Saturday, June 15, 2013

MREMA AKABIDHI URAIS KWA LOWASSA MWAKA 2015...!!!


Augustine Mrema (kushoto) na Edward Lowassa.
Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema amesema biashara ya kugombea urais mwaka 2015 haiwezi kamwe na ametaka ifanywe na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.
Mrema alisema hayo jana kabla ya harambee ya Saccos ya Walimu wa Wilaya ya Moshi Vijijini, iliyoongozwa na Lowassa katika uwanja wa Ushirika mjini hapa.
Alisema kugombea urais mwaka 2015 ni biashara kubwa kwake kwani amezoea kufanya biashara ndogo ya rejareja yaani ubunge na kumwomba Mungu mwaka huo ufike kwani atakuwa tayari kumwunga mkono Lowassa kwenye kinyang’anyiro hicho.
‘’Nasema biashara ya urais ni biashara kubwa kwangu kwa sasa na biashara hiyo namwachia Lowassa na niko tayari kumwunga mkono kwa hali na mali,’’ alisema Mrema

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI TAREHE 15.06.2013

.
.

Friday, June 14, 2013

IJUE HISTORIA YA MAREHEMU LANGA KILEO 'LANGA'


Ni mtaalamu na mwanamuziki stadi wa Hip Hop nchini aliyeweka wazi kuathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya.
 Ili kuonyesha anachukizwa, Langa alilieleza jarida moja la burudani kwamba anakusudia kuanzisha Taasisi ya kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya.

Alisema matumizi ya dawa hizo yaliathiri shughuli zake za muziki na hakuwa na jambo lolote endelevu katika muziki wake.

Kimuziki Langa alianzia kundi la Wakilisha akiwa na Witness Mwaijega na Sarah Kaisi, ambapo walikuwa washiriki wa mashindano ya muziki ya Cocacola Pop stars, yaliyofanyika nchini Afrika Kusini.

Wakiwa na kundi hilo walifanikiwa kufyatua kibao cha ‘Hoi’, ambacho kiliteka wapenzi wa muziki.

Baadaye Sarah Kaisi (Shaa) alijitoa. Lakini Langa na Witness walifyatua kibao cha ‘No Chorus’.

Baada ya hapo Langa alifyatua kibao chake cha kwanza akiwa mwanamuziki binafsi, ‘Matawi ya Juu’ ambacho Dj John Dilinga (JD) aliwahi kuelezea ni moja ya kazi nzuri kutoka kwake, licha ya dosari za matumizi ya lugha.

Hata hivyo Langa alionyesha yeye ni bora na ana kipaji cha muziki. Amekuwa shujaa kwa kuendesha kampeni kali za kupinga matumizi ya dawa za kulevya kwa vijana. Serikali inapaswa kusaidia juhudi zake pamoja.Huyu ni mmoja wa matunda ya shindano la muziki la Coca-Cola Pop Stars mwaka 2004 ambalo washindi wake waliounda kundi la Wakilisha.  Mbali ya Langa, wengine ni Sarah Kaisi `Shaa’ na Witness Mwaijaga `Witness’. Huo ndio uliokuwa mwanzo wa kung’ara kisanii kwa wakali hao, ingawa kwa sasa kundi hilo limesambaratika, kila mmoja akitamba kivyake.

HII NDIO MAKALA YA KWANZA YA LWAKATARE BAADA YA KUTOKA JELA '"MREJESHO KUTOKA MAHABUSU"

Sina budi kumshukuru sana mwenyenzi Mungu kwa kunitendea mema na zaidi ya yote kunipa uhai na afya hadi sasa. Wanasema “shukuruni katika yote” na mimi nalazimika kushukuru kwa yale yote niliyofunuliwa na kuwa sehemu ya ushuhuda wangu katika maisha niliyobakiza hapa duniani.

Namshukuru Mungu muweza wa yote kwa kunirejesha tena uraiani na kwa kuniunganisha na familia yangu,mke na watoto,wazazi ,ndugu,majirani na marafiki,viongozi wenzangu na wanachama wa chama kikubwa CHADEMA na zaidi ya yote watanzania walio wazalendo wanaoipenda na kuipigania nchi yao.

Ninapojikuta huru nje ya milango ya mninga uliowekewa makufuli makubwa,madirisha yenye nondo,ukuta uliowekewa waya wenye miiba mikali na ulinzi wa maaskari wanaonichunga saa 24,inanikumbusha wimbo mmoja wa mchakamchaka uliokuwa ukiimbwa gerezani kila siku saa 11:00 alfajiri tunapoamshwa uliokuwa na maneno;

“Kama raia!kama raia!kama raia!kama raia!
Iko siku moja nitarudi kwetu kwa baba na mama kama raia!
Iko siku moja nitarudi kwetu kwa ndugu na rafiki kama raia!
Kama raia…….”

SIMBA, YANGA NA SUPER FALCONS KAZI KWAO, ZARUHUSIWA KWENDA DARFUL....!!!

amos

Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Siku chache baada ya Serikali ya Tanzania kukataa kuziruhusu timu tatu za Tanzania, Simba , Yanga na Super Falcons ya visiwani Zanzibar kushiriki michuano ya kombe la Kagame, leo hii Serikali imeziruhusu klabu hizo kwenda Sudan kushiriki michuano ya Klabu Buingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Amos Makalla akiongea na waandishi wa habari kanda ya kati Dodomo asubuhi ya leo amesema wameruhusu klabu hizo ziende Sudan baada ya kuhakikishiwa na Serikali ya nchi hiyo kwamba itatoa ulinzi wa kutosha dhidi ya timu za Tanzania.
Makalla amesema wameandikiwa barua na Serikali ya Sudan ikiwahakikishia kwamba timu za Tanzania zitapewa ulinzi mkubwa zisiathirike na machafuko yanayoedelea Sudan.

BAADA YA KUPATA TUZO MBILI ZA KILI DIAMOND AMSUTA ‘MGANGA WAKE’

Nasibu Abdul ‘Diamond’.
STAA anayeng’aa katika Muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amemsuta mganga aliyejitokeza na kudai kwamba mwaka huu staa huyo hatapata mafanikio yoyote na  atapotea katika fani.
Mganga huyo ambaye alidai utaalamu wake ndiyo uliompandisha chati Diamond alisema  mwaka huu staa huyo hatapata tuzo, atafifia na jina lake litasahaulika kutokana na kukiuka masharti yake.

Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Diamond alisisitiza kutomtambua mganga huyo na anamshangaa kwa kuwa mwaka huu amepata mafanikio tofauti na alivyosema.
“Hebu angalieni, mganga alidai mwaka huu nitafutika katika fani, mbona nimepata tuzo mbili kwenye Kil na nimechaguliwa kuwa balozi wa Cocacola na shoo zinajaza kinoma?” alihoji Diamond.
Aidha, alisema shoo zake bado zinajaza watu wengi huku akiitolea mfano ya mwisho iliyofanyika Dar Live, Mbagala Zakhem, Dar hivi karibuni iliyojaza nyomi ya watu.
 
NA GPL

WANAFUNZI WA CHUO KIMOJA MKOANI MTWARA WAFANYA PARTY YA KIFUSKA

Pombe  iko  kichwani  hapo....Kila  kitu  kwake  ni  sawa ..

Katika hali isiyokuwa ya kawaida,  wanafunzi wa chuo kimoja maarufu Mkoani Mtwara hivi karibuni walifanya party ya ufuska na kuwaacha watu midomo wazi kwa mambo yaliyokuwa yanatendeka.
Party hiyo ambayo  ilifanyika ndani ya pub moja  mkoani  humo  ilihudhuriwa  kwa  wingi  na  wanafunzi wa chuo  hicho  ambao  wengi  wao  walikuwa  wamevaa  kihasara ...

 Huyu  ni mmoja wa wanafunzi hao aliyefahamika kwa jina la Zaitun ambae anasoma mwaka wa kwanza katika chuo hicho.

KINANA AMBURUZA KORTINI MBUNGE MSIGWA BAADA YA KUMWUITA JANGILI

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdul-rahman Kinana amemfungulia kesi Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa (Chadema), kutokana na kumtuhumu anajihusisha na ujangili na biashara haramu ya pembe za ndovu.
Kinana amefungua kesi hiyo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutokana na kitendo cha Mbunge huyo kutoa tuhuma hizo dhidi yake kwa nyakati tofauti nje na ndani ya Bunge, pia alikataa kuzikanusha na kumuomba radhi.
Inadaiwa kuwa Aprili 21 mwaka huu Msigwa ambaye ni Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii alitoa tuhuma hizo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Shule ya Msingi Mbuguni wilayani Nyamagana mkoani Mwanza.
Aidha alizitoa bungeni wakati akiwasilisha hotuba ya Kambi ya Upinzani katika Makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii mwaka 2013/2014. Katika hati ya madai, Kinana anadai kuwa kutokana na tuhuma hizo ameharibiwa tabia yake, uaminifu, hadhi yake kitaaluma na weledi na kumfanya achukiwe na kudharauliwa katika jamii.
Anadai jina lake na heshima ambayo ameijenga kwa muda mrefu, vimharibiwa na Msigwa kwa nia mbaya, pia kwa tuhuma hizo anazosisitiza kuwa ni za uwongo, licha ya kumsababishia maumivu ya kisaikolojia, pia zimemsababishia hasara ya fedha.
Anadai kuwa kabla ya tuhuma hizo alikuwa katika hatua za mwisho za mchakato wa mazungumzo ya mradi wa ubia wa kilimo cha mboga na mwekezaji kutoka kampuni ya nje, lakini tuhuma hizo zimesababisha kampuni hiyo kuvunja majadiliano hayo.
Kinana anadai kuwa sababu iliyotolewa na kampuni hiyo kuvunja mazungumzo hayo ni kutajwa kwake na mbunge huyo kuwa ni jangili anayejishughulisha na biashara hiyo.

TAARIFA KAMILI KUHUSU KIFO CHA LANGA NA RATIBA YA MAZISHI...!!


Wakati ambapo mashabiki wa muziki wa Hip Hop nchini wakianza kusahau majonzi ya kumpoteza Albert Mangweha aka Ngwair mwezi uliopita, leo wametoneshwa tena kwa kifo cha mwana hip hop mwingine, Langa Kileo aka Lyrically And Naturally Gifted African.
971547_562592510448211_1469657651_n
Kwa mujibu wa Afisa Uhusiano wa hospitali ya taifa ya Muhimbili, Aminiel Aligaesha aliyezungumza na Clouds FM, Langa amefariki leo June 13, saa 11 jioni baada ya kufikishwa hospitalini hapo tangia juzi mida ya jioni. Hata hivyo amesema kutokana na maadili na taratibu za hospitali asingeweza kutoa chanzo cha kifo cha Langa na jukumu hilo ni la ndugu zake.
Hata hivyo taarifa za awali zilidai kuwa Langa alikuwa anaumwa Malaria kali iliyopelekea kukimbizwa Muhimbili jana jioni.
Baba wa marehemu Mzee Kileo amesema taarifa kamili na mipango ya mazishi zitatolewa pale vikao vya familia vitakapofanywa.Pia baba yake alisema msiba huu umetokea wakati mama yake Langa hayupo Tanzania,alisema kwa sasa mama yake Langa yupo Marekani lakini baada ya kupewa taarifa hizo tayari ameshakata tiketi ya kurudi Tanzania na ataanza safari kesho.Msiba uko nyumbani kwao maeneo ya Mikocheni(Anna Peter).

MAJINA YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA 2013 NA KAMBI ZA JESHI WALIKOPANGIWA...TAREHE YA KURIPOTI NI 24 MWEZI HUU

TANGAZO
MKUU WA JKT MEJA JENERALI RAPHAEL MUHUGA ANAWAITA VIJANA 10,849 WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA MWAKA 2013 KUJIUNGA NA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA KAMA IFUATAVYO:-

1. VIJANA WOTE WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA WALIOPATA DIVISION I NA DIVISION II.

2. VIJANA WOTE WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA WALIOSOMA MASOMO YA MCHEPUO WA SAYANSI NA KUPATA DIVISION III.

3. VIJANA HAO WANATAKIWA KURIPOTI KATIKA MAKAMBI YA JKT TAREHE 24 JUNI 2013 BILA KUKOSA. AMBAYE HATARIPOTI ATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA.

4. TANGAZO HILI HALIWAHUSU VIJANA WOTE WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA 2013 KATIKA SHULE ZA SEKONDARI ZA UNGUJA NA PEMBA. AIDHA, SHULE 27 AMBAZO VIJANA WAKE WAMEHITIMU MAFUNZO YA JKT AWAMU YA KWANZA HAZIHUSIKI.

5. VIJANA HAO WATUNZE TIKETI ZAO KWA AJILI YA KUREJESHEWA NAULI WATAKAZOTUMIA MARA TU WATAKAPORIPOTI VIKOSINI.

6. TAARIFA ZAIDI ZITATOLEWA KWENYE MAGAZETI MBALIMBALI YA HAPA NCHINI.


Zifuatazo  ni  selection  za  kambi  walikopangiwa
 Attached Files

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JUNI 14, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.

.
.
.
.

Thursday, June 13, 2013

KAULI YA BALOZI WA TANZANIA KUHUSU MSICHANA ANAYEDAIWA KUTAKA KUNYONGWA BAADA YA KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA EGYPT

.
Baada ya watu wengi kuzipata habari na bila kujua imekuaje kwa Mtanzania anaedaiwa kukamatwa na dawa za kulevya nchini Egypt na kwamba alikua anakaribia kunyongwa, balozi Mohamed Haji wa Tanzania nchini Egypt ameongea Exclusive na millardayo.com na kueleza yote anayoyafahamu kuhusu hii ishu. Namkariri akizungumza 1. Ni kweli kuna raia wawili Watanzania wamekamatwa na dawa za kulevya ambao ni Mbarak Abdallah Salim (28) na Sharifa Mahmud (27) wakazi wa Magomeni Kagera Dar es salaam, wanaundugu wa mtoto wa shangazi na mjomba. 2. Walikamatwa tarehe 16 May 2013 wakati wakiingia Misri, kwa mujibu wa maelezo safari yao ilianzia Dar es salaam kwenda Mombasa, Nairobi mpaka Misri.
.
3. Dawa za kulevya walizokamatwa nazo zimetajwa kwamba ni Heroine kilo saba. 4. May 18 2013 ndio tuliitwa kwenda kutazama Raia wetu, nikatuma maafisa wawili wazuri kwenda kutazama ili raia wetu wasimbambikiwe kesi. 5. Baada ya hapo waliwekwa rumande na tukapata nafasi ya kuwaunganisha na nyumbani huku Tanzania wakaongea kwenye simu kilichowapata. . 6. 26 May 2013 ndio walipelekwa Mahakamani kwa mara ya kwanza na kurudishwa rumande wote wawili. 7. Hawa ndio Watanzania wa kwanza kukamatwa na kesi kama hii na ikithibitishwa wamefanya kweli, hili kosa ndilo litakua doa la kwanza kwa Tanzania hapa Misri. 8. Ishu ya kunyongwa, tunajaribu kufanyia kazi lakini hakuna kumbukumbu za mgeni yeyote kwa sisi tunavyojua ambae amewahi kunyongwa kuhusu ishu ya dawa za kulevya. 9. Tunajitahidi kuwasiliana na mamlaka zinazohusika ili kujua siku gani watapelekwa tena Mahakamani alafu tutawafahamisha nyumbani. Kwa ushahidi unaweza kumsikiliza balozi hapa chini na pia kutazama video hapo chini ya ushahidi wa kukamatwa na dawa za kulevya…

PICHA ZA KALA JEREMIAH AKIAMKABIDHI MAMA MZAZI WA MANGWAIR TUZO YAKE

Mama mzazi wa marehemu Albert Mangweha akiwa ameshikilia tuzo aliyopewa kwa niaba ya mwanae, tuzo hii aliipata msanii Kala Jeremiah kwenye tuzo za Kilimanjaro ikiwa kama tuzo ya msanii bora ya Hip Hop 2013-14


 
 
 
 

MH: ZITO KESHO KUWA MGENI RASMI SHOW YA MWANA FA, HUKU SUGU AKIWA KWA JIDE

 
Ile the Big Square 1, show za magwiji wa muziki Tanzania mwana FA ‘The Finest’ na Lady Jay Dee ‘Miaka 13 ya Lady Jay Dee’ zitapigwa kesho June 14, huku presha ikiwa inaongezeka hasa kwa fans wanaotamani kuhudhuria show walioichagua na kuona ukubwa wa show kama walivyotarajia.

Show hizi kubwa zina nguvu sana kutokana na ukubwa wa majina ya wasanii husika. Kwa mujibu wa lady Jay Dee timu anaconda kesho itaungwa mkono na mheshimiwa Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu.

Jide ambae hivi karibuni ameachia wimbo mpya unaopatikana kwenye album yake ‘Nothing but the truth’ inayoitwa Yahaya, amepost kupitia kupitia ukurasa wake wa facebook na pia katika akaunti yake ya Twitter kuonesha list ya wasanii watakaopanda jukwaani, na pia uwepo wa Sugu.

” Miaka 13 ya Lady JayDee, Ijumaa ya kesho shughuli inaanza rasmi saa 3:00 usiku...Ukiskia paaaa ujue show imeisha

1. Prof Jay 2. Juma Nature 3. Grace Matata 4. Hamza Kalala 5. Wakazi na ugeni wa Mh. Joseph Mbilinyi a.k.a SUGU

Nyimbo zote unazozipenda zitalia tar 14 June, pale Nyumbani Lounge sababu yaaaaa sababu yaaaaaa ?????????”


Kwa upande wa Mwana FA ambae atapiga show yake na Live band akiwa na kundi kubwa na maarufu kwa upigaji wa Live Band ‘Wananjenje’, yeye amepewa full sapoti na mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto kabwe.
Zitto ameweka wazi kupitia akaunti yake ya twitter kuwa anamsapoti sana msanii huyo.

“You have my full support “@MwanaFA”

"BABY MADAHA ASITAKE KUPATA UMAARUFU KUPITIA JINA LANGU TENA ANIKOME" ...... JACK WOLPER

MWANADADA anayefanya vizuri katika tasnia ya filamu Jaqueline Massawe ‘Wolper Gambe’ amesema anamshangaa sana msanii wa muziki ambaye pia ni mwigizaji Baby Madaha kutumia vyombo vya habari kutengeneza ugomvi wakati hana mawasiliano naye yoyote na wala si rafiki yake au mtu aliyekaribu naye na hana mazoea naye.


“Nimelizika na umaarufu nilio nao sihitaji kujipeleka katika magazeti na kuongelea vitu ambavyo havina faida katika jamii, mimi sina urafiki na Baby Madaha, namshanga anavyotapatapa kuniandika vibaya kwa jambo lisilo nihusu, mambo hayo niliyafanya nikiwa Chipukizi”

“Nakumbuka mimi nilipigiwa simu na rafiki yake akiniomba namba mwenye nyumba lakini ghafla nikapiwa simu na mwandishi wa habari mara Polisi nikashangaa huyo mtu hata namba ya mwenye nyumba sijamtumia nasumbuliwa na watu utafikiri mimi ndio mtuhumiwa, lakini jambo ninalomshangaa mimi ni dalali?,” alihoji Wolper.
Hivi karibuni yalizuka maneno yakiwahusisha wasanii hawa wawili ikisemekana walikuwa wakigombea nyumba ya kupanga, huku Baby Madaha kuigizwa mjini na mwenye nyumba kwa kupangishwa nyumba hewa, Wolper amedai kuwa kwa sasa yeye amekuwa makini halipii nyumba kienyeji bali ulipia kwa mwanasheria wake tena kwa kufuata taratibu kwa kukwepa utapeli.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...