Ni takribani siku sita sasa toka wasichana wawili raia wa Tanzania
Agnes Gerald na Melisa Edward kukamatwa katika uwanja wa ndege wa OR
Tambo Afrika Kusini wakitokea Tanzania, wakituhumiwa kusafirisha dawa za
kulevya aina ya Crystal Methamphetamine yenye thamani ya zaidi ya
billion 6 za Tanzania.
Swala
linalozua maswali mengi ni jinsi gani wasichana hao waliweza kupita
katika uwanja wa ndege Julius Nyerere na karibia kilo 150 za dawa hizo
za kulevya, kiasi ambacho Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini imesema
ndio mzigo mkubwa zaidi wa dawa za kulevya kuwahi kukamatwa katika
mipaka yote ya nchi hiyo kama mzigo mmoja (kwa lugha nyingine imevunja
rekodi).
Idara ya polisi nchini Tanzania imekiri kuwa Agnes na Melisa walipitia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, na walisafiri na ndege ya shirika la ndege la South African Airways inayomilikiwa na serikali ya Afrika Kusini.