Tuesday, June 25, 2013
VIONGOZI WATANO WA CHADEMA WASHITAKIWA KWA UGAIDI .... MAJINA YA VIONGOZI HAO HAYA HAPA
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Dar es Salaam na vijana wengine leo wameshtakiwa kwa Ugaidi katika mahakama ya Hakimu mkazi Tabora mjini.
Mbali
ya Kileo, vijana wengine wa Chadema, ni Evodius Justinian wa Buboka,
Oscar Kaijage wa Shinyanga, Seif Magesa Kabuta wa Mwanza, Rajab Daniel
Kihawa wa Dodoma, leo wamesomewa shitaka la Ugaidi kwa kumteka na
kumwagia tindikali Musa Tesha katika kampeni za Uchaguzi mdogo wa
Igunga uliofanyika mwaka 2011.
Watuhumiwa hao walisomewa mashtaka mawili wote, la kwanza ni la kufanya ugaidi, na la pilini kumwagia tindikali Musa Tesha.
Kesi
hiyo ilikuwa ilisikilizwa mbele ya hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi,
ya Tabora Mjini,Joktani Rushwera, huku upande wa serikali
ukiwakilishwa na Wakili Juma Massanja na Ildefons Mukandara Baada
ya kusomewa shitaka hilo, Upande wa utetezi wa ukiongozwa na wakili
Prof Abdalah Safari, ukiwajumlisha Peter Kibatala na Gasper Mwalyela
ulitoa hoja kuiomba mahakama hiyo ifutilie mbali mashtaka hayo kwa
sababu, kwanza mashtaka hayakuwa na uhai kwa kuwa yamefunguliwa bila ridhaa ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini.
WABUNGE NA MASHOGA WATETA..... HOFU YA KUWA NA RAIS SHOGA TANZANIA YATANDA....!!!
WABUNGE wanachama wa Chama cha Kupambana na Ukimwi (TAPAC), wiki iliyopita walikutana na kujadiliana mambo mbalimbali na mashoga katika mkutano wa mwaka wa chama hicho uliofanyika kwa muda wa siku tatu mjini Dodoma. Katika mkutano huo, baadhi ya wabunge walionyesha wasiwasi wa taifa kupata rais shoga katika miaka ijayo kutokana na ongezeko la mashoga hapa nchini.
Mbali na wasiwasi ulioonyeshwa na wabunge, mashoga waliokuwa wakihudhuria mkutano huo, walilalamikia vitendo vya unyanyasaji wanavyofanyiwa na wanajamii wenzao na kudai watambulike na wapatiwe huduma za msingi za kibinadamu.
Akizungumza katika mkutano huo uliomalizika jana, Mbunge wa Nkasi, Ally Kessy (CCM), alitahadharisha uwezekano wa nchi kupata rais shoga katika miaka ijayo, iwapo hatua za makusudi za kudhibiti hali hiyo hazitachukuliwa.
“Tabia ya kuwapeleka watoto kwenye shule za mabweni wangali wadogo wa umri wa miaka hadi miwili, itatuletea matatizo baadaye.
“Katika shule nyingi za bweni vitendo vichafu vinafanyika, vikiwamo vya ushoga. Katika vyuo vikuu hivi sasa kuna mashoga wasiopungua 40,000. Hii ni hatari, tusipojihadhari tutakuwa na rais shoga katika miaka ijayo,” alisema Kessy huku akishangiliwa na wabunge.
Mbunge huyo alitaka elimu dhidi ya ushoga na athari zake ienezwe nchini kupitia vyombo vya habari na nyumba za ibada.
MWANAMKE AOLEWA NA WANAUME WAWILI NA KUISHI NAO...!!!
MWANAMKE
mkazi wa kijiji cha Ikandamoyo, wilayani Katavi, Veronica Saleh ‘Mama
Kaela’ (50), amefanya uamuzi adimu wa kuolewa na wanaume wawili ambao
anaishi nao kijijini hapo.
Kijiji
hicho kipo umbali wa takribani kilometa 30 kutoka mjini hapa katika
Jimbo la Katavi linalowakilishwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Pamoja
na ndoa hiyo iliyowezeshwa na mume mkubwa kukubali kuishi na mume
mdogo, imeelezwa kuwa mwanamke huyo ndiye ‘aliyewaoa’ wanaume hao kwa
zaidi ya miaka saba sasa, huku akiwa na amri kuu katika nyumba, kama
ilivyo katika ndoa za kawaida.
Wanaume hao ni Paulo Sabuni ‘Baba Kaela’ (60) ambaye ndiye mume mkubwa na Arcado Mlele (45) ambaye ni mume mdogo.
Taarifa
za kuwapo kwa ndoa hiyo ya aina yake, ziliifikia Globu ya Jamii na
kufanyiwa uchunguzi kwa zaidi ya wiki tatu, na hatimaye katikati ya wiki
hii, wahusika walikubali wao wenyewe kuzungumzia suala hilo. Kwa mujibu
wa maelezo ya mwanamke huyo ambaye alionekana kuwa msemaji wa familia
hiyo, yeye na mumewe mkubwa, walifika kijijini hapo miaka 24 iliyopita,
wakitoka kijiji cha Usumbwa mpakani mwa Chunya, Mbeya na Tabora.
Monday, June 24, 2013
MSHTAKIWA WA EPA ASIMULIA JINSI WAJANJA WALIVYOMZIDI ‘KETE’ KWENYE AKAUNTI YAKE
Godfrey Mosha |
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Principal Ltd, Godfrey Mosha amesimulia jinsi Benki ya
Akiba Commercial (DCB), tawi la Kariakoo, ilivyoidhinisha malipo ya
fedha kwa mtu mwingine kutoka akaunti yake ndani bila yeye kujua.
Mosha
ni mmoja wa washtakiwa katika kesi ya wizi wa fedha kwenye Akaunti ya
Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Pamoja na
wenzake, Bahati Mahenge, Manase Makale, Davis Kamungu na Eda Makale,
wanakabiliwa na kesi ya wizi wa Sh1.86 bilioni za EPA, katika Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuipitia Kampuni ya Changanyikeni Residential
Complex.
Katika
kesi hiyo dhidi ya DCB, inayosikilizwa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu, Warialwande Lema, Mosha anaidai benki hiyo Sh46.8
milioni, zilizolipwa kwa mtu asiyemfahamu kwa kutumia hundi nne tofauti
na tarehe tofautitofauti.
Katika
ushahidi wake Ijumaa iliyopita, akiongozwa na Wakili wake, Michael
Ngalo, Mosha alidai alibaini uhamisho huo wa fedha kutoka akaunti
yake namba 0400438671, Novemba 15, 2011 alipochukua taarifa ya benki.
SOGGY DOGGY NAE ATANGAZA KUGOMBEA UBUNGE 2015
Nguli wa muziki wa kizazi kipya Soggy Doggy Anter aka Anselm Tryphone
Ngaiza leo ametangaza nia ya kugombea Ubunge wa jimbo la Segerea, Dar es
Salaam kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA,
MWAKA 2015.
Msanii huyo ametiririka katika ukurasa wake wa facebook, na hapa nanukuu
"Shikamoo Mbunge wa Segerea, Makongoro Mahanga, imetosha sasa nadhani
ni zamu yangu kuwatumikia wana-segerea 2015 kupitia CHADEMA" mwisho wa
kunukuu. Pia kwenye ukurasa wake wa twitter imesomeka ivyo ivyo.
Nilipoongea na Msanii huyu aliniambia ameamua kufanya ivi ili kuwasaidia
na kuwaletea maendeleo wana-segerea na watanzania kiujumla.
Pia aliniambia ameamua kugombea kupitia CHADEMA, kwasababu ndo chama kinachoweza kufanya mabadiliko kwenye jamii kwasasa.
Nikamuuliza je amemfuata rafiki yake Joseph Mbilinyi aka "SUGU" katika
chama icho, akasema hapana, hawajawahi kupewa ushawishi wowote wa
kisiasa na Nguli huyo wa muziki wa Hip Hop.
Wana-Segerea kazi kwenu kijana ameamua na amedhamiria.
SIKU 17 KABURINI... FAMILIA YASHANGAA RIPOTI KIFO CHA NGWEA.
ZIKIWA
zimekatika siku 17 tangu aliyekuwa mkali wa Hip Hipo Bongo, Albert
Kenneth Mangweha ‘Ngwea’ alale kaburini, familia imeshangaa kupelekewa
vitu vingine bila ripoti ya kifo chake.
Kwa
mujibu wa mtu wa ndani wa familia hiyo, Millard Ayo wa Clouds FM ndiye
aliyepewa majukumu ya kushughulikia kila kitu baada ya kifo tata cha
Ngwea kilichotokea Johannesburg, Afrika Kusini Mei 28, mwaka huu.
Chanzo
hicho kilieleza kuwa mara baada ya mwili wa marehemu Ngwea kuletwa
Bongo, familia ilitarajia kukabidhiwa kila kitu ikiwemo ripoti ya nini
kilimuua Ngwea.
“Hakuna
swali tunaloulizwa kama ripoti ya kifo cha Albert (Ngwea). Kila mtu
anataka kujua nini hasa kilitokea hadi akafa kwa sababu maneno ni mengi
sana.
“Ripoti ndiyo ingeweza kumaliza maneno na kuwafunga watu midomo,” kilisema chanzo chetu mjini hapa.
“Ripoti ndiyo ingeweza kumaliza maneno na kuwafunga watu midomo,” kilisema chanzo chetu mjini hapa.
Kiliendelea
kunyetisha kuwa mwili ulipofika ilibidi familia ‘idili’ na maziko
kwanza ambapo Millard aliahidi kuipeleka baada ya msiba.
“Kweli
Millard alikuja tena juzikati, alichokabidhi ni cheti cha kifo (death
certificate) na hati ya kusafiria ya marehemu Ngwea,” kilisema chanzo
chetu na kuongeza:
“Familia nzima ilishangaa kwani ilikuwa ni tofauti na tulichotarajia lakini tulipomuuliza kuhusu ripoti ya kifo cha Ngwea, alikabidhi barua iliyoelezea kuwa chanzo cha kifo bado kinachunguzwa huko Afrika Kusini ambapo wanafanya critical investigation (uchunguzi wa kina) na tutajulishwa mara tu uchunguzi huo utakapokamilika.”
“Familia nzima ilishangaa kwani ilikuwa ni tofauti na tulichotarajia lakini tulipomuuliza kuhusu ripoti ya kifo cha Ngwea, alikabidhi barua iliyoelezea kuwa chanzo cha kifo bado kinachunguzwa huko Afrika Kusini ambapo wanafanya critical investigation (uchunguzi wa kina) na tutajulishwa mara tu uchunguzi huo utakapokamilika.”
Baada
ya kudakishwa habari hizo, Ijumaa Wikienda lilizungumza na mama wa
marehemu Ngwea, Denisia Mangweha ambaye alikiri kupokea vitu hivyo na
kwamba ni kweli familia ilijiandaa kupokea ripoti ya kifo lakini
haikuwa hivyo.
Credit: GLP
SUMAYE AMPONDA LOWASSA KANISANI...!!!
WAZIRI
Mkuu mstaafu Frederick Sumaye amesema anashangazwa na baadhi ya
viongozi wa dini kutoa sifa nzuri kwa watu wanaochanga fedha na si
kuzingatia uadilifu na wema walionao.
Kiongozi huyo alitoa kauli hiyo jana katika sherehe za kutimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), zilizofanyika katika Chuo Kikuu cha Makumira mkoani Arusha.
Sumaye
alihoji kuwa inakuwaje wema wa baadhi ya watu unajitokeza zaidi
wakati nchi ikielekea kwenye uchaguzi unaotegemewa kufanyika mwaka
2015.
Sherehe
hizo za kutimiza miaka 50 zilifanyika katika Chuo Kikuu cha Makumira
na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa KKKT kutoka sehemu mbalimbali
duniani pamoja na maaskofu wote wa dayosisi 20 zilizopo nchini.
MH. SUGU AMUOMBA RADHI WAZIRI MKUU
Mhe Sugu |
Waziri Mkuu, Mhe. Pinda |
BAADA
ya kauli yake iliyoibua mjadala mkubwa nchini dhidi ya Waziri Mkuu,
Mhe. Mizengo Pinda kufuatia majibu yake aliyoyatoa wiki iliyopita
Bungeni kwa kutaka Polisi kuendelea kuwapiga raia, Mbunge wa Mbeya
Mjini, Mhe Joseph Mbilinyi 'Sugu', aomba radhi.
Sugu
amemuomba radhi mhe Pinda na watanzania kwa ujumla kwa lugha aliyotumia
katika kuonyesha hisia zake juu ya kauli aliyoitoa mhe Pinda bungeni.
Kupitia
akaunti yake ya Facebook, Mbunge huyo machachari amenukuliwa akiwaomba
radhi Watanzania waliokerwa na kauli yake iliyodai kwamba Tanzania
haijawahi kuwapata Waziri Mkuu kama Mhe. Pinda kwa kusema;
"Ndugu
watanzania, naombeni radhi kwa tusi nililolitoa kwa mhe Pinda, kwani
nilikua nimeghafirika, halikuwa kusudio langu kumtukana mmoja wa
viongozi wa nchi."
ANGALIA PICHA ZA MAZISHI YA MAMA MZAZI WA BARNABA (BI MARIAMUARUBETH)
Mama Diamond |
Siku ya leo jumapili ndio ilikuwa siku husika kabisa katika kutoa heshima za mwisho kwa Bi Mariamu
Arubeth aliezaliwa 4/12/1967 na kufariki tarehe 22/6/2013.
Zifuatazo ni picha za Mazishi Ya Mama mzazi wa Barnaba kuanzia nyumbani hadi makaburini....
Sunday, June 23, 2013
The Finest : FA apata wakati mgumu kwa kulazimishwa na mashabiki kutaja jina la Lady Jay Dee.
by IRENE MWAMFUPE
Mwanamuziki
Hamis Mwinjuma, maarufu Mwana FA, amepata wakati mgumu kwa
kulazimishwa na mashabiki kutaja jina la Lady Jay Dee, baada ya
kuliruka jina hilo alipokuwa akiimba wimbo wa Mabinti ambao ndani yake
kuna jina la Jay Dee.
Mwana FA alisita kwa muda na baadaye aliamua kurudia wimbo huo na alipofika katika kipengele cha kumtaja Jide aliimba kwa kumtaja, hali iliyoufanya ukumbi huo ulipuke kwa shangwe na mashabiki kumtaka arudie tena na tena.
Kutokana na hilo FA aliamua kufunguka; “Tunaishi na watu hivyo lazima mtagongana, hata mapacha wanakosana na kusameheana, lakini wakati mwingine shida inawafanya mnapatana,” alisema Mwana FA.
Awali
shoo ilitangazwa kuwa ingekuwa ya watu 400 tu. Lakini mpaka inafika
saa nne kasoro usiku, muda uliotangazwa kuanzwa kwa shoo hiyo watu
waliokuwa wamefika walikuwa kama 250 tu.
Saa
nne kamili mwanamuziki Hamis Mwinjuma, Mwana FA alikanyaga ‘red
carpet’ akiwa na mbunifu wa mavazi Sheria Ngowi, na baada ya
kuchukuliwa picha kadhaa alianza kuelekea nje ya ukumbi sehemu
waliyosimama watu wakipata chakula na vinywaji, watu walizidi kufurika
lakini kila aliyeingia alikuwa alwatan kidogo.
Waliendelea kuwasili mastaa na shoo inaanza Mashabiki wanaanza kuingia ukumbini saa tano kamili baada ya kupata vyakula na vinywaji nje, huku muziki wa taratibu ukipigwa na bendi ya muziki wa dansi ya Njenje. Mashabiki wanaendelea kubadilishana mawazo mpaka inapotimu saa tano na robo usiku, ambapo Mwana FA anapanda jukwaani.
Anaanza kazi kwa shoo ya aina yake baada ya kuimba hip hop live akiwa na bendi ya muziki wa dansi, kwenye shoo hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
FA
alipanda jukwaani na wimbo wa Binamu akisindikizwa na wanamuziki
Mandojo na Domokaya waliovalia suruali nyeusi na mashati meupe huku
wakiwa wamevalia mikanda aina ya ‘suspender’, baadaye aliimba wimbo
Unanijua Unaniskia na Bado Niponipo Kwanza ambao uliwapendeza
mashabiki.
Alisimamisha shoo kwa muda na msanii Bernald Paul maarufu kama Benpol alipanda jukwaani na kuimba nyimbo zake tatu kwa kuziunganisha ukiwamo wa Maneno, Pete na Nikikupata na baadaye aliimba na Mwana FA wimbo wa Asubuhi aliomshirikisha Q Chief.
FA alipanda jukwaani na wanamuziki kadhaa katika vipindi tofauti akiwamo Linah Sanga ‘Linah’, Maua, Abdul Sykes ‘Dully Sykes’.
Baadhi
ya nyimbo alizoimba ni pamoja na Kama Zamani, Alikufa kwa Ngoma,
Habari Ndio Hiyo, Leo, Mabinti, Unanitega, Yalaiti na nyingine nyingi.
HII NDIO HALI YA MSANII BARNABAS TANGU KUPOKEA TAARIFA ZA MSIBA WA MAMA YAKE
Kiukweli inasikitisha sana tangu asubuhi hajatia kitu chochote tumboni analia ananyamaza,akipewa chakula hakitaki.mungu mjalie ndugu yetu mpe nguvu aweze kumzika mama yake kwa aman na upendo.
R.i.P mamaa BARNABAS, Maziko ni leo saa 10 katika makaburi ya mburahati,kuanzia asubuhi saa 5 tutakuwa na misa maalum kwa ajili ya marehemu mama barnabas.
Subscribe to:
Posts (Atom)