Wednesday, July 31, 2013

UN: VIFO VITOKANAVYO NA HIV VYAPUNGUA AFRIKA

hiv 8da7b

UMOJA wa Mataifa umetangaza kwamba Afrika imepiga hatua kubwa katika vita dhidi ya maambukizi ya Ukimwi.
Vifo vinavyotokana na maradhi ya Ukimwi Mashariki na Kusini mwa Afrika vimepungua kwa asili mia 40.

Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na ukimwi- UNAIDS umehusisha hatua za sasa na kutolewa kwa dawa za kukabiliana na makali ya Ukimwi. (HM)

Umoja wa Mataifa umesema mataifa ya Botswana, Ethiopia, Kenya, Zambia na Zimbabwe yamepunguza idadi ya watu wanaokufa kwa ukimwi kwa zaidi ya nusu.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa Maradhi nyemelezi ya kifua kikuu pia yamepungua sana tangu mwaka 2005. Chanzo: bbcswahili

Tuesday, July 30, 2013

KANISA KATOLIKI PAROKIA YA URU LAKUMBWA NA MAMBO YA KISHIRIKINA


HOFU kubwa imetawala Kanisa Katoliki Parokia ya Uru iliyopo Wilaya ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro, kutokana na matukio kadhaa yanayoendelea kutokea katika kanisa hilo huku baadhi ya watu wakiyahusisha na imani za kishirikina. 

  Katekista wa parokia hiyo, Lucian Tesha, aliwaambia waamini waliokusanyika katika ibada ya misa ya kwanza kanisani hapo juzi Jumapili kuwa usalama katika kanisa hilo upo shakani na kuwataka kuwa macho.

Hali hiyo inatokana na kile alichodai kuwa kuna mtu mmoja (mwanaume) kwamba amekuwa akionekana eneo la kanisa akiweka vitu mbalimbali ambavyo havina nia njema na kanisa hilo la Moyo Mtakatifu wa Yesu.
 
“Mtu huyu ameonekana kanisani hapa kwa mara ya nne sasa, hatujui anataka nini, lakini amekuwa akiweka vitu mbalimbali katika sanamu ya Bikira Maria na karibu na sakristi ya mapadri…kwa kweli hali hii inatisha.

OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA YAWACHANA CHADEMA...!!!


 
OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa, imesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) hakina ubavu wa kumkataa au kutomtambua John Tendwa kuwa ndiye msajili wa vyama vya siasa nchini.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Msajili wa Vyama vya Siasai, Rajab Baraka alipozungumza na MTANZANIA kuhusu kauli iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa aliyedai chama hicho hakimtambui John Tendwa kuwa ndiye msajili wa vyama vya siasa.

Katika madai yake Dk. Slaa alidai Tendwa anakipendelea CCM katika kutoa haki ya demokrasia na hatendi haki kama mlezi wa vyama vyote vya siasa nchini.

Dk. Slaa alisema hayo wiki iliyopita alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari na kusisitiza hata katika barua zao za mawasiliano kwenda kwa ofisi ya msajili chama hicho hakitumii jina la John Tendwa.

MSHIRIKI WA BBA...... "NIMELALA NA WANAUME MATAJIRI KWASABABU YA PESA ZA KUHUDUMIA FAMILIA YANGU"

It seems Beverly Osu no longer remember that cameras and microphones are everywhere in the Big Brother Africa house and as such whatever she says or do will being captured and transmitted to viewers. That could only explain why she revealed her top secret to her in-house lover, Angelo, without thinking twice in one of their recent get together sessions. Talking about her "runs" life in Lagos, Beverly said:
"I’ve done all sorts. I’ve slept with men for money when I had to take care of my family." We observed that it was also in the Big Brother house that Beverly revealed the fact that she had once aborted a four-month old pregnancy she had for her estranged boyfriend.
Beverly also confirmed that she once dated singer 2shotz, but the newly married singer is denying her.

VIWANGO VIPYA VYA MISHAHARA YA WATUMISHI WA SERIKALI 2013.

TGOS A
TGOS A 1. (Sh240,000), TGOS A 2. (Sh245,600), TGOS A 3. (Sh251,200), TGOS A 4. (Sh256,800), TGOS A 5. (Sh262,400), TGOS A 6. (Sh268,000), TGOS A 7.(Sh272,000), TGOS A 8(Sh279,000), TGOS A 9.(Sh284,800), TGOS A 10(Sh290,400), TGOS A 11(Sh296,000), TGOS A 12(Sh301,600), TGOS A 13(Sh 307,200), TGOS A 14(Sh312,800), TGOS A 15(Sh 318,400), TGOS A 16(Sh324,000), TGOS A 17(Sh329,600) na TGOS A 18(Sh335,200).
TGOS B
TGOS B 1. (Sh347,000), TGOS B 2. (Sh356,500) TGOS B 3 . (Sh366,000), TGOS B 4 . (Sh375,500), TGOS B 5. (Sh385,000), TGOS B 6. (Sh394,500), TGOS B 7. (Sh404,000), TGOS B 8. (Sh413,500), TGOS B 9. (Sh423,000), TGOS B 10. (Sh432,500), TGOS B 11 . (Sh442,000) na TGOS B 12. (Sh451,500).
TGOS C
TGOS C 1 . (Sh471,000), TGOS C 2 . (Sh482,000), TGOS C 3 . (Sh493,000), TGOS C 4. (Sh504,000), TGOS C 5. (Sh515,000), TGOS C 6. (Sh526,000), TGOS C 7. (Sh537,000), TGOS C 8. (Sh548,000), TGOS C 9. (Sh559,000), TGOS C 10. (Sh570,000), TGOS C 11. (Sh581,000) na TGOS C 12. (Sh592,000).

RAIS KIKWETE AINGILIA KATI UGOMVI WA WAZIRI KAGASHEKI NA MEYA

  Rais Jakaya Kikwete ameingilia kati ugomvi uliopo kati ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Hamis Kaghasheki na Meya wa Manispaa ya Bukoba, Dk. Anatoli Amani, kwa kuwataka wakae chini na kumaliza tofauti zao kwani hakuna lisilokuwa na mwisho.

Rais aliyasema hayo katika uwanja wa Kaitaba alipokuwa akihitimisha ziara yake mkoani Kagera aliyoanza Jumatano wiki iliyopita.

“Mbunge na Meya wakiendelea kutiliana shaka wanaoumizwa ni wananchi, malizeni tofauti zenu kwa sababu hakuna lisilokuwa na mwisho,” alisema.

Hata hivyo, Rais Kikwete alisema masuala yaliyokuwa yakiwagonganisha Meya na Balozi Kaghasheki ambaye ni Mbunge wa Bukoba Mjini, ya ujenzi wa soko pamoja na viwanja ni mambo ya maendeleo.

WAFUNGWA MBEYA WAMUOMBA NCHIMBI KUCHUNGUZA MAUAJI GEREZANI...!!!



WAFUNGWA wa Gereza  la Ruanda lililopo mjini Mbeya wameiomba ofisi ya Waziri wa Mambo  ya ndani ya nchini kuunda tume huru kuchunguza mauaji ya kikatili ya mahabusu wawili katika Gereza hilo.



Kupitia barua ya Septemba 22,2012 ya wafungwa hao kwenda ofisi hiyo, imesema kuwa kama si lengo la kupunguza ufanisi wa kazi za waziri wa Wizara hiyo basi ni mikakati iliyoundwa kwa ajili ya kuchafua wizara nzima.



‘’Mhe. Waziri, Uongozi wa Gereza hili la Ruanda umekabidhi Mamlaka ya utendaji wa shughuli za gereza mikononi mwa kundi dogo la wafungwa wanne, kundi hilo ujulikana kwa jina la Maumau’’ imesema barua hiyo yenye kurasa tatu.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE JULAI 30, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


DSC 0001 665f7
DSC 0002 d25e1

MHE. PANDU KIFICHO ALITAHADHARISHA BARAZA LA WAWAKILISHI KUWA MAKINI KUFANYA MAAMUZI YAKE

mr-pandu-ameir-kifichoNa Ali Issa-Maelezo Zanzibar 
Spika wa baraza la wakilishi Zanzibar Pandu ameir kificho amesema Baraza la wakilishi liwe na Tahadhari sana kufanya maamuzi ambayo utekelezaji wake umo katika mikono ya Serikali ili kuiepusha Serikali kuja kuingia katika kitahanani kwa lile amblo kulitimizia Taifa mahitaji yake muhimu.
 
Hayo ameyasema  leo huko Baraza la wakilishi  wakati alipokuwa akitoa ufafanuzi kwa mwakilishi wa Kwamtipura CCM  Hamza Hassan Juma wakati alipokuwa amezuia kifungu kuipitisha Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kusema uagiziaji wa kuku kutoka Nnje uzuuliwe kwani una uwasokosesha mapato wafugaji wa ndani na kuliua soko lao.
 
Amesema si vyema kutoa maamuzi ya moja kwa moja kulilazimisha hilo kuzuia kuku kutoka nje wasiletwe nchini bila ya kuwa na utafiti wa
kutosha utao bainisha wazi kuwa hawahitajiki kuku wa nje.
 
 “sivizuri kuzuia fungu hili na kukusema kuku wasiagiziwe kutoka nje bali tuwachie Serikali wakachunguze ukweli wa hilo na baadae watuleteeripoti,”alisema Spika.
Aidha ali sema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina wapenda sana wananchi wake kuona kua wanafanikiwa katika uzalishaji kwani ndio
lengo la Serikali yao kujikwamua na umasikini na kujipatia kipato wawe makini kuliko kuchukuwa maamuzi ya haraka.

Monday, July 29, 2013

CHANGUDOA APAWE KICHAPO NA WENZAKE KWA KUUZA MWILI WAKE KWA BEI YA CHINI...!!!

 
 
Kwa hali isiyo ya kawaida changudoa mmoja huko Naivasha Nairobi Alipewe kichapo cha mbwa mwizi Baada ya kugundulika na wenzake kuwa huwa anauza kwa bei ndogo na saa zingine huwa anatoa kwa mkopo..kitendo hicho kimelaaniwa na wenzake kwa vile kinapunguza bei yao na kuonekana kuwa si  wa gharama...inafikia kipindi watu wanaokuja wanamtafuta yeye tu kwa vile ni wa bei ya chini ..... “Kwani unafikiria sisi tutakula wapi kama utaendelea kujiuza hii bei hasara" Alisikia Changudoa mmoja akisema huku akishusha kichapo...
Watu mbali mbali waliingilia kati na kuanza kumuokoa katika kichapo hicho... Mteja mmoja alisikika akisema: “Unajua huyu mama huwa ananipatia kwa credit on a bad day so siwezi muacha auliwe na hawa wenzake (she offers me services on credit when I’m broke so I can’t let them kill her),”

HILI NDILO GARI LILILOSHAMBULIWA AMBALO LILIKUWA LIMEBEBA ASKARI WA TANZANIA HUKO DARFUR

 
 


DIAMOND AENDA KUSOMA AFRIKA YA KUSINI...!!!



MAMA AMCHOMWA MWANAE NA MKASI MARA 90 KWA MADAI YAKUMG'ATA ZIWA AKIWA ANANYONYA....!!!

Maskini unyama mwingine hauna hata maana maybe alikuwa amechanganyikiwa
Kweli ukistaajabu ya Musa....
Ni kama miujiza kwa mtoto wa kichina kuwa hai mpaka sasa licha ya kuchomwa chomwa mara 90 na mama yake mzazi huko China kwa madai kuwa alimng’ata ziwa mama yake wakati akinyonyeshwa.
Kwa mujibu wa Daily Mail mtoto huyo Xiao Bao mwenye miezi 8 tu ameshonwa zaidi ya nyuzi 100 ili kuurudisha uso wake katika hali nzuri baada ya shambulizi hilo lililotokea katika jiji la Xuzhou mashariki mwa China.
Bao anaishi na mama yake pamoja na wajomba zake wawili ambao wanajishughulisha na ukusanyaji wa taka kwaajili ya kipato. Mmoja wa wajomba hao ndiye aliyegundua kuwa Bao ameumizwa baada ya kumkuta akiwa amelala kwenye damu iliyotapakaa nyumbani hapo kabla hajamkimbiza hospitali
Mama wa mtoto huyo baadaye alikiri kumchoma choma mwanae na mkasi mara 90 hususan eneo la usoni baada ya mtoto huyo kumng’ata ziwa wakati akimnyonyesha.
Baada ya tukio hilo majirani wa familia hiyo wameiomba serikali imnyang’anye mama huyo wa kichina mtoto kwa sababu za kiusalama, lakini ombi hilo limekataliwa kwa madai kuwa hakuna uthibitisho wowote mpaka sasa kama mwanamke huyo anamatatizo ya akili, lakini wameongeza kuwa hata hivyo mtoto huyo bado ana walezi wengine wawili anaoishi nao (wajomba zake)
Mtoto huyo anaendelea kupata nafuu akiwa hospitali.

Source: Vijimamo

RAIS KIKWETE ATAWAZWA OMUKUMA (CHIFU) WA MISSENYI, AHITIMISHA ZIARA YA KAGERA

  Rais Jakaya Kikwete akitawazwa kuwa Omukama (Chifu) wa Missenyi wakati wa ziara yake ya siku sita mkoani Kagera. Anayemsimika ni kiongozi wa wazee wa Missenyi, Mzee Ernest Babeiya.
 Kwa heshima kubwa Rais Jakaya Kikwete akivishwa uchifu.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia maelefu ya wananchi wa mkoa wa Kagera waliofurika katika uwanja wa michezo wa Kaitaba kumsikiliza siku ya mwisho ya ziara yake ya siku sita mkoani humo.
 
PICHA NA IKULU

MAGAZETI YA LEO JUMATATU JULAI 29, 2013

DSC 0428 06f2f
DSC 0429 f6f98

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...