Ndizi ni tunda ambalo limezoeleka kwa watu wengi , linapatikana karibu kila mahali . Hata hivyo inawezekana ukawa hujafahamu umuhimu wa tunda hili mwilini mwako . Taarif aifuatayo itabadilisha mtazamo wako kwa tunda hili na utafahamu kwanini hupaswi kulichukulia poa hata siku moja .
Ndizi mbivu zina sukari zinazohitajika kwenye mwili wako , sukari hizi ni zile ambazo zinafahamika kwa majina ya kitaalamu ya Sucrose , Fructose na Glucose ambazo kwa pamoja zimechanganyikana na Fibre muhimu ambazo zinalifanya tunda hili kuwa chanzo muhimu cha nishati au nguvu inayohitajika mwilini mwako .
Utafiti umeonyesha kuwa ndizi mbivu mbili zinatosha kukupa nishati ambayo utaitumia kwa mazoezi ya nguvu ya dakika 90 ambazo ni sawa na saa moja na nusu . Hii ndio sababu wanamichezo wengi hutumia ndizi mbivu kabla na baada ya mazoezi mazito na wakati mwingine kabla na baada ya mashindano katika mchezo husika .
Nishati si faida pekee inayokuja kwenye tunda la ndizi , tunda hili lina faida nyingine ambayo ni kuusaidia mwili wako kupambana na kujikinga na maradhi kadhaa.