Thursday, April 25, 2013

FFU WAACHA LINDO NA KUINGIA DISCO KUKATA MAUNO


ASKARI Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) mkoani Kilimanjaro wanaolinda mipaka kukabiliana na biashara za magendo zisiende Kenya, wanadaiwa kuacha lindo na kutinga ukumbi wa disko wakiwa na silaha nzito za kivita aina ya SMG.

Tukio hilo lilitokea usiku wa Aprili 20 mwaka huu, ambapo askari hao zaidi ya watano waliingia katika ukumbi wa disko wa High Way uliopo njia panda ya Himo na hivyo kutoa mwanya kwa magari sita aina ya Fuso yaliyokuwa yamesheheni sukari ya magendo kupita kirahisi kwenda nchini Kenya.
  
Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima umebaini kuwa baada ya askari hao kutinga katika ukumbi huo, ilichukua muda wa dakika 20 magari yakaanza kupita eneo hilo ambako askari hao walikuwa wameweka doria katika barabara ya Mwika.

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS 25.04.2013

9 b8945

1 eeb16
2 3508b

Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) amwonya Rais kutoipigia debe CCM.


Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) amemtahadharisha Rais Jakaya Kikwete asiitumie ziara yake ya Mkoa wa Mbeya kukipigia debe Chama Cha Mapinduzi(CCM) bali afanye kazi za kiserikali.


Rais Kikwete anatazamiwa kuwasili mkoani Mbeya, Jumapili ijayo kwa ziara ya kikazi ya siku nne.


Akizungumza katika mkutano wa hadhara jana Mjini Mbeya, Sugu alisema kuwa kitendo hicho kitasaidia kuimarisha umoja miongoni mwa wananchi wa Mbeya.


“Wakazi wa Mbeya muwe tayari kumpokea Rais Kikwete endapo ataifanya ziara yake kuwa ya kiserikali na yeye akiwa ni rais wa nchi na siyo kuifanya ziara hiyo kuwa ya kisiasa kwa vile tu yeye ni mwenyekiti wa CCM,”alisema Sugu.

Wednesday, April 24, 2013

UWOYA KUJIPATI MILIONI 200 ZA BUREEEEE KUTOKA GLOBAL PUBLISHERS BAADA YA KUCHAFULIWA: GLOBAL KUANIKA VIDEO YA TUKIO ZIMA HOTELINI:


 Mfano wa sehemu ya fedha atazolipwa Uwoya
DIVA anayetesa katika sinema za Bongo, Irene Pancras Uwoya ananukia utajiri ambapo hivi karibuni ‘anatarajia’ kuogelea kwenye  mamilioni ya fedha kwa kukomba Shilingi Milioni 200 za madafu, Risasi Mchanganyiko lina kila kitu mkobani.
Uwoya ni mke halali wa msakata kabumbu wa kulipwa nchini Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ ambapo ndoa yao ilifungwa

mwaka 2009 katika Kanisa Katoloki, Parokia ya Mt. Joseph, Posta jijini Dar es Salaam.

KUTOKA DAR ES SALAAM
Msanii huyo ambaye hakaukwi na skendo, huenda akaibuka milionea ikithibitika kwamba habari iliyoandikwa na gazeti damu moja

na hili, Ijumaa Wikienda la Jumatatu Aprili 8 – 14, toleo namba 310 iliyokuwa na kichwa; UWOYA, DIAMOND WANASWA

HOTELINI ni ya uongo.
Habari kutoka katika vyanzo vyetu vya kuaminika, zinasema kuwa  mdada huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja aitwaye Krish

Hamad Ndikumana yu mbioni kuandika barua ya madai kupitia kwa mawakili wake  waliopo Dar ili kudai fedha hizo kwa maelezo

(eti) alichafuliwa na kuingiliwa faragha yake.

BINTI ANUSURIKA KUBAKWA BAADA YA KUKATIZA MITAA YA SINZA AKIWA AMEVAA KIMINI

Wanawake ambao majina yao hayakupatikana, wakazi wa Sinza, Dar es Salaam wamekumbana na sekeseke  la aina yake la ubakaji kisa kikiwa ni uvaaji wa vimini ambao kwa sasa umeshika kasi kila kona Bongo...
Mwanahabari wetu mwishoni mwa wiki iliyopita usiku wa manane, alinyetishiwa tukio la wanawake watatu kuvamiwa na midume na kufanyiwa kitu mbaya baada ya  kuchaniwa vimini vyao maeneo ya Barabara ya Shekilango, Dar kabla ya kuokolewa na wasamaria wema.
Wasichana hao, wakiwa wamejipodoa vilivyo na kutinga vimini vilivyoonesha sawia maungo yao nyeti bila ‘makufuli’, walijikuta  katika hali hiyo mbaya baada ya kurushiana maneno na vijana hao wahuni hivyo wakaonja joto ya jiwe.

Warembo hao ambao walikuwa wakitokea Sinza kuelekea Manzese, Dar walivamiwa na vijana hao ambao wengi wao ni waendesha  pikipiki maarufu kama bodaboda,  walipokaribia Makutano ya Barabara ya Shekilango na Morogoro, Dar.

“Kila siku wanapita hapa wakiwa nusu utupu, sasa leo tumewakomesha, serikali inatangaza Ukimwi ni hatari, wao hawajali,  wanatutia majaribuni,” alisikika akisema mwendesha bodaboda mmoja ambaye alikuwa miongoni mwa waliowavamia wasichana
hao.

Mwendesha bodaboda mwingine alimwambia  mwandishi wetu  kuwa waliwaeleza wasichana hao kuacha tabia ya kutembea nusu utupu kwani ni hatari kwa maisha yao na ni kinyume cha maadili ya Watanzania lakini walijifanya jeuri ndiyo maana wakawaadabisha.
Aliweka wazi kuwa baada ya kuelezwa hivyo akina dada hao hawakufurahishwa na maneno hayo na badala yake
wakawaporomoshea matusi mazito madereva hao, hali iliyowafanya wapandwe na hasira.
“Madereva wale baada ya kusikia wakitukanwa waliwavamia wasichana hao na kuanza kuwachania nguo kwa maelezo kwamba badala ya kuwa nusu utupu, ni vema wakakaa uchi wa mnyama kabisa.

“Warembo wawili walifanikiwa kutimua mbio licha ya kuchaniwa vimini vyao lakini mmoja aliyekuwa na ‘mdomo mchafu’ 

“Shukrani ziwaendee wasamaria wema waliomukoa kwa sababu kwa vyovyote lazima angebakwa kwani alikuwa  ameshachaniwachaniwa nguo na ku... ,” alisema shuhuda mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake.

Shuhuda huyo aliongeza kuwa binti huyo alifanyiwa kitu mbaya kwa kushikwa sehemu nyeti kabla ya wale wenzake waliokimbia kurudi wakiwa kwenye Bajaj na mabaunsa wao kisha kutokomea na mwenzao aliyekuwa amehenyeshwa vya kutosha na wanaume
hao.

“Wale wasichana wawili walirudi wakiwa na Bajaj na mabaunsa, wakasaidiwa na raia wema ndipo wakafanikiwa kumuokoa  mwenzao na kutokomea naye kusikojulikana,” alisema shuhuda huyo.

Credit: GPL

SUALA LA JUMA NATURE KUTIMULIWA CHANNEL 5 ALIPOINGIA NA NDALA LACHUKUA SURA MPYA ....


Kitendo cha mtangazaji wa EATV Sam Misago kumtoa nje ya studio Sir Juma Nature weekend iliyopita baada ya kwenda studio kwenye kipindi cha Saturday Night Live akiwa na ndala na kaoshi, hajakichukulia poa staa huyo.
  
Licha ya kuwasilisha malalamiko yake kwenye Facebook kutokana na kitendo hicho, Nature hajaishia hapo na sasa amemchana mtangazaji wa kipindi hicho kwenye wimbo mpya wa TMK Halisi, Fitina.
Katika wimbo huo Nature anachana, “Halafu watu wengine sijui wanakuwaga ni mapimbi, eti msanii kaingia studio na ndala na amevaa pensi hakujua anayosema kwenye Facebook na Twitter sijui kisa hela alizopewa na mameneja feki wasiopenda wa Uswazi, mzomeeni huyo, sasa kazi kwake na raia wake.”

MAGAZETI YA LEO JUMATANO TAREHE 24.04.2013

.
.
.
.
.
.

Mdogo wa Wema aibukia Redds Miss Hai.

WAREMBO 14 kutoka vitongoji vitano vya wilaya za Siha na Hai, Kilimanjaro, akiwemo mdogo wake Wema Sepetu, wamejitokeza kushiriki shindano la kumsaka mrembo wa Hai, ‘Redds Miss Hai 2013.
Shindano hilo linalotarajiwa kulindima Hoteli ya Snow View Bomang’ombe Hai, Ijumaa.Akizungumza mjini hapa jana, muandaaji wa mashindano hayo, Grace 

Mmari, kupitia kampuni ya ulinzi ya FEM ya jijini Arusha, alisema maandalizi ya mashindano hayo yamekamilika na tayari warembo hao wako kambini kwa wiki mbili sasa katika hoteli ya Sinza B.

Alisema warembo hao wamepatikana kutoka vitongoji vya Kwa Sadala, Bomang’ombe, Sanya Juu, Machame na KIA, ambao wana vigezo vyote huku akitamba mwaka huu, Mrembo wa Tanzania atatoka wilaya ya Hai.

“Warembo wangu ni wazuri, warefu, wanajiamini na wana uwezo wa kuwakilisha vyema wilaya ya Hai, mkoa wa Kilimanjaro na hata taifa, kwa kuwa tunao kina Wolper wengine hapa na kina Sepetu wapo pia,“ alisema.

Alisema miongoni mwa warembo waliojitokeza kushiriki shindano hilo ni pamoja na mdogo wa mrembo wa zamani wa Miss Tanzania (2006), Wema Sepetu, Weru Sepetu, ambaye alidai kuwa huenda akafuata nyayo za dada yake.

Aliwataja warembo watakaoshiriki shindano hilo kuwa ni Sharon Abdalah, Zena Ally, Ivony Steven, na Winny Shayo wanaotoka Machame na Sanya Juu.
Wengine ni Julieth Kimaro, Rehema John, Mary Chemponda, Catherine Leonard na Modesta Joseph.

Mmari alisema shindano hilo litapambwa na msanii wa muziki wa kizazi kipya, Rich Mavoko pamoja na Jambo Squad, ambako mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Novatus Makunga.

Kwa upande wake, mwalimu wa warembo hao, Evameri Gamba, alisema warembo wanaendelea na mazoezi ya mwisho pamoja na kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii, ikiwemo uoteshaji wa miti na kutembelea wagonjwa katika hospitali ya wilaya ya Hai.
Shindano hilo linafanyika kwa mara ya pili sasa, huku wadhamini wakiwa ni TBL kupitia kinywaji chake cha Redds, Fem Security, Bonite Bottlers, Snow View Hotel, Panone pamoja migodi ya madini ya Anglo America Mining na Manga Germ.

Zitto Kabwe atoa majibu kwa Umma kuhusu Habari za mama yake Mzazi Bi. Shida kuvamiwa na kutishiwa bastola.


Mh.Zitto Kabwe.
Nimekuwa naulizwa kuhusu Habari za mama yangu Mzazi Bi. Shida kuvamiwa na kutishiwa bastola. Nawajibu watu Kwa ujumla kwamba 
“Moja, mie sio msemaji wa familia. Ni basi tu katika watoto wa mama yetu mie najulikana zaidi na hivyo mama anaitwa Mama Zitto. Kwetu Kigoma haitwi hivyo, ama Ni mama Salum au mama Lulu. 
Pili, hili Ni suala la polisi. Lipo polisi na linashughulikiwa na polisi. Nisingependa kulisemea wakati Ni suala linalochunguzwa na polisi. Mama yangu Ni mama wa kawaida wa kitanzania kama mama mwingine yeyote yule. Matukio ya namna hii yamezagaa nchi nzima. Hivyo suala lake litashughulikiwa kama yanavyoshughulikiwa masuala mengine yote ya Watanzania. Polisi wakimaliza uchunguzi wao naamini hatua mwafaka zitachukuliwa. 
Ushauri- tuwe makini na “Agente provocatuers” au in English “provocation agents” nyakati kama hizi. Calmness is the best protection against provocations. Nadhani mmenipata”
Nawatakia Kila la kheri katika kazi za ujenzi wa Taifa letu na kuimarisha Umoja na mshikamano wa Watanzania dhidi ya ufisadi, umasikini na ugandamizaji.
Majibu haya  ameandika kupitia mtandao wa Kijamii wa facebook.

POMBE YAMTOA MADEE...ANADAI IMEMPA HESHIMA KUBWA MTAANI......!!


Msanii wa Kundi la Tip Top Connection, Madee au Rais wa Manzese ameeleza kuwa wimbo wake wa Nani Kamwaga Pombe Yangu umempa heshima kubwa.
  
Akiongea  na  mwandishi  wetu, Madee, ambaye jina lake halisi ni Hamad Ally Seneda alisema licha ya kupata shoo nyingi, lakini pia ni wimbo ambao unapigwa sana kwenye klabu mbalimbali na kila unapopigwa hakuna anayekaa kitini.
Alisema kuwa kufuatia kutoa wimbo huo ameshakusanya Shilingi 16 milioni.
Alisema pamoja na kupata fedha nyingi kupitia wimbo huo bado hajaamua azifanyie nini ila ameamua atulie kwanza akitafakari nini kinafuata.
“Wimbo bado upo juu na unafanya vizuri, hivyo ninachofanya kwa sasa ni kuendelea kukusanya fedha kutokana na shoo ambazo nitapata kutoka kwenye wimbo huo baada ya hapo ndio nitajua nifanyie nini,” alieleza.
Aidha, Madee alisema kuwa anafurahi kuona amefanya kitu ambacho kila mpenda burudani kinamfurahisha kwani sio wasanii wengi ambao wanaweza kufanya kitu kama hicho hasa kwa wale waliopo kwenye usanii kwa muda mrefu. Kalunde Jamal

Tuesday, April 23, 2013

RAIS KIKWETE AKUTANA NA VIONGOZI WA MADHEHEBU MBALIMBALI YA KIKRISTO LEO IKULU

 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mkutano na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini ya Kikristo alipokutana nao leo April 23, 2013 Ikulu jijini Dar es salaam katika kukutana na makundi mbalimbali ya kidini ili kuondoa changamoto za kiimani zilizojitokeza nchini hivi karibuni.
 Raisi akiwa katika picha ya Pamoja na viongozi wa dini mbalimbali
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini ya Kikristo alipokutana nao leo April 23, 2013 Ikulu jijini Dar es salaam katika kukutana na makundi mbalimbali ya kidini ili kuondoa changamoto za kiimani zilizojitokeza nchini hivi karibuni.
PICHA NA IKULU

HII NDIO STYLE MPYA YA NYWELE YA TUNDA MAN

Msanii kutoka kundi la Tip Top Connection maarufu kama Tunda Manameonekana kubadili muonekano wake wa zamani na sasa kuja na mpya ....

Muonekano huo mpya wa style ya nywele zake [pichani] umeonekana kuwashangaza watu kwa jinsi ulivyokuwa wa kipekee ...

Haijafahamika ameutoa wapi na ni kwa ajili gani anautumia, ila hivi ndivyo anavyoonekana sasa Tunda Man kichwani kwake ...

MCHINA AJA NA SIMU MPYA INAYOCHAJIWA KWA SODA

HII NDO SIM INAYOCHAJIWA KWAKUTUMIA SODA YA COCA COLA

Wanasema hii dunia kilichoshindikana ni kumtengeneza binadamu peke yake, kuna vitu vingine ni ngumu kuamini lakini ni ukweli vimetokea, hiyo ni simu ambayo chaji yake inatokana na soda ya Cocacola.

MAAFANDE WACHEZEA NYETI ZA MTUHUMIWA KWA KISINGIZIO CHA UKAGUZI.......!!

Pengine hizi  ndo  starehe  pekee  wanazozipa  "maafande" hasa  wale  wanahusika  na  ulinzi  wa  mageti.....
Miongoni  mwa  majukumu  yao  ni  "kuwapapasa"   na "kuwashika- shika" watu wanaofika  katika  maeneo  hayo  yenye  ulinzi  mkali  ili  kujiridhisha  kwamba  hawana  silaha  au  kitu  chochote  kibaya....
Kinachoshangaza  zaidi  ni  kitendo  cha mafande   kukomaa  na  nyeti  za  akina  mama  wakati  kuna  sehemu  zingine  kibao  za  mwili  ambazo  walitakiwa  wazikague.....
 
Hata  hivyo, kwa  dunia  ya  leo, ukaguzi  kama  huu  umepitwa  na  wakati  kwa  sababu  kuna  vifaa vingi  sana  vya  kitaalam  ambavyo  vinaweza  kufanya  kazi  hizi  badala  ya  maafande  kushinda  wakicheza  na  makalio  ya  watu.
Sourec Gumzo la Jiji

RAIS MASKINI KULIKO WOTE DUNIANI


NCHI ya Uruguay yenye raia takribani milioni 4, inatajwa kuwa na bahati ya kuwa na Rais asiye na chembe ya tamaa. Hana makuu, kiasi kwamba anatajwa kuwa ndiye Rais masikini zaidi kuwahi kutokea duniani.
Huyu si mwingine, bali ni Jose Mujica, Rais wa sasa wa Uruguay ambaye pia ni Rais wa 40 wa nchi hiyo. Tangu aingie madarakani Machi mosi mwaka 2010, amekuwa akionekana kuwa kiongozi wa tofauti kabisa, tofauti na waliomtangulia.
Mathalan, baada ya kufanikiwa kuishika nchini, hakuwa na tamaa ya kukimbilia Ikulu, yeye alichokifanya ni kuamua kuishi katika makazi yake yaleyale, katika nyumba ya mkewe iliyoko shambani, nje ya Jiji la Montevideo.

Kwa ujumla, anapenda maisha ya kawaida, maisha ya kuwahurumia wengine na kujitahidi kuonesha kwa vitendo.
Ni vigumu kuamini, licha ya kuwa ni Rais wa nchi, amejishusha mno kiasi cha mara kadhaa kuonekana akijichanganya na raia wake katika shughuli za ujenzi wa taifa, ikiwamo ujenzi wa barabara, kulima mashamba ya mfano.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...