA LA EID LILILOANDALIWA NA UMOJA WA WAHADHILI MKOANI MOROGORO.
DAKIKA KUMI KABLA YA KONGAMANO HILO KUMALIZIKA ALIFIKA SHEKHE PONDA
ISSA PONDA AMBAYE ALIZUNGUMZA KWA MUDA MFUPI.
2.
KONGAMANO HILO LILIFUNGWA MAJIRA YA SAA 12:05 JIONI AMBAPO WATU
WALIANZA KUTAWANYIKA, BAADHI YAO WAKIWA WAMEZINGIRA GARI DOGO ALILOKUWA
AMEPANDA SHEKHE PONDA. BAADA YA KUTOKA KATIKA ENEO HILO, ASKARI WA
JESHI LA POLISI WALIZUIA GARI HILO KWA MBELE KWA NIA YA KUTAKA KUMKAMATA
SHEKHE PONDA AMBAYE MPAKA SASA ANATUHUMIWA KWA KOSA LA KUTOA MANENO YA
UCHOCHEZI SEHEMU MBALIMBALI HAPA NCHINI YENYE MLENGO WA KUSABABISHA
UVUNJIVU WA AMANI.
3.
BAAADA YA ASKARI KUTAKA KUMKAMATA, WAFUASI WAKE WALIZUIA UKAMATAJI HUO
KWA KUWARUSHIA MAWE ASKARI. KUFUATIA PURUKUSHANI HIYO, ASKARI WALIPIGA
RISASI HEWANI KAMA ONYO LA KUWATAWANYA.
4.
KATIKA VURUGU HIZO, WAFUASI HAO WALIFANIKIWA KUMTOROSHA MTUHUMIWA. HIVI
SASA IMETHIBITIKA KUWA SHEKHE PONDA YUKO KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA
MUHIMBILI AKITIBIWA JERAHA KATIKA BEGA LA MKONO WA KULIA LINALODAIWA
ALILIPATA KATIKA PURUKUSHANI HIZO.
5.
KUFUATIA TUKIO HILO, TIMU INAYOSHIRIKISHA WAJUMBE KUTOKA JUKWAA LA HAKI
JINAI IKIONGOZWA NA KAMISHINA WA JESHI LA POLISI CP ISSAYA MNGULU
IMEANZA KUFANYA UCHUNGUZI WA TUKIO HILO.
6. AIDHA, JESHI LA POLISI LINATOA WITO KWA WANANCHI KUWA WATULIVU WAKATI SUALA HILI LINASHUGHULIKIWA KISHERIA.
Imetolewa na:-
Advera Senso- SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Subscribe to:
Posts (Atom)