Sunday, June 16, 2013

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JUNI 16, 2013

.
.

HABARI YA KINA KUHUSU MLIPUKO WA BOMU ARUSHA


Mkutano wa Chadema wa kumaliza kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani mjini Arusha, jana ulivunjika baada ya bomu kulipuka na kuua watu wanne na wengine kujeruhiwa.Bomu hilo lililipuka jana saa 11:50 dakika chache kabla ya Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe kumaliza kuhutubia mkutano huo uliofanyika katika Viwanja vya Soweto mjini Arusha na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi.Hilo ni tukio la pili la bomu kulipuka katika mkusanyiko wa watu, Mei 5 mwaka huu bomu lililipuka katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasit mjini Arusha na kuua watu watatu na wengine kujeruhiwa.


Mama akikimbizwa hospitali kupata matibabu.

 Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mount Meru Frida Mokiti alisema katika hospitali yake kuna maiti moja ya mtoto na majeruhi 11.Habari zingine zilisema katika hospitali ya Misheni ya Selian kuna maiti za watu wawili, waliokufa kutokana na shambulio hilo na majeruhi ambao idadi yao haijafahamika.Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema katika tukio hilo watu wawili wamepoteza maisha, mwanamke na mwanamume na kwamba idadi ya majeruhi bado haijafahamika kwa kuwa wametawanywa katika hospitali mbalimbali mkoani humo.

HILI NDILO CHIMBUKO LA JINA LA ANACONDA ANALOTUMIA JAYDEE

 Huyu naye alikuwepo ili kuonyesha uhalisia wa jina la Anaconda ambalo sasa anatumia msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya nchini Jay Dee, ambapo jina hilo limetokana na vuguvugu ambalo linaendelea hivi sasa ambalo hilo vuguvugu ndilo limechangia shoo ya mwanamuziki huyo kujaa huku mashabiki wakionyesha hali ya kumshinda mtu anyemkandamiza msanii huyo

CHADEMA YAKANA TUHUMA ZA KUUA WATU.

Singo Kigaila.

Huku kukiwa na madai kuwa Chadema inahusika na matukio ya kula njama za utekaji na kuteka, kupiga na kuua watu, chama hicho kimekuja juu na kukanusha madai hayo.

Pamoja na kukanusha, kimemwomba Rais Jakaya Kikwete aunde tume huru ya kimahakama kuchunguza matukio yaliyotokea ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wote watakaobainika kuhusika.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganaizesheni wa chama hicho, Singo Kigaila, alisema walishamwomba Rais aunde Tume lakini akadai ombi hilo halijatekelezwa hadi sasa.

Saturday, June 15, 2013

HAWA NI MAJERUHI WA MLIPUKO WA BOMU MKUTANI WA CHADEMA WAKIPATIWA HUDUMA YA KWANZA KATIKA HOSPITAL YA MOUNT MERU

MADAKTARI NA WAUGUZI WAKITOA HUDUMA YA KWANZA KWA WATU WANAODAIWA KUATHIRIKA KATIKA MLUPUKO WA KITU KIN
ACHODHANIWA KUWA NI BOMU BAADA YA KUJERUHIWA WAKATI WAKIWA KATIKA MKUTANO WA CHADEMA JIJINI ARUSHA ENEO LA SOWETO.
Majeruhi. Mungu urehemu tz

JOH MAKINI ALAZWA SINZA PALESTINA, HII NDIO MESEJI YAKE

Moja ya rapper memba wa kikundi cha hip hop TZ, Joh Makini, yuko hospitali huku akiomba tumuombee na kusema yuko katika hali ya kawaida na si mbaya sana.
 

POLISI WAMTIA MBARONI MAMA ALIYEMTUPA MTOTO BAADA YA BABA WA MTOTO KUMKANA KISA ANA NYWELE ZA KIARABU



Binti mmoja aliyefahamika kwa jina la Khadija Idd anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Morogoro akidaiwa kumtupa barabarani mtoto wake mwenye umri wa miezi 6 baada ya mwanaume aliyezaa naye kumkataa.

Shuhuda wetu ambaye ni dereva wa bodaboda aliyefahamika kwa jina la Shabani, alisema tukio hilo lilitokea Juni 11, mwaka huu maeneo ya Mafiga karibu na Msikiti wa Mahita ambapo Khadija alichukua uamuzi huo baada ya mwanaume aliyezaa naye kumgomea mtoto kwa madai ana nywele za Kiarabu hivyo si wake.


“Huyu dada alifika kwenye kijiwe chetu akiwa amembeba mtoto mgongoni na kukodi pikipiki ili nimpeleke mjini.

“Tulipofika kwenye msitu uliopo karibu na mashamba ya SUA, aliniambia niendeshe spidi kuna mtu anamuwahi.

Nilitii amri lakini tulipofika mbele kidogo nikashangaa anamtupa yule mtoto.

RAIS OBAMA AHAIRISHA ZIARA YAKE YA KUZITEMBELEA NCHI ZA AFRICA IKIWEMO TANZANIA...!!!


WAKATI Serikali ya Tanzania ikiendelea na maandalizi ya kupokea msafara wa watu 700 waliotarajia kuingia nchini kwa ziara ya Rais wa Marekani Barack Obama, Rais huyo amesitisha safari yake.
 
Ikulu ya Marekani imetangaza kwamba msafara wa Rais Obama kuja kutembelea Bara la Afrika haitakuwepo tena,baada ya serikali ya nchi hiyo kukosa fedha itakayoweza kugaramia safari ya Rais huyo.

Taarifa iliyonaswa na kutoka katika mitandao mbalimnali  nchini Uingereza na Marekani  zinaeleza kwamba mbali na suala la bajeti ya Rais huyo kuja nchini Tanzania kuwa kubwa pia kamati ya sheria ,ulinzi na usalama wa Marekani imeshindwa kuthibitisha juu ya suala la ulinzi na Usalama wa Rais Obama katika kipindi chote atakachokuwa nchini Tanzania pamoja na baadhi ya nchi Barani Afrika.
 
Taarifa hiyo pia ilieleza kwamba msafara wa Rais Obama unahitaji maandalizi ya kutosha kwa sababu ni msafara unaohusisha watu wengi pamoja na vyombo mbalimbali vya ulinzi ikiwemo wanyama.
 
Msemaji wa Ikulu ya Marekani alisema kwamba serikali ilijaribu kuangalia uwezekano wa Rais Obama kuja Tanzania na baadaye kutembelea Senegel pamoja na Afrika Kusini ambapo alitakiwa kukaa Tanzania kwa saa mbili tu lakini gharama za ulinzi imekuwa kubwa sana.
Katika msafara wa Obama inatakiwa kuwe na ndege mbili za mwendo kasi, kwa ajili ya kulinda ndege ya Rais,iwepo ndege za askari wa majini zinazotembea kwenye meli habarini, iwepo pea maalum za magari zitakazo sushwa katika nchi zote tatu mapema kwa kutumia ndege za jeshi kwa ajili kuimarisha ulinzi kabla ya Rais kutua katika nchi hizo" alisema Mseaji wa Ikulu ya marekani Josh Earnest.

Nakala ya taarifa hiyo  pia ilimkariri msemaji huyo wa Ikulu ya Marekani akisema kwamba pia katika msafari huo ni lazima iwe na vifaa maalum vya kutolea matibabu katika kipindi chote cha ziara ya Rais, lazima pia iwe na chombo maalum kwa ajili ya waandishi mbalimbali wa habari pamoja na vyombo vingine vya usalama kwa ajili ya kutoa taarifa ya safari ya Rais ,pamoja ndege zitakazokuwa zikizunguka kuangalia hali ya usalama katika hoteli zote atakapo kuwa ana alala Rais Obama na msafara wake.
 
Taarifa hiyo ilifafanua kwamba safari hiyo ndiyo safari kubwa kuliko aliyowahi kuifanya Barani Afrika ambapo alifika nchini Ghana, tangu alipochaguliwa kuwa Rais wa Marekani mwaka 2009 ambapo inakadiriwa kuwa itachukua kati ya dola za marekani 60 million sawa na tsh bilioni 96,000,000,000 na dola 100 milion sawa tsh bilioni 160,000,000,000.

LOWASSA ATANGAZA NDOTO YAKE, ISOME HAPA

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akiwapungia mkono walimu walioshiriki katika hafla ya harambee ya kuchangia Saccos ya walimu iliyofanyika kwenye Viwanja vya Chuo cha Ushirika Moshi, jana. Picha na Dionis Nyato. 
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema kuwa ana ndoto kwamba siku moja sekta ya elimu itapewa kipaumbele cha kwanza nchini na kuzikomboa rasilimali za taifa la Tanzania zinazowanufaisha wageni na kuacha wananchi wakiambulia faida kidogo.Huku akimtaja Dk Martin Luther King aliyekuwa mwanaharakati wa haki za Wamarekani weusi aliyefariki kabla ya kuuona utimilifu wa ndoto yake, Lowassa alisema kuwa anamwomba Mungu asimwondoe duniani ili aweze kushiriki kuifanya ndoto hiyo kuwa kweli itakayokamilika siku si nyingi ambapo viongozi watakubali kuwa elimu bora ndiyo itakayowasaidia Watanzania kuchimba madini yao na kuyauza kwa faida duniani. 
Akizungumza wakati wa kuchangia SACCOS ya walimu ya Moshi Vijijini, Ushirika wa Stadium jana, Lowassa alisema kuwa katika ndoto yake anawaona viongozi wakikubali kwamba elimu bora ndiyo italisaidia taifa kuumiliki utalii na kunufaika nao, badala ya kuwaachia wageni wanufaike nao, huku Watanzania tukiambulia makombo.Wakati Lowassa akieleza ndoto yake hiyo, Mwenyekiti wa TLP na mbunge wa Vunjo Augustine Mrema amesema: “Biashara ya urais imenishinda namwachia Lowassa kwani mimi nimeamua kurudi kwenye biashara ya rejareja.”

MSANII WA VICHEKESHO MASELE APATA AJALI YA GARI...!!!

 


Habari za uhakika ni kuwa muigizaji wa vichekesho hapa nchini maarufukwa jina la ''Masele cha Pombe'' ni mzima wa afya na hajafariki kamabaadhi ya tetesi zilivyoanza
kuenea kwa kasi.tetesi kuwaMasele amepata ajali ya gari
maeneo ya barabara ya 14 jijini Tanga, Wasanii wenzake walipatwa na mshtuko mkubwa, ilibidi kundi zima la VITUKO SHOW litie tim Eneo la tukio na kumkuta masele mzima wa afya,Ukweli ni kwamba masele 
alimgonga mtu baada ya kumgonga mtu
alisogeza gari mbele ili apaki aongee na raia mara gafla mawe yakaanza kurushwa na watu asiowatambua! kwa kuokoa uhai

wake akawasha gari na kuwatoka raia wenye hasira kali mara akajikuta amemgonga mtu mwingine ambaye kwa bahati nzuri hakuumia, pale ndipo raia walivamia gari la masele na kulipiga mawe wakapora simu hela na baadi ya vitu vilivyokuwemo kwenye gari ilifikia hatua mtu mmoja asiejulikana alichoma kisu tairi la gari la masele na kulitoboa toboa!
 wengine walipiga mawe kioo pamoja na taa za nyuma, na kutaka
kumuua. Jeshi la police lilitia tim eneo la tukio na kumchukua masele mpaka kituo cha police Mabawa, Mpaka sasa masele yuko poa.

MREMA AKABIDHI URAIS KWA LOWASSA MWAKA 2015...!!!


Augustine Mrema (kushoto) na Edward Lowassa.
Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema amesema biashara ya kugombea urais mwaka 2015 haiwezi kamwe na ametaka ifanywe na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.
Mrema alisema hayo jana kabla ya harambee ya Saccos ya Walimu wa Wilaya ya Moshi Vijijini, iliyoongozwa na Lowassa katika uwanja wa Ushirika mjini hapa.
Alisema kugombea urais mwaka 2015 ni biashara kubwa kwake kwani amezoea kufanya biashara ndogo ya rejareja yaani ubunge na kumwomba Mungu mwaka huo ufike kwani atakuwa tayari kumwunga mkono Lowassa kwenye kinyang’anyiro hicho.
‘’Nasema biashara ya urais ni biashara kubwa kwangu kwa sasa na biashara hiyo namwachia Lowassa na niko tayari kumwunga mkono kwa hali na mali,’’ alisema Mrema

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI TAREHE 15.06.2013

.
.

Friday, June 14, 2013

IJUE HISTORIA YA MAREHEMU LANGA KILEO 'LANGA'


Ni mtaalamu na mwanamuziki stadi wa Hip Hop nchini aliyeweka wazi kuathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya.
 Ili kuonyesha anachukizwa, Langa alilieleza jarida moja la burudani kwamba anakusudia kuanzisha Taasisi ya kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya.

Alisema matumizi ya dawa hizo yaliathiri shughuli zake za muziki na hakuwa na jambo lolote endelevu katika muziki wake.

Kimuziki Langa alianzia kundi la Wakilisha akiwa na Witness Mwaijega na Sarah Kaisi, ambapo walikuwa washiriki wa mashindano ya muziki ya Cocacola Pop stars, yaliyofanyika nchini Afrika Kusini.

Wakiwa na kundi hilo walifanikiwa kufyatua kibao cha ‘Hoi’, ambacho kiliteka wapenzi wa muziki.

Baadaye Sarah Kaisi (Shaa) alijitoa. Lakini Langa na Witness walifyatua kibao cha ‘No Chorus’.

Baada ya hapo Langa alifyatua kibao chake cha kwanza akiwa mwanamuziki binafsi, ‘Matawi ya Juu’ ambacho Dj John Dilinga (JD) aliwahi kuelezea ni moja ya kazi nzuri kutoka kwake, licha ya dosari za matumizi ya lugha.

Hata hivyo Langa alionyesha yeye ni bora na ana kipaji cha muziki. Amekuwa shujaa kwa kuendesha kampeni kali za kupinga matumizi ya dawa za kulevya kwa vijana. Serikali inapaswa kusaidia juhudi zake pamoja.Huyu ni mmoja wa matunda ya shindano la muziki la Coca-Cola Pop Stars mwaka 2004 ambalo washindi wake waliounda kundi la Wakilisha.  Mbali ya Langa, wengine ni Sarah Kaisi `Shaa’ na Witness Mwaijaga `Witness’. Huo ndio uliokuwa mwanzo wa kung’ara kisanii kwa wakali hao, ingawa kwa sasa kundi hilo limesambaratika, kila mmoja akitamba kivyake.

HII NDIO MAKALA YA KWANZA YA LWAKATARE BAADA YA KUTOKA JELA '"MREJESHO KUTOKA MAHABUSU"

Sina budi kumshukuru sana mwenyenzi Mungu kwa kunitendea mema na zaidi ya yote kunipa uhai na afya hadi sasa. Wanasema “shukuruni katika yote” na mimi nalazimika kushukuru kwa yale yote niliyofunuliwa na kuwa sehemu ya ushuhuda wangu katika maisha niliyobakiza hapa duniani.

Namshukuru Mungu muweza wa yote kwa kunirejesha tena uraiani na kwa kuniunganisha na familia yangu,mke na watoto,wazazi ,ndugu,majirani na marafiki,viongozi wenzangu na wanachama wa chama kikubwa CHADEMA na zaidi ya yote watanzania walio wazalendo wanaoipenda na kuipigania nchi yao.

Ninapojikuta huru nje ya milango ya mninga uliowekewa makufuli makubwa,madirisha yenye nondo,ukuta uliowekewa waya wenye miiba mikali na ulinzi wa maaskari wanaonichunga saa 24,inanikumbusha wimbo mmoja wa mchakamchaka uliokuwa ukiimbwa gerezani kila siku saa 11:00 alfajiri tunapoamshwa uliokuwa na maneno;

“Kama raia!kama raia!kama raia!kama raia!
Iko siku moja nitarudi kwetu kwa baba na mama kama raia!
Iko siku moja nitarudi kwetu kwa ndugu na rafiki kama raia!
Kama raia…….”

SIMBA, YANGA NA SUPER FALCONS KAZI KWAO, ZARUHUSIWA KWENDA DARFUL....!!!

amos

Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Siku chache baada ya Serikali ya Tanzania kukataa kuziruhusu timu tatu za Tanzania, Simba , Yanga na Super Falcons ya visiwani Zanzibar kushiriki michuano ya kombe la Kagame, leo hii Serikali imeziruhusu klabu hizo kwenda Sudan kushiriki michuano ya Klabu Buingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Amos Makalla akiongea na waandishi wa habari kanda ya kati Dodomo asubuhi ya leo amesema wameruhusu klabu hizo ziende Sudan baada ya kuhakikishiwa na Serikali ya nchi hiyo kwamba itatoa ulinzi wa kutosha dhidi ya timu za Tanzania.
Makalla amesema wameandikiwa barua na Serikali ya Sudan ikiwahakikishia kwamba timu za Tanzania zitapewa ulinzi mkubwa zisiathirike na machafuko yanayoedelea Sudan.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...