Na Gladness Muushi wa Fullshangwe-Meru
Chama cha mapinduzi Wilaya ya Meru kimefanikiwa kutoa Kiasi cha
Shilingi Milioni sita pamoja na ahadi ya Milioni nane ikiwa ni ahadi
ya Katibu mkuu wa chama hicho Abdulrahman Kinana aliyotoa mwaka jana
kwa ajili ya maendeleo ya vijana na wanawake wa Wilaya hiyo ingawaje
inatawaliwa na wapinzani
Akikabidhi fedha hizo mapema jana katika uzinduzi wa mashina ya
wakereketwa wa ccm mjumbe wa kamati ya siasa mkoa wa arusha John
Pallangyo alisema kuwa fedha hizo ni moja ya ahadi zilizotolewa na
katibu mkuu wa ccm taifa Abdulrhaman Kinana mara alipofanya ziara ya
kujitambulisha mwaka jana
Alisema kuwa mara baada ya katibu huyo kufanya ziara wilayani humo
aliamua kuwaunga mkono vijana wa bodaboda na wanawake wajasiramali
wa wilaya hiyo mkono ili waweze kujiendeleza kiuchumi ili waweze
kujikwamua katika hali ngumu ya kimaisha.
Aliongeza kuwa kwa kuwa ajira ni sehemu ya ilani ya chama cha
mapinduzi wameamua kutekeleza ahadi hiyo ili kuhakikisha kuwa vikundi
hivyo vinajiendeleza na kuachana na hali ya kuwa tegemezi kwa kuwa
kupitia fedha hizo wataweza kujipatia mitaji ya kujienedeleza.
“Katika kutekeleza ilani ya chama chetu cha mapinduzi ni lazima
kuhakikiasha kuwa ajira inakuwepo hasa kwa vijana hivyo naombeni fedha
hizi mzitumie kwa uangalifu ili ziweze kuwasaidia kujiajiri wenyewe na
pia zitawasaidia kuachana na makundi ya upotoshaji”alisema Pallangyo
Kwa upande wake katibu wa chama hicho wilaya ya meru Langaeli Akyoo
alitoa wito kwa vijana wote na wanawake wa uwt wilayani humo kutumia
vizuri mitaji waliyopewa na chama hicho na kuhakikisha kuwa fedha hizo
zinawabadilishia hali zao za maisha pamoja na familia zao.
Aidha akyoo akielezea kuhusiana na uzinduzi wa mashina ya wakereketwa
alisema kuwa ni mkakati wa wa chama hicho wa kuhamasisha wananchi wote
katika harakati zake za kurudisha jimbo lililoko chadema na
kulirudisha mikononi mwao
Hata hivyo katika uzinduzi huo mashina yaliyozinduliwa ni pamoja na
kilala,usa madukani,sabato,imbaseny madukani,mji mpya,njia ng’ombe
,kimandafu pamoja na Arudeco.