Maandalizi
ya ujio wa Rais wa Marekani, Barack Obama nchini yanazidi kupamba moto
huku maofisa wa usalama wa Marekani wakipiga kambi katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam.
Aidha,
kutokana na ujio huo, Serikali imeagiza mashirika yote ya ndege
kubadili ratiba zao za safari Julai Mosi, siku ambayo Rais huo atatua
nchini. Jana,
waandishi wetu walishuhudia pilikapilika za kuimarisha ulinzi katika
uwanja huo jambo ambalo uongozi wa uwanja huo jambo wamelieleza kwamba
halijawahi kutokea.
Ulinzi haujawahi kutokea Mkurugenzi
wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Moses Malaki alisema
jana kwamba ratiba za uwanjani hapo zitabadilika kutokana na uzito wa
ugeni huo.Alisema
kwa kawaida anapokuja kiongozi mkubwa wa kitaifa katika uwanja huo
hakuna ndege inayoruhusiwa kutua kwa kipindi cha nusu saa. “Ni
kweli hali hiyo pia itakuwapo atakapokuja Rais Obama na safari za ndege
zitabadilika kulingana na ratiba ya kutua na kuondoka kwa Rais huyo,”
alisema Malaki.Pia
alisema ulinzi katika uwanja huo umeimarishwa kwa mwezi mmoja sasa na
tangu wakati huo, maofisa wa usalama wa Marekani wamekuwa wakifika kwa
nyakati mbalimbali. “Sijawahi
kuona ulinzi mkali kama huu, wamekuja marais wengi hapa nchini lakini
ulinzi huu ni wa kutisha, sijui kwa sababu gani?” alisema Malaki.Alisema
awali, wakati maofisa hao walipoanza kuwasili nchini hawakutambua ni
mgeni gani anayetarajia kufika lakini baadaye walipelekewa taarifa kuwa
ni Rais Obama na baadaye walitaarifiwa kuwa angetua saa 8.40 mchana,
Julai Mosi.Mkurugenzi
huyo alisema Rais Obama atakuja na ndege nne, moja itakayombeba, ya
pili kwa ajili ya mizigo, ya tatu itakuwa ya waandishi wa habari na
maofisa wa usalama na ya mwisho ni kwa ajili ya dharura ambayo
itaegeshwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).