Watanzania wenzangu,
Ni dhahiri kumekuwa na mijadala kadha wa kadha kuhusu vyama vya siasa kuwa na vijana wao wa kuwa linda.
Nilionesha tofauti baina ya red brigade na greenguard. Wanaojitetea wakakimbilia Dictionary bila kutumia muda kufuatilia historia na chimbuko la kikundi hicho ambacho jina , matendo na malengo yake yako sawasawa na kule kilikoanzia.
Lakini mjadala mkubwa ni kuhusu mpango wa CHADEMA kuanzisha jeshi lao la chama chao, Jeshi ambalo halihitaji msaada wa polisi wala wa Jeshi la wananchi wa Tanzania kwa mjibu wa kauli ya mkt wao mhe Mbowe.
Ni kinyume na katiba ya nchi na hata katiba ya chama chao (pitia katiba yao). Wanavunja katiba hiyo sio kwa bahati mbaya bali ni mpango wao unawabana wa kuhakikisha amani ya nchi inatoweka .
Jeshi wanalotaka kulianzisha si bahati mbaya,ni mpango wa siku nyingi hasa ukifuatilia walikojifunzia ideology ya Red Brigade na aliyeileta CHADEMA.
MAANA HALISI YA RED BRIGADE NA WAANZILISHI WA HIYO TAASISI.
Red Brigade ilianzia ITALIA mwaka 1970 kwa kifupi ni BR,Wanzilishi wake anafahamika kwa jina la Renato Curcio na Margherita(mara) Cagol waliokutana wakiwa wanafunzi chuo kikuu cha Trento karibu na chuo alichokuwa akisoma Dr Slaa.