Dodoma. Baada ya kutumikia adhabu ya kutohudhuria vikao vitano vya
Bunge, wabunge watano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
jana waliingia bungeni wakionekana kuwa na ari mpya.
Wabunge waliosimamishwa Aprili 17 ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya
Upinzani Bungeni ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu
na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa.
Wengine ni Highness Kiwia (Ilemela), Ezekiel Wenje (Nyamagana),
Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (Mbeya Mjini) na Godbless Lema (Arusha Mjini).
Jana
asubuhi Mchungaji Msigwa alikuwa miongoni mwa wabunge waliowahi kuingia
mapema ndani ya Ukumbi wa Bunge na kufuatiwa na Lissu muda mfupi baada
ya kikao kuanza.
Ndani ya Ukumbi wa Bunge, Msigwa
alipata nafasi ya kuuliza swali namba 115 lililokuwa liulizwe na Joyce
Mukya kuhusu Kampuni ya Kamwene Woodworks . Kwa upande wake, Lissu
aliomba mwongozo wa Spika kuhusu kukwama kwa Bajeti ya Wizara ya Maji.
Wabunge wengine haikujulikana sababu za kutofika jana licha ya
kuwa adhabu yao ilikwisha tangu April 25 huku taarifa zikieleza kuwa
Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema alikuwa apelekwe mahakamani kujibu
staka la uchochezi.
Mwananchi