Tuesday, July 02, 2013

ANGALIA PICHA ZA GEORGE BUSH ALIPOKUTANA NA RAIS OBAMA TANZANIA KABLA HAJAONDOKA

  
Rais Obama pamoja na Bush walikutana leo Asubuhi katika Ubalozi wa Marekani uliopo jijini Dar es Salaam na kufanya tendo la kutoa heshima zao kwa Walipoteza Maisha pamoja na wale wote walioathirika katika shambulio la Ugaidi katika Ubalozi wao hapa nchini mwaka 1998.




RAIS BARACK OBAMA WA MAREKANI AMALIZA ZIARA YAKE YA SIKU MBILI HAPA NCHINI


 
Rais Barack Obama wa Marekani ameondoka nchini mchana huu kurudi nchini Marekani,baada ya kumaliza  ziara yake ya siku mbili hapa nchini iliyoanza jana.Rais Obama na mwenyezi wake Rais Jakaka Kikwete,leo walifanya ziara ya kutembelea mitambo ya kuzalisha umeme ya Symbion
iliopo Ubungo jijini Dar es Salaam na kuzindua rasmi mradi huo.

MAREKANI KUFUNGUA UKURASA MPYA KATIKA UWEKEZAJI NCHINI.

3
Rais wa Marekani Barack Obama akiwahutubia wafanyabiashara leo(jana) jijini Dar es salaam juu ya mpango wa Nchi yake wa kufungua milango ya ushirikiano na uwekezaji kwa Nchi za Afrika Mashariki katika sekta mbalimbali na hivyo kuongeza kiwango cha bidhaa ya Afrika Mashariki zinazoingia nchini Marekani.
4
Rais wa Marekani Barack Obama akiwa katika mkutano jana (leo) jijini Dar es salaam wa kujadiliana na watendaji wakuu(CEO) wa Makampuni mbalimbali yaliyowekeza Afrika juu ya kuimarisha fursa za ushirikiano kati ya Marekani na Afrika katika uwekezaji kwenye sekta mbalimbali za maendeleo.
(Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es salaa)
………………………………………………
 
Na Eleuteri Mangi—MAELEZO—Dar es salaam
Serikali ya Marekani imeahidi kufungua ukurasa mpya kwa Nchi za Afrika Mashariki kwa kuongeza uwekezaji katika sekta mbalimbali ili kuinua uchumi wan chi hizo.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dar es salaam na Rais Barack Obama kwenye hotuba yake kwa wafanyabiashara wakati wa ziara yake ya siku mbili nchini Tanzania.
Alisema kuwa hatua hiyo inalenga kuongeza kiwango cha bidhaa kutoka Nchi za afrika Mashariki kuingia nchini Marekani na hivyo kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na kiuchumi kwa manufaa ya pande zote.
 “Sasa ni wakati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwekeza nchini Marekani  ili kuongeza mauzo yake nchini Marekani hadi ifike asilimia 40,” alisema Rais Obama.

NANDO WA TANZANIA APENDEKEZWA KUTOKA NDANI YA JUMBA LA BIG BROTHER...KURA YAKO INAHITAJIKA


Mchezo unazidi kuwa mgumu kadri siku zinavyozidi kwenda sababu idadi ya wanaopaswa kuendelea na mchezo ndivyo inavyohitajika kuwa ndogo mpaka siku ya 91 atakapobaki mtu mmoja wa kukabidhiwa $300,000 kama zawadi ya BBA The Chase. 

Nominations za wiki hii zimewagusa baadhi ya washiriki ambao hawajawahi kabisa kupendekezwa kutoka, na wengine ambao wameshawahi kupendekezwa mara moja na zaidi lakini waliokolewa na kura za watazamaji.

Baada ya kupona kutoka wiki iliyopita na kuwa HOH , cheo kilichompa nafasi ya kujiokoa katika nomination zilizopita Nando wa Tanzania ameungana na washiriki wengine 6 katika orodha ya majina yaliyotajwa na Biggie kuingia katika kikaango cha eviction ya wiki hii.

Washiriki ambao wameingia kwa mara ya kwanza katika nominations za wiki hii ni pamoja na aliyekuwa kipenzi cha Huddah mjengoni, Angelo wa Afrika Kusini ambaye amewekwa na HOH wa wiki hii Elikem aliyejiokoa na nafasi yake kumuwekea yeye.

Fatima wa Malawi, Bimp wa Ethiopia pamoja na Cleo wa Zambia ndio washiriki wengine ambao wameingia dangerzone kwa mara ya kwanza toka mchezo umeanza.

Washiriki ambao waliwahi kupendekezwa na kuokolewa na kura za watazamaji na wameingia tena wiki hii ni pamoja na Pokello wa Zimbabwe, Hakeem wa Zimbabwe pamoja na Nando wa Tanzania.

Wiki hii Ghana na Nigeria ndio zimekalia viti vya utawala wa nyumba, Ruby ikiongozwa na Elikem na Melvin akiiongoza Diamond.

Kura yako inahitajika kumwokoa Nando ili aendelee kubaki na kuiwakilisha Tanzania katika msimu wa 8 wa BBA The Chase unaoendelea Afrika Kusini.

MAHAKAMA YAWATIA MBARONI WAPENZI WAWILI WALIOAMUA KUTALII WAKIWA UCHI....!!!


Njemba moja, Stephen Gough aliyewahi kuwa mwanajeshi amekamatwa na polisi katika Jiji la Portsmouth, Uingereza baada  ya kukutwa na mpenzi wake wakidunda kutalii mitaani wakiwa uchi wa nyama.

Mwanamke Melodine Roberts aliyefuatana naye aliachiwa na polisi kwa kuwa mara baada ya kuonywa kuacha tabia hiyo, aliacha lakini mpenzi wake huyo aligoma na hii ni mara ya 14 akifanya hivyo licha ya kufungwa jela huko nyuma.
 
Baada ya kugoma polisi walimfunga pingu na wakampeleka mahakamani moja kwa moja  ambapo Mwendesha Mashitaka, Simon Jones alisema Gough alikuwa amekiuka sheria na aliwahi kufungwa miaka sita na moja ya makosa yaliyosababisha  afungwe ni kutemba uchi wa mnyama hadharani.
 
Baada ya maelezo hayo, jaji aliyekuwa akisikiliza shauri hilo, Sarah Munro alisema kuwa kwenda jela kwa mtu huyo ndiyo ilikuwa njia pekee kwake kwa kuwa hilo ni kosa kubwa katika jamii ya Waingereza na ni ukiukwaji wa taratibu za umma wa sehemu hiyo.

POLISI WALA KICHAPO KIKALI KUTOKA KWA POLISI WENZAO BAADA YA KUKAIDI AMRI...!!!



MAAFISA watatu wa polisi wa utawala (AP) walijeruhiwa kwenye mapigano yaliyozuka kati yao na wenzao wa Uganda kwenye kisiwa kinachozozaniwa cha Migingo.

Mzozo huo wa mwishoni mwa wiki ulianza pale maafisa wa Uganda waliokuwa na sare rasmi walipoenda katika ufuo wa karibu wa Nyandiwa kurekebisha mashua yao.




Lakini wakazi wa Nyandiwa waliwazuia kutia nanga wakisema kwa vile walikuwa na sare na bunduki, walihofia wangeliwahangaisha kwa kuwapokonya samaki wao.

Mmoja wa wavuvi wa eneo hilo Bw Oloo Okello, alisema maafisa hao wa Uganda walirejea Migindo wakuwa na hasira bila ya kurekebisha boti lao.



“Waliporejea walisema kwamba polisi wa Utawala wa Kenya wa kitengo cha kushika doria mpakani, Rural Border Patrol Unit (RBPU), walio kisiwani Ugingo hawatakiwi kutia guu Migingo.

TANZANIA YAUMBULIWA....GAZETI MAARUFU LA MAREKANI LAANIKA UKATILI UNAOTENDEKA NCHINI

 


Tanzania imekosolewa na gazeti maarufu la Marekani wakati Rais Obama akipokewa kwa nderemo na vifijo.
Gazeti hilo maarufu nchini Marekani la The New York Times, limechapisha habari za kuonesha matukio ya ukatili yanayofanyika Tanzania.
Habari hiyo iliyochapishwa katika toleo lake ya Juni 30, imeleza tukio la kuteswa na kuumiza kwa kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Stephen Ulimboka.
Mwandishi wa habari hiyo amejaribu kunukuu kauli ya Dk. Ulimboka akieleza jinsi alivyotekwa na kuteswa kinyama kisha kutupwa kwenye Msitu wa Mabwepande.

Mwandishi huyo amesema kuwa Tanzania inaheshimika nje ya nchi kama kisiwa cha amani ndani ya ukanda wenye machafuko wa Afrika Mashariki.
Kwamba kutokana na sifa hizo, Tanzania imejizolea sifa na ufadhili wa fedha kutoka kwa mataifa mbalimbali yaliyoendelea, ikiwamo Marekani, ambayo mwaka jana
iliipatia zaidi ya dola milioni 480.

Alisema kuwa wakati Rais Obama akiwasili Tanzania makundi ya kutetea haki za binadamu na chama kikuu cha upinzani wanasema matukio ya vitisho na ukandamizaji wa wapinzani wa kisiasa yanashika kasi. “Kuna woga, si amani”.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE JULAI 2, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

DSC 0161 a3658

DSC 0157 db3db



DSC 0158 c75a3

JINSI CIA NA FBI WALIVYOMLINDA RAIS OBAMA KWA ULINZI MKALI AJABU



Helikopta ya Polisi ikiwa katika doria ya hapa na pale, hata hivyo eneo lote la uwanja wa Ndege ulidhibitiwa na Wamarekani wenyewe ikiwemo na kazi ya kuongoza ndege. 
Ulinzi kila kona
Ulinzi ulimarishwa.
Bendera ya Tanzania ikiwekwa katika gari lililombeba Rais wa Marekani, Barack Obama.
Gari alilopanda Rais Obama
(Picha na Habari Mseto Blog)

KIKAPTURA KIFUPI CHA MTOTO WA KIKE WA RAIS OBAMA CHAZUA GUMZO KUBWA

Binti mdogo wa rais Barack Obama, Sasha, alikua jijini New York hivi karibuni akifanya shopping huku
amevaa kikaptura kifupi (short shorts, al maarufu kama daisy dukes.) Mapaparazzi walimpiga picha binti huyo akiwa mitaani na raha zake na kuuliza mitandaoni kama ni sahihi kwa binti wa miaka 12, kuvaa kaptura fupi hivyo. Kama kawaida za mitandaoni, kilichozuka ni ubishi mkali kati ya wanaoona si sahihi, hasa kwa binti ya rais, na wale wanaoona ni poa tu. Wewe upo kwenye camp ipi? Unaweza ruhusu binti yako avae kaptura kama hii?



Monday, July 01, 2013

MAGAZETI YA LEO JUMATATU JULAI 1, 2013


DSC 0234 1d864 
DSC 0233 b4230

HUU NDIO UJUMBE MZITO TOKA KWA ZITTO KABWE KWENDA KWA OBAMA

Obama: Tunataka Uwazi wa Mikataba. Omba radhi Kwa mauaji ya Lumumba

    Hatimaye Barack Obama, Rais wa Marekani anatembelea tena bara la Afrika. Hii itakuwa ni mara ya pili Obama kutembelea Bara hili alikotoka baba yake baada ya ziara yake ya kwanza mwaka 2009. Mwaka huo alitembelea Ghana na Misri ilhali mwaka huu anatembelea Senegali, Afrika Kusini na Tanzania. Ziara hiyo itakayoanza tarehe 26 mwezi Juni, itamfikisha Tanzania tarehe 1 Julai na kuondoka siku ya pili yake.

    Uchaguzi wa Obama kuwa Rais wa Marekani ulipokolewa kwa shangwe Afrika nzima. Wakati Waziri wa mambo ya nje wa Nigeria alilia kwa furaha, nchi ya Kenya ilitangaza siku ya mapumziko na Rais wa zamani wa Afrika Kusini ndugu Nelson ‘Madiba’ Mandela alisema ‘ushindi wa Obama unawafanya Waafrika wathubutu kuota ndoto (Jarida la The Economist). Hapa Tanzania kulikuwa kuna shamra shamra za kila namna na magazeti yaliweka vichwa vya habari kana kwamba ni Rais wa Tanzania aliyechaguliwa.

    Waafrika walikuwa na matumaini makubwa sana na bwana Obama. Yamefikiwa?
    Ni vema ifahamike kuwa Barack Obama ni Rais wa Marekani na siku zote atalinda maslahi ya Marekani tu. Kuwa na matumaini makubwa kwamba labda yeye angeliweza kuiweka Afrika mbele sana ilikuwa ni kujifurahisha tu nafsi. Maslahi ya Marekani ni ya kipaumbele kuliko kitu kingine chochote kwa Rais Obama. Kwa wengi Obama amekuwa kama amewavunja moyo.

WATANZANIA 60 WAKAMATWA ZIARA YA OBAMA....!!!

Watanzania 60 wamekamatwa Afrika Kusini kutokana na maandalizi yaliofanyika nchini humo ya kumpokea Rais Barack Obama wa Marekani.

Rais Obama amewasili Afrika Kusini juzi kwa ziara ya siku tatu akitokea Senegal.

Watu hao wamekamatwa baada ya kudaiwa kuishi kinyume cha sheria Afrika Kusini. Baada ya Watanzania hao kutiwa mbaroni na vyombo vya usalama wamehifadhiwa hapa nchini kusubiri  hatua za kisheria zaidi.

Ofisa mmoja wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, Sadiki Msele amesema Watanzania hao walirejeshwa nchini jana na kwamba hivi sasa wanasubiri sheria kuchukua mkondo wake.

“Safisha safisha kama iliofanyika jijini Dar es Salaam, pia imefanyika Afrika Kusini na kuwaathiri wafanyabiashara na watu wengine,” amesema ofisa huyo.

Hivi sasa Rais Obama yupo Afrika Kusini akiwa ameongoza na mkewe Michelle Obama na watoto wao wawili; Malia na Sasha.

Leo Rais Obama na ujumbe wake anatarajiwa kutua Tanzania kwa ziara ya siku mbili na Jumanne ataondoka kurejea Marekani.

ANGALIA MITAA MBALIMBALI YA BONGO ILIVYOPAMBWA KWA MAANDALIZI YA UJIO WA OBAMA

 
 
 
 
Barabara ya Baharini mchana wa leo, ikiwa shwari huku ikiwa imepambwa na mabango yenye picha za Rais wa Marekani, Barack Obama na Bendera za Nchi hiyo na Tanzania. KARIBU OBAMA
 
credit: sufiani mafoto

WAPENZI WADONDOKA NA KUFA WAKATI WAKIFANYA MAPENZI DIRISHANI...!!!

 
Wapenzi wameanguka na kufa baada ya dirisha walipokuwa wakifanyia mapenzi kufunguka ghafla nchini China.

Wawili hao wanasemekana kudondoka kutoka kwenye dirisha la jengo moja la makazi kwenye jiji la Wuhan nchini humo pale dirisha hilo walilokuwa wameegemea kufunguka.

Mashuhuda walivieleza vyombo vya habari vya China kwamba wapenzi hao walikumbatiana wakati wakianguka kwenye njia ya waenda kwa miguu nje.
Kwa mujibu wa The Sun, chanzo kimoja cha habari kilisema: "Huku wawili hao wakiwa wameshikamana vilivyo, walianguka nje ya jengo hilo."
Picha za kuogofya zimefichuliwa kwenye tovuti za nchini humo zikionesha wapenzi hao wakiwa wamefunikwa kwa mashuka na polisi.
Damu ilitapakaa kwenye njia ya waenda kwa miguu karibu na wapelelezi wanaonekana wakichunguza eneo la tukio.
Miili ya wapenzi hao ilipigwa picha karibu na baiskeli ambayo ilikuwa imelazwa chini, lakini hakukuwa na ripoti zozote kwamba yeyote chini alikuwa amejeruhiwa katika ajali hiyo.
Ripoti zinasema kwamba madirisha hayo kwenye jengo hilo la makazi yalikuwa hayana ubora unaotakiwa.
Inafikiriwa kwamba mwanaume huyo na mwanamke wanawezekana walikuwa wakijaribu kujipooza kando ya dirisha hilo ndipo tukio hilo likatokea.
Haikufahamika ni umbali gani kutoka juu wawili hao walikuwa wakati wakianguka.
Wuhan ni jiji maarufu zaidi lililopo katikati ya China.
Ukiwa na historia ya miaka 3,500 ni moja kati ya miji mikongwe na iliyostaarabika katika China.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...