IGP SAIDI MWEMA.
KATIBU MKUU MPYA WA CCM ABDULRAHMAN KINANA.
MLIPUKO wa bomu uliotokea wiki iliyopita katika mkutano wa kufunga kampeni za udiwani kwa CHADEMA mkoani Arusha na kuua watu wanne, umeiweka kwenye wakati mgumu serikali ya CCM, Jeshi la Polisi na Bunge.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema juzi bomu lililolipuliwa katika mkutano wa CHADEMA ni la kijeshi na limetengenezwa China na uzoefu unaonesha hutumiwa na wanajeshi kujihami wakiwa katika makabiliano na maadui vitani.
Wakati Pinda akitoa kauli hiyo bungeni, viongozi wa CHADEMA wamelihusisha Jeshi la Polisi na tukio hilo huku wakidai wanao ushahidi unaon
esha askari aliyevalia sare akilirusha kwenye mkutano huo.
Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kijamii, wamelidokeza Tanzania Daima kuwa kukiri kwa serikali kuwa bomu hilo limetengenezwa China, inapaswa iibane nchi hiyo ieleze iliyemuuzia na alivyoliingiza nchini.
“Kwanini isiundwe tume huru nchini ili nchi ya China iulizwe baada ya kutengeneza bomu hilo ilimuuzia nani? Na kama haikuiuzia serikali, basi ni dhahiri tuiulize China kwanini inafadhili vikundi vya kigaidi nchini kwetu ?.