Tuesday, July 02, 2013

POLISI WALA KICHAPO KIKALI KUTOKA KWA POLISI WENZAO BAADA YA KUKAIDI AMRI...!!!



MAAFISA watatu wa polisi wa utawala (AP) walijeruhiwa kwenye mapigano yaliyozuka kati yao na wenzao wa Uganda kwenye kisiwa kinachozozaniwa cha Migingo.

Mzozo huo wa mwishoni mwa wiki ulianza pale maafisa wa Uganda waliokuwa na sare rasmi walipoenda katika ufuo wa karibu wa Nyandiwa kurekebisha mashua yao.




Lakini wakazi wa Nyandiwa waliwazuia kutia nanga wakisema kwa vile walikuwa na sare na bunduki, walihofia wangeliwahangaisha kwa kuwapokonya samaki wao.

Mmoja wa wavuvi wa eneo hilo Bw Oloo Okello, alisema maafisa hao wa Uganda walirejea Migindo wakuwa na hasira bila ya kurekebisha boti lao.



“Waliporejea walisema kwamba polisi wa Utawala wa Kenya wa kitengo cha kushika doria mpakani, Rural Border Patrol Unit (RBPU), walio kisiwani Ugingo hawatakiwi kutia guu Migingo.

TANZANIA YAUMBULIWA....GAZETI MAARUFU LA MAREKANI LAANIKA UKATILI UNAOTENDEKA NCHINI

 


Tanzania imekosolewa na gazeti maarufu la Marekani wakati Rais Obama akipokewa kwa nderemo na vifijo.
Gazeti hilo maarufu nchini Marekani la The New York Times, limechapisha habari za kuonesha matukio ya ukatili yanayofanyika Tanzania.
Habari hiyo iliyochapishwa katika toleo lake ya Juni 30, imeleza tukio la kuteswa na kuumiza kwa kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Stephen Ulimboka.
Mwandishi wa habari hiyo amejaribu kunukuu kauli ya Dk. Ulimboka akieleza jinsi alivyotekwa na kuteswa kinyama kisha kutupwa kwenye Msitu wa Mabwepande.

Mwandishi huyo amesema kuwa Tanzania inaheshimika nje ya nchi kama kisiwa cha amani ndani ya ukanda wenye machafuko wa Afrika Mashariki.
Kwamba kutokana na sifa hizo, Tanzania imejizolea sifa na ufadhili wa fedha kutoka kwa mataifa mbalimbali yaliyoendelea, ikiwamo Marekani, ambayo mwaka jana
iliipatia zaidi ya dola milioni 480.

Alisema kuwa wakati Rais Obama akiwasili Tanzania makundi ya kutetea haki za binadamu na chama kikuu cha upinzani wanasema matukio ya vitisho na ukandamizaji wa wapinzani wa kisiasa yanashika kasi. “Kuna woga, si amani”.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE JULAI 2, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

DSC 0161 a3658

DSC 0157 db3db



DSC 0158 c75a3

JINSI CIA NA FBI WALIVYOMLINDA RAIS OBAMA KWA ULINZI MKALI AJABU



Helikopta ya Polisi ikiwa katika doria ya hapa na pale, hata hivyo eneo lote la uwanja wa Ndege ulidhibitiwa na Wamarekani wenyewe ikiwemo na kazi ya kuongoza ndege. 
Ulinzi kila kona
Ulinzi ulimarishwa.
Bendera ya Tanzania ikiwekwa katika gari lililombeba Rais wa Marekani, Barack Obama.
Gari alilopanda Rais Obama
(Picha na Habari Mseto Blog)

KIKAPTURA KIFUPI CHA MTOTO WA KIKE WA RAIS OBAMA CHAZUA GUMZO KUBWA

Binti mdogo wa rais Barack Obama, Sasha, alikua jijini New York hivi karibuni akifanya shopping huku
amevaa kikaptura kifupi (short shorts, al maarufu kama daisy dukes.) Mapaparazzi walimpiga picha binti huyo akiwa mitaani na raha zake na kuuliza mitandaoni kama ni sahihi kwa binti wa miaka 12, kuvaa kaptura fupi hivyo. Kama kawaida za mitandaoni, kilichozuka ni ubishi mkali kati ya wanaoona si sahihi, hasa kwa binti ya rais, na wale wanaoona ni poa tu. Wewe upo kwenye camp ipi? Unaweza ruhusu binti yako avae kaptura kama hii?



Monday, July 01, 2013

MAGAZETI YA LEO JUMATATU JULAI 1, 2013


DSC 0234 1d864 
DSC 0233 b4230

HUU NDIO UJUMBE MZITO TOKA KWA ZITTO KABWE KWENDA KWA OBAMA

Obama: Tunataka Uwazi wa Mikataba. Omba radhi Kwa mauaji ya Lumumba

    Hatimaye Barack Obama, Rais wa Marekani anatembelea tena bara la Afrika. Hii itakuwa ni mara ya pili Obama kutembelea Bara hili alikotoka baba yake baada ya ziara yake ya kwanza mwaka 2009. Mwaka huo alitembelea Ghana na Misri ilhali mwaka huu anatembelea Senegali, Afrika Kusini na Tanzania. Ziara hiyo itakayoanza tarehe 26 mwezi Juni, itamfikisha Tanzania tarehe 1 Julai na kuondoka siku ya pili yake.

    Uchaguzi wa Obama kuwa Rais wa Marekani ulipokolewa kwa shangwe Afrika nzima. Wakati Waziri wa mambo ya nje wa Nigeria alilia kwa furaha, nchi ya Kenya ilitangaza siku ya mapumziko na Rais wa zamani wa Afrika Kusini ndugu Nelson ‘Madiba’ Mandela alisema ‘ushindi wa Obama unawafanya Waafrika wathubutu kuota ndoto (Jarida la The Economist). Hapa Tanzania kulikuwa kuna shamra shamra za kila namna na magazeti yaliweka vichwa vya habari kana kwamba ni Rais wa Tanzania aliyechaguliwa.

    Waafrika walikuwa na matumaini makubwa sana na bwana Obama. Yamefikiwa?
    Ni vema ifahamike kuwa Barack Obama ni Rais wa Marekani na siku zote atalinda maslahi ya Marekani tu. Kuwa na matumaini makubwa kwamba labda yeye angeliweza kuiweka Afrika mbele sana ilikuwa ni kujifurahisha tu nafsi. Maslahi ya Marekani ni ya kipaumbele kuliko kitu kingine chochote kwa Rais Obama. Kwa wengi Obama amekuwa kama amewavunja moyo.

WATANZANIA 60 WAKAMATWA ZIARA YA OBAMA....!!!

Watanzania 60 wamekamatwa Afrika Kusini kutokana na maandalizi yaliofanyika nchini humo ya kumpokea Rais Barack Obama wa Marekani.

Rais Obama amewasili Afrika Kusini juzi kwa ziara ya siku tatu akitokea Senegal.

Watu hao wamekamatwa baada ya kudaiwa kuishi kinyume cha sheria Afrika Kusini. Baada ya Watanzania hao kutiwa mbaroni na vyombo vya usalama wamehifadhiwa hapa nchini kusubiri  hatua za kisheria zaidi.

Ofisa mmoja wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, Sadiki Msele amesema Watanzania hao walirejeshwa nchini jana na kwamba hivi sasa wanasubiri sheria kuchukua mkondo wake.

“Safisha safisha kama iliofanyika jijini Dar es Salaam, pia imefanyika Afrika Kusini na kuwaathiri wafanyabiashara na watu wengine,” amesema ofisa huyo.

Hivi sasa Rais Obama yupo Afrika Kusini akiwa ameongoza na mkewe Michelle Obama na watoto wao wawili; Malia na Sasha.

Leo Rais Obama na ujumbe wake anatarajiwa kutua Tanzania kwa ziara ya siku mbili na Jumanne ataondoka kurejea Marekani.

ANGALIA MITAA MBALIMBALI YA BONGO ILIVYOPAMBWA KWA MAANDALIZI YA UJIO WA OBAMA

 
 
 
 
Barabara ya Baharini mchana wa leo, ikiwa shwari huku ikiwa imepambwa na mabango yenye picha za Rais wa Marekani, Barack Obama na Bendera za Nchi hiyo na Tanzania. KARIBU OBAMA
 
credit: sufiani mafoto

WAPENZI WADONDOKA NA KUFA WAKATI WAKIFANYA MAPENZI DIRISHANI...!!!

 
Wapenzi wameanguka na kufa baada ya dirisha walipokuwa wakifanyia mapenzi kufunguka ghafla nchini China.

Wawili hao wanasemekana kudondoka kutoka kwenye dirisha la jengo moja la makazi kwenye jiji la Wuhan nchini humo pale dirisha hilo walilokuwa wameegemea kufunguka.

Mashuhuda walivieleza vyombo vya habari vya China kwamba wapenzi hao walikumbatiana wakati wakianguka kwenye njia ya waenda kwa miguu nje.
Kwa mujibu wa The Sun, chanzo kimoja cha habari kilisema: "Huku wawili hao wakiwa wameshikamana vilivyo, walianguka nje ya jengo hilo."
Picha za kuogofya zimefichuliwa kwenye tovuti za nchini humo zikionesha wapenzi hao wakiwa wamefunikwa kwa mashuka na polisi.
Damu ilitapakaa kwenye njia ya waenda kwa miguu karibu na wapelelezi wanaonekana wakichunguza eneo la tukio.
Miili ya wapenzi hao ilipigwa picha karibu na baiskeli ambayo ilikuwa imelazwa chini, lakini hakukuwa na ripoti zozote kwamba yeyote chini alikuwa amejeruhiwa katika ajali hiyo.
Ripoti zinasema kwamba madirisha hayo kwenye jengo hilo la makazi yalikuwa hayana ubora unaotakiwa.
Inafikiriwa kwamba mwanaume huyo na mwanamke wanawezekana walikuwa wakijaribu kujipooza kando ya dirisha hilo ndipo tukio hilo likatokea.
Haikufahamika ni umbali gani kutoka juu wawili hao walikuwa wakati wakianguka.
Wuhan ni jiji maarufu zaidi lililopo katikati ya China.
Ukiwa na historia ya miaka 3,500 ni moja kati ya miji mikongwe na iliyostaarabika katika China.

HUYU NDIYE MWANAMKE ALIYEMKATA UUME MUMEWE AFUNGWA MAISHA GEREZANI...!!!

 

Mwanamke mmoja wa California ambaye alituhumiwa kukata uume wa mumewe kabla ya kuutupa kwenye mashine ya kusagia taka amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani.
Catherine Kieu, mwenye miaka 50, alipatikana na hatia ya mashitaka ya kutesa na kosa la kuharibu viungo vya mwili katika shambulio la Julai 11, 2011 na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela, lakini anaweza kufikiriwa kupewa msamaha baada ya kutumikia miaka saba.

Alitiwa hatiani Aprili kwa kila kosa moja la kutesa na kuharibu viungo vya mwili.
Muathirika, anayefahamika kama Glen wakati wote wa kesi, alikuwa mahakamani kwa ajili ya hukumu ya jana.
"Natumaini hii itakuwa mara ya mwisho kabisa ninayoweza kumwona," alisema Glen. "Najihisi nafuu kiasi fulani, na ilikuwa siku ya huzuni kubwa kwangu."
Muathirika huyo alikimbizwa hospitali, lakini upasuaji kurejesha uume wake haukufanikiwa.
Wakati wa kesi hiyo, muathirika huyo mwenye umri wa miaka 60 alitoa ushahidi kwamba uume wake hauwezi tena kuunganishwa mahali pake na kwamba anahisi kama ameuawa.
Kieu alikuwa na wivu na hasira kuhusu mipango ya  mumewe kumpa talaka sababu alimwona rafiki yake wa zamani wa kike, upande wa mashitaka ulisema.

Sunday, June 30, 2013

LOWASSA AMTAKA OBAMA ASIZUNGUMIE MAMBO YA USHOGA NA NDOA ZA JINSIA MOJA AKIWA TANZANIA



Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo yaNje na Ushirikiano wa Kimataifa, Edward Lowassa, amemtahadhalisha kujiepusha na kauli za kuunga mkono ushoga.
Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Alisema  jana kuwa ushoga na hai za ndoa kwa watu wa jinsia moja vinaweza `kuiharibu’ ziara yake hapa nchini.
Mapema wiki hii, Rais Obama alikaririwa akizungumzia masuala hayo yanayotajwa kuwa ni moja ya haki za msingi za binadamu, alipokuwa Senegal, lakini akapingwa.
“Watanzania hawatalikubali na wataendelea kushikilia uhuru na heshima walizojengewa tangu awali, kwamba ushoga na ndoa za jinsia moja havikubaliki,” alisema.
Akiwa Senegal, Rais Obama alitaka serikali za Afrika kutoa haki kwa mashoga kama inavyotoa kwa raia wengine.
"Ninachotegemea, I pray and hope (ninasali na kutegemea) kwamba kuhusu mashoga na ndoa za jinsia moja, Rais Obama hatarudia kauli aliyoitoa kule Senegal,” alisema.
Aliongeza, "ninasema hivi kwa sababu Tanzania hatuamini katika ushoga, na endapo utawalazimisha Watanzania, watakukatalia na kushikilia uhuru na heshima waliyojengewa toka awali."


JK AMGEUKA MWENYEKITI WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA JAJI JOSEPH WARIOBA

RAIS Jakaya Kikwete amemgeuka Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, kwa kuridhia azimio la Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutaka uwepo muundo wa serikali mbili.
Rais Kikwete ambaye juzi aliongoza kikao cha Kamati Kuu (CC), mjini Dodoma, aliridhia azimio hilo, huku akijua fika kuwa ndiye aliyemruhusu Jaji Warioba kuingiza kipengele hicho kwenye rasimu wakati alipoifikisha mbele yake kabla ya kuitoa hadharani.
Kutoka na hali hiyo, Kamati Kuu imewataka wanachama wao wote kupitia mabaraza ya CCM kuhakikisha wanakubaliana na msimamo wa chama wa kupinga muundo wa serikali tatu kama ilivyopendekezwa na tume ya Jaji Warioba.
Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho kutoka Zanzibar, waliliambia Tanzania Daima Jumapili kuwa Kamati Kuu
imepitisha azimio la kutaka mabaraza ya Katiba ya chama hicho yajadili na kuridhia msimamo wa kuwa na serikali mbili.
Kamati Kuu ya CCM imekuja na mapendekezo ya namna ya kurekebisha kasoro kubwa za Muungano ambazo kwa muda mrefu zimekuwa zikilalamikiwa na Wazanzibari.

BEYONCE ATINGA VAZI LA KANGA, ILIYOTENGENEZWA NA MTANZANIA



clip_image001[6] 
Christina (katikati)
Utajiskiaje kuona Beyonce akiwa amevaa vazi lililotengenezwa kwa kanga yenye maneno ya Kiswahili? ‘Wawili Ninyi Yawahusu….’ yanasomekana maandishi kwenye vazi alilolivaa mwanamuziki wa Marekani, 

 clip_image001
  Beyonce Knowles.
Vazi hili alilolivaa Beyonce kwenye moja ya show zake za tour ya Mrs Carter, limetengenezwa na mwanamitindo wa Tanzania aishie jijini London Uingereza, Christine Mhando mwenye brand ya Chichia London. Chichia London ndio brand iliyo maarufu sana nchini Uingereza kwa kutengeneza nguo za Kitanzania kwa kutumia Kanga na material mengine Kiafrika.
Hizi ni baadhi ya nguo alizotengeneza.
clip_image001[8]

LOWASSA AWATEKA WAENDESHA BODABODA ARUSHA...!!!

Wafanyabiashara maarufu jijini Arusha wakiongozwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Diwani wa Mererani, Mathias Manga, ndiyo waliyobuni wazo hilo la kuwaanzishia mfuko vijana wa bodaboda.
Katika harambee hiyo, sh milioni 84 zilipatikana huku Lowassa pamoja na marafiki zake wakichangia sh milioni 10 na pikipiki 1WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, amesema usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda ni sera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya kusaidia kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana.
Akizungumza katika haraambee na uzinduzi wa mfuko wa waendesha pikipiki maarufu mkoani Arusha, Lowassa alisema sera hiyo ni ya kuwakomboa vijana.

Alisema kuwa kitendo cha wafanyabishara wa Arusha kujipanga kusaidia bodaboda ni mfano kwa wafanyabishara wengine nchini.

“CCM ni chama kinachotetea wanyonge, na nyinyi ni wanyonge mnaohitaji kunyanyuliwa kimaisha, kitendo hiki cha wafanyabisharaa wa Arusha ni cha kuunga mkono sera ya CCM,” alisema.

Lowassa alisema tatizo la ajira ni bomu linalosubiri kulipuka na kwamba wasipowasaidia vijana kuondokana na tatizo hilo amani itatoweka.

“Ndiyo maana CCM katika ilani yake ya uchaguzi imeliweka hilo na pia kulisisitiza katika vikao vyake vya juu vya Mkutano Mkuu pamoja na Halmashauri Kuu,” alisema.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...