Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali nchini imesema karibu nusu ya watu waliojitokeza kupima vinasaba (DNA) ili kubaini uhalali wa watoto wao, vipimo vimeonesha si wazazi halisi wa watoto waliopimwa.
Takwimu hizo ni kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2010, ikionesha kuwa, asilimia 48.32 ya wazazi 'wanalea' watoto wasio wa kwao wakati asilimia 51.68 ndio wazazi halali.
Hayo yameelezwa jana na Mkuu wa Kitengo cha Makosa ya Jinai, Vinasaba na Baiolojia wa ofisi hiyo, Gloria Machuve katika mkutano na wanahabari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dar es Salaam.