Waziri
Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akiwapungia mkono walimu walioshiriki
katika hafla ya harambee ya kuchangia Saccos ya walimu iliyofanyika
kwenye Viwanja vya Chuo cha Ushirika Moshi, jana. Picha na Dionis
Nyato.
Waziri
Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema kuwa ana ndoto kwamba siku moja
sekta ya elimu itapewa kipaumbele cha kwanza nchini na kuzikomboa
rasilimali za taifa la Tanzania zinazowanufaisha wageni na kuacha
wananchi wakiambulia faida kidogo.Huku
akimtaja Dk Martin Luther King aliyekuwa mwanaharakati wa haki za
Wamarekani weusi aliyefariki kabla ya kuuona utimilifu wa ndoto yake,
Lowassa alisema kuwa anamwomba Mungu asimwondoe duniani ili aweze
kushiriki kuifanya ndoto hiyo kuwa kweli itakayokamilika siku si nyingi
ambapo viongozi watakubali kuwa elimu bora ndiyo itakayowasaidia
Watanzania kuchimba madini yao na kuyauza kwa faida duniani.
Akizungumza wakati wa kuchangia SACCOS ya walimu ya Moshi Vijijini, Ushirika wa Stadium jana, Lowassa alisema kuwa katika ndoto yake anawaona viongozi wakikubali kwamba elimu bora ndiyo italisaidia taifa kuumiliki utalii na kunufaika nao, badala ya kuwaachia wageni wanufaike nao, huku Watanzania tukiambulia makombo.Wakati Lowassa akieleza ndoto yake hiyo, Mwenyekiti wa TLP na mbunge wa Vunjo Augustine Mrema amesema: “Biashara ya urais imenishinda namwachia Lowassa kwani mimi nimeamua kurudi kwenye biashara ya rejareja.”