Thursday, April 25, 2013
Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) amwonya Rais kutoipigia debe CCM.
Mbunge
wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) amemtahadharisha Rais Jakaya
Kikwete asiitumie ziara yake ya Mkoa wa Mbeya kukipigia debe Chama Cha
Mapinduzi(CCM) bali afanye kazi za kiserikali.
Rais Kikwete anatazamiwa kuwasili mkoani Mbeya, Jumapili ijayo kwa ziara ya kikazi ya siku nne.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara jana Mjini Mbeya, Sugu alisema kuwa kitendo hicho kitasaidia kuimarisha umoja miongoni mwa wananchi wa Mbeya.
“Wakazi wa Mbeya muwe tayari kumpokea Rais Kikwete endapo ataifanya ziara yake kuwa ya kiserikali na yeye akiwa ni rais wa nchi na siyo kuifanya ziara hiyo kuwa ya kisiasa kwa vile tu yeye ni mwenyekiti wa CCM,”alisema Sugu.
Wednesday, April 24, 2013
UWOYA KUJIPATI MILIONI 200 ZA BUREEEEE KUTOKA GLOBAL PUBLISHERS BAADA YA KUCHAFULIWA: GLOBAL KUANIKA VIDEO YA TUKIO ZIMA HOTELINI:
Mfano wa sehemu ya fedha atazolipwa Uwoya
DIVA
anayetesa katika sinema za Bongo, Irene Pancras Uwoya ananukia utajiri
ambapo hivi karibuni ‘anatarajia’ kuogelea kwenye mamilioni ya fedha
kwa kukomba Shilingi Milioni 200 za madafu, Risasi Mchanganyiko lina
kila kitu mkobani.Uwoya ni mke halali wa msakata kabumbu wa kulipwa nchini Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ ambapo ndoa yao ilifungwa
mwaka 2009 katika Kanisa Katoloki, Parokia ya Mt. Joseph, Posta jijini Dar es Salaam. KUTOKA DAR ES SALAAM Msanii huyo ambaye hakaukwi na skendo, huenda akaibuka milionea ikithibitika kwamba habari iliyoandikwa na gazeti damu moja na hili, Ijumaa Wikienda la Jumatatu Aprili 8 – 14, toleo namba 310 iliyokuwa na kichwa; UWOYA, DIAMOND WANASWA HOTELINI ni ya uongo. Habari kutoka katika vyanzo vyetu vya kuaminika, zinasema kuwa mdada huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja aitwaye Krish Hamad Ndikumana yu mbioni kuandika barua ya madai kupitia kwa mawakili wake waliopo Dar ili kudai fedha hizo kwa maelezo (eti) alichafuliwa na kuingiliwa faragha yake. |
BINTI ANUSURIKA KUBAKWA BAADA YA KUKATIZA MITAA YA SINZA AKIWA AMEVAA KIMINI
Mwanahabari
wetu mwishoni mwa wiki iliyopita usiku wa manane, alinyetishiwa tukio
la wanawake watatu kuvamiwa na midume na kufanyiwa kitu mbaya baada ya
kuchaniwa vimini vyao maeneo ya Barabara ya Shekilango, Dar kabla ya
kuokolewa na wasamaria wema.
Wasichana hao, wakiwa wamejipodoa vilivyo na kutinga vimini
vilivyoonesha sawia maungo yao nyeti bila ‘makufuli’, walijikuta katika
hali hiyo mbaya baada ya kurushiana maneno na vijana hao wahuni hivyo
wakaonja joto ya jiwe.
Warembo hao ambao walikuwa wakitokea Sinza kuelekea Manzese, Dar
walivamiwa na vijana hao ambao wengi wao ni waendesha pikipiki maarufu
kama bodaboda, walipokaribia Makutano ya Barabara ya Shekilango na
Morogoro, Dar.
“Kila siku wanapita hapa wakiwa nusu utupu, sasa leo tumewakomesha, serikali inatangaza Ukimwi ni hatari, wao hawajali, wanatutia majaribuni,” alisikika akisema mwendesha bodaboda mmoja ambaye alikuwa miongoni mwa waliowavamia wasichana
hao.
Mwendesha bodaboda mwingine alimwambia mwandishi wetu kuwa waliwaeleza wasichana hao kuacha tabia ya kutembea nusu utupu kwani ni hatari kwa maisha yao na ni kinyume cha maadili ya Watanzania lakini walijifanya jeuri ndiyo maana wakawaadabisha.
Aliweka wazi kuwa baada ya kuelezwa hivyo akina dada hao hawakufurahishwa na maneno hayo na badala yake
wakawaporomoshea matusi mazito madereva hao, hali iliyowafanya wapandwe na hasira.
wakawaporomoshea matusi mazito madereva hao, hali iliyowafanya wapandwe na hasira.
“Madereva
wale baada ya kusikia wakitukanwa waliwavamia wasichana hao na kuanza
kuwachania nguo kwa maelezo kwamba badala ya kuwa nusu utupu, ni vema
wakakaa uchi wa mnyama kabisa.
“Warembo wawili walifanikiwa kutimua mbio licha ya kuchaniwa vimini vyao lakini mmoja aliyekuwa na ‘mdomo mchafu’
“Shukrani ziwaendee wasamaria wema waliomukoa kwa sababu kwa vyovyote lazima angebakwa kwani alikuwa ameshachaniwachaniwa nguo na ku... ,” alisema shuhuda mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Shuhuda huyo aliongeza kuwa binti huyo alifanyiwa kitu mbaya kwa kushikwa sehemu nyeti kabla ya wale wenzake waliokimbia kurudi wakiwa kwenye Bajaj na mabaunsa wao kisha kutokomea na mwenzao aliyekuwa amehenyeshwa vya kutosha na wanaume
hao.
“Wale wasichana wawili walirudi wakiwa na Bajaj na mabaunsa, wakasaidiwa na raia wema ndipo wakafanikiwa kumuokoa mwenzao na kutokomea naye kusikojulikana,” alisema shuhuda huyo.
Credit: GPL
SUALA LA JUMA NATURE KUTIMULIWA CHANNEL 5 ALIPOINGIA NA NDALA LACHUKUA SURA MPYA ....
Kitendo cha mtangazaji wa EATV Sam Misago kumtoa nje ya studio Sir Juma Nature weekend iliyopita baada ya kwenda studio kwenye kipindi cha Saturday Night Live akiwa na ndala na kaoshi, hajakichukulia poa staa huyo.
Licha
ya kuwasilisha malalamiko yake kwenye Facebook kutokana na kitendo
hicho, Nature hajaishia hapo na sasa amemchana mtangazaji wa kipindi
hicho kwenye wimbo mpya wa TMK Halisi, Fitina.
Katika wimbo huo Nature anachana, “Halafu
watu wengine sijui wanakuwaga ni mapimbi, eti msanii kaingia studio na
ndala na amevaa pensi hakujua anayosema kwenye Facebook na Twitter
sijui kisa hela alizopewa na mameneja feki wasiopenda wa Uswazi,
mzomeeni huyo, sasa kazi kwake na raia wake.”
Mdogo wa Wema aibukia Redds Miss Hai.
WAREMBO
14 kutoka vitongoji vitano vya wilaya za Siha na Hai, Kilimanjaro,
akiwemo mdogo wake Wema Sepetu, wamejitokeza kushiriki shindano la
kumsaka mrembo wa Hai, ‘Redds Miss Hai 2013.
Shindano
hilo linalotarajiwa kulindima Hoteli ya Snow View Bomang’ombe Hai,
Ijumaa.Akizungumza mjini hapa jana, muandaaji wa mashindano hayo,
Grace
Mmari,
kupitia kampuni ya ulinzi ya FEM ya jijini Arusha, alisema maandalizi
ya mashindano hayo yamekamilika na tayari warembo hao wako kambini kwa
wiki mbili sasa katika hoteli ya Sinza B.
Alisema
warembo hao wamepatikana kutoka vitongoji vya Kwa Sadala, Bomang’ombe,
Sanya Juu, Machame na KIA, ambao wana vigezo vyote huku akitamba mwaka
huu, Mrembo wa Tanzania atatoka wilaya ya Hai.
“Warembo
wangu ni wazuri, warefu, wanajiamini na wana uwezo wa kuwakilisha
vyema wilaya ya Hai, mkoa wa Kilimanjaro na hata taifa, kwa kuwa tunao
kina Wolper wengine hapa na kina Sepetu wapo pia,“ alisema.
Alisema
miongoni mwa warembo waliojitokeza kushiriki shindano hilo ni pamoja
na mdogo wa mrembo wa zamani wa Miss Tanzania (2006), Wema Sepetu, Weru
Sepetu, ambaye alidai kuwa huenda akafuata nyayo za dada yake.
Aliwataja
warembo watakaoshiriki shindano hilo kuwa ni Sharon Abdalah, Zena
Ally, Ivony Steven, na Winny Shayo wanaotoka Machame na Sanya Juu.
Wengine ni Julieth Kimaro, Rehema John, Mary Chemponda, Catherine Leonard na Modesta Joseph.
Mmari
alisema shindano hilo litapambwa na msanii wa muziki wa kizazi kipya,
Rich Mavoko pamoja na Jambo Squad, ambako mgeni rasmi anatarajiwa kuwa
Mkuu wa Wilaya ya Hai, Novatus Makunga.
Kwa
upande wake, mwalimu wa warembo hao, Evameri Gamba, alisema warembo
wanaendelea na mazoezi ya mwisho pamoja na kushiriki shughuli
mbalimbali za kijamii, ikiwemo uoteshaji wa miti na kutembelea wagonjwa
katika hospitali ya wilaya ya Hai.
Shindano hilo linafanyika kwa mara ya pili sasa, huku wadhamini wakiwa
ni TBL kupitia kinywaji chake cha Redds, Fem Security, Bonite
Bottlers, Snow View Hotel, Panone pamoja migodi ya madini ya Anglo
America Mining na Manga Germ.
Zitto Kabwe atoa majibu kwa Umma kuhusu Habari za mama yake Mzazi Bi. Shida kuvamiwa na kutishiwa bastola.
Mh.Zitto Kabwe.
Nimekuwa naulizwa kuhusu Habari za mama yangu Mzazi Bi. Shida kuvamiwa na kutishiwa bastola. Nawajibu watu Kwa ujumla kwamba
“Moja,
mie sio msemaji wa familia. Ni basi tu katika watoto wa mama yetu mie
najulikana zaidi na hivyo mama anaitwa Mama Zitto. Kwetu Kigoma haitwi
hivyo, ama Ni mama Salum au mama Lulu.
Pili,
hili Ni suala la polisi. Lipo polisi na linashughulikiwa na polisi.
Nisingependa kulisemea wakati Ni suala linalochunguzwa na polisi. Mama
yangu Ni mama wa kawaida wa kitanzania kama mama mwingine yeyote yule.
Matukio ya namna hii yamezagaa nchi nzima. Hivyo suala lake
litashughulikiwa kama yanavyoshughulikiwa masuala mengine yote ya
Watanzania. Polisi wakimaliza uchunguzi wao naamini hatua mwafaka
zitachukuliwa.
Ushauri-
tuwe makini na “Agente provocatuers” au in English “provocation agents”
nyakati kama hizi. Calmness is the best protection against
provocations. Nadhani mmenipata”
Nawatakia
Kila la kheri katika kazi za ujenzi wa Taifa letu na kuimarisha Umoja
na mshikamano wa Watanzania dhidi ya ufisadi, umasikini na ugandamizaji.
Majibu haya ameandika kupitia mtandao wa Kijamii wa facebook.
POMBE YAMTOA MADEE...ANADAI IMEMPA HESHIMA KUBWA MTAANI......!!
Msanii wa Kundi la Tip Top Connection, Madee au Rais wa Manzese ameeleza kuwa wimbo wake wa Nani Kamwaga Pombe Yangu umempa heshima kubwa.
Akiongea
na mwandishi wetu, Madee, ambaye jina lake halisi ni Hamad Ally
Seneda alisema licha ya kupata shoo nyingi, lakini pia ni wimbo ambao
unapigwa sana kwenye klabu mbalimbali na kila unapopigwa hakuna anayekaa
kitini.
Alisema kuwa kufuatia kutoa wimbo huo ameshakusanya Shilingi 16 milioni.
Alisema
pamoja na kupata fedha nyingi kupitia wimbo huo bado hajaamua
azifanyie nini ila ameamua atulie kwanza akitafakari nini kinafuata.
“Wimbo
bado upo juu na unafanya vizuri, hivyo ninachofanya kwa sasa ni
kuendelea kukusanya fedha kutokana na shoo ambazo nitapata kutoka
kwenye wimbo huo baada ya hapo ndio nitajua nifanyie nini,” alieleza.
Aidha,
Madee alisema kuwa anafurahi kuona amefanya kitu ambacho kila mpenda
burudani kinamfurahisha kwani sio wasanii wengi ambao wanaweza kufanya
kitu kama hicho hasa kwa wale waliopo kwenye usanii kwa muda mrefu.
Kalunde Jamal
Tuesday, April 23, 2013
RAIS KIKWETE AKUTANA NA VIONGOZI WA MADHEHEBU MBALIMBALI YA KIKRISTO LEO IKULU
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mkutano na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini ya Kikristo alipokutana nao leo April 23, 2013 Ikulu jijini Dar es salaam katika kukutana na makundi mbalimbali ya kidini ili kuondoa changamoto za kiimani zilizojitokeza nchini hivi karibuni.
Raisi akiwa katika picha ya Pamoja na viongozi wa dini mbalimbali
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini ya Kikristo alipokutana nao leo April 23, 2013 Ikulu jijini Dar es salaam katika kukutana na makundi mbalimbali ya kidini ili kuondoa changamoto za kiimani zilizojitokeza nchini hivi karibuni.
PICHA NA IKULU
HII NDIO STYLE MPYA YA NYWELE YA TUNDA MAN
Msanii
kutoka kundi la Tip Top Connection maarufu kama Tunda Manameonekana
kubadili muonekano wake wa zamani na sasa kuja na mpya ....
Muonekano huo mpya wa style ya nywele zake [pichani] umeonekana kuwashangaza watu kwa jinsi ulivyokuwa wa kipekee ...
Haijafahamika ameutoa wapi na ni kwa ajili gani anautumia, ila hivi ndivyo anavyoonekana sasa Tunda Man kichwani kwake ...
MCHINA AJA NA SIMU MPYA INAYOCHAJIWA KWA SODA
HII NDO SIM INAYOCHAJIWA KWAKUTUMIA SODA YA COCA COLA
Wanasema
hii dunia kilichoshindikana ni kumtengeneza binadamu peke yake, kuna
vitu vingine ni ngumu kuamini lakini ni ukweli vimetokea, hiyo ni simu
ambayo chaji yake inatokana na soda ya Cocacola.
MAAFANDE WACHEZEA NYETI ZA MTUHUMIWA KWA KISINGIZIO CHA UKAGUZI.......!!
Pengine hizi ndo starehe pekee wanazozipa "maafande" hasa wale wanahusika na ulinzi wa mageti.....
Miongoni
mwa majukumu yao ni "kuwapapasa" na "kuwashika- shika" watu
wanaofika katika maeneo hayo yenye ulinzi mkali ili
kujiridhisha kwamba hawana silaha au kitu chochote kibaya....
Kinachoshangaza
zaidi ni kitendo cha mafande kukomaa na nyeti za akina mama
wakati kuna sehemu zingine kibao za mwili ambazo walitakiwa
wazikague.....
Hata
hivyo, kwa dunia ya leo, ukaguzi kama huu umepitwa na wakati
kwa sababu kuna vifaa vingi sana vya kitaalam ambavyo vinaweza
kufanya kazi hizi badala ya maafande kushinda wakicheza na
makalio ya watu.
Sourec Gumzo la Jiji
RAIS MASKINI KULIKO WOTE DUNIANI
NCHI ya Uruguay yenye raia takribani
milioni 4, inatajwa kuwa na bahati ya kuwa na Rais asiye na chembe ya
tamaa. Hana makuu, kiasi kwamba anatajwa kuwa ndiye Rais masikini zaidi
kuwahi kutokea duniani.
Huyu si mwingine, bali ni Jose Mujica,
Rais wa sasa wa Uruguay ambaye pia ni Rais wa 40 wa nchi hiyo. Tangu
aingie madarakani Machi mosi mwaka 2010, amekuwa akionekana kuwa
kiongozi wa tofauti kabisa, tofauti na waliomtangulia.
Mathalan, baada ya kufanikiwa kuishika
nchini, hakuwa na tamaa ya kukimbilia Ikulu, yeye alichokifanya ni
kuamua kuishi katika makazi yake yaleyale, katika nyumba ya mkewe
iliyoko shambani, nje ya Jiji la Montevideo.
Kwa ujumla, anapenda maisha ya kawaida, maisha ya kuwahurumia wengine na kujitahidi kuonesha kwa vitendo.
Ni vigumu kuamini, licha ya kuwa ni Rais
wa nchi, amejishusha mno kiasi cha mara kadhaa kuonekana akijichanganya
na raia wake katika shughuli za ujenzi wa taifa, ikiwamo ujenzi wa
barabara, kulima mashamba ya mfano.
WALIMU WAPIGWA MAWE NA WANAFUNZI WA SHULE YA MIZENGO PINDA KWA MADAI KUWA NI WACHAWI
WANAFUNZI
wa shule ya sekondari ya Mizengo Pinda kata ya Kibaoni Wilayani Mlele
mkoani Katavi, wamemshambulia kwa mawe na matofali mkuu wa shule hiyo
na mwalimu wa taaluma na kuharibu jengo la utawala na nyumba za walimu
hao baada ya kuwatuhumu walimu hao kuwa ni washirikina.
Kaimu
kamanda wa polisi wa mkoa wa katavi, Joseph Myovela, alisema tukio hilo
limetokea juzi saa 2:30 usiku shuleni hapo baada ya kuzuka kwa tafrani
iliyodumu kwa zaidi ya saa 1:30.
Habari
kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa chanzo cha tukio hilo kilitokana na
mwanafunzi mmoja aitwaye Jofley Pinda kushikwa na ugonjwa wa mapepo
uliomfanya aanguke chini ambapo tukio hilo lilitokea mchana wa saa saba.
Alisema
wakati akiwa ameshikwa na mapepo hayo aliwataja Alico Kamyoge (36)
ambaye ni Mkuu wa shule hiyo ya sekondari ya Mizengo Pinda na mwalimu wa
taaluma Bonifasi Nsalamba (35) kuwa ndio wamemroga ugonjwa huu wa
mapepo.
Subscribe to:
Posts (Atom)