WANAFUNZI
wa shule ya sekondari ya Mizengo Pinda kata ya Kibaoni Wilayani Mlele
mkoani Katavi, wamemshambulia kwa mawe na matofali mkuu wa shule hiyo
na mwalimu wa taaluma na kuharibu jengo la utawala na nyumba za walimu
hao baada ya kuwatuhumu walimu hao kuwa ni washirikina.
Kaimu
kamanda wa polisi wa mkoa wa katavi, Joseph Myovela, alisema tukio hilo
limetokea juzi saa 2:30 usiku shuleni hapo baada ya kuzuka kwa tafrani
iliyodumu kwa zaidi ya saa 1:30.
Habari
kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa chanzo cha tukio hilo kilitokana na
mwanafunzi mmoja aitwaye Jofley Pinda kushikwa na ugonjwa wa mapepo
uliomfanya aanguke chini ambapo tukio hilo lilitokea mchana wa saa saba.
Alisema
wakati akiwa ameshikwa na mapepo hayo aliwataja Alico Kamyoge (36)
ambaye ni Mkuu wa shule hiyo ya sekondari ya Mizengo Pinda na mwalimu wa
taaluma Bonifasi Nsalamba (35) kuwa ndio wamemroga ugonjwa huu wa
mapepo.