Jeshi
la polisi mkoani Arusha linawashikilia viongozi wanne wa CHADEMA na
watu wengine huku likiendelea kuwatafuta wabunge wawili na watu wengine.
Jeshi
la Polisi limesema limewatua nguvuni watu hao kwa makosa ya kuhutubia
mkutano haramu wakati wa kuwaaga marehemu waliopoteza maisha kwenye
mlipuko wa bomu uliotokea katika eneo la Soweto jijini humo mwishoni mwa
wiki. Makosa mengine ni wanayotuhumiwa kwayo ni kufunga barabara na kuwashambulia askari polisi.
Amesema wataendelea kubaki korokoroni hadi uchunguzi utakapokamilika.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas amewataja Wabunge wanaoshikiliwa ni pamoja na Tundu Lissu na Mustapha Akunai.
Wanaotafutwa
ni pamoja na Mwenyekiti CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe na Mbunge wa
Arusha Mjini, Godbless Lema ambao waliponyoka mikono ya polisi.